STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,770
- 553
Kwa kawaida - na karibu mara zote - shujaa wa kwenye filamu hauawi. Hata apitie matatizo kiasi gani tunajua kuwa mwisho wa siku shujaa wetu ataendelea kuwepo. Ndio maana ya ule msemo wa "sterling hauawi". Lakini kuna kitu kingine ambacho ni kweli pia, shujaa hatokei mwisho wa movie! Hata kama atachelewa kidogo kutokea lakini mara moja tutatambulishwa kuwa huyu ni shujaa wetu na toka mwanzo tutamuona anvyopambana na mgogoro. Fikiria shows kama 24 au filamu kama za Rambo, n.k
Sasa inakuwaje kwenye filamu uangalie hadi mwisho hadi kisa kimekwisha halafu shujaa anatokea? Fikiria kuwa umeangalia movie nzima na matukio yote muhimu yametokea na filamu imeshaandikwa "the end" halafu credits zina roll down halafu shujaa anatokea na kuanza kuelezea jinsi ambavyo angeweza kupambana na maadui au jinsi gani maadui walivyoshindwa! Kwanza itabidi ujiulize kama ni shujaa kweli na kama ni shujaa basi unajiuliza ni shujaa wa kitu gani!
Nilichojifunza ni kuwa shujaa hatokei mwisho wa filamu kupewa sifa!
MMM
Well said MMM, I wish hii tafsiri waTZ wote wangeielewa vizuri hata mhusika mkuu wa hii muvi, wacheza muvi na wote wanaoingalia hii muvi...