Shujaa anapotokea mwisho wa filamu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kwa kawaida - na karibu mara zote - shujaa wa kwenye filamu hauawi. Hata apitie matatizo kiasi gani tunajua kuwa mwisho wa siku shujaa wetu ataendelea kuwepo. Ndio maana ya ule msemo wa "sterling hauawi". Lakini kuna kitu kingine ambacho ni kweli pia, shujaa hatokei mwisho wa movie! Hata kama atachelewa kidogo kutokea lakini mara moja tutatambulishwa kuwa huyu ni shujaa wetu na toka mwanzo tutamuona anvyopambana na mgogoro. Fikiria shows kama 24 au filamu kama za Rambo, n.k

Sasa inakuwaje kwenye filamu uangalie hadi mwisho hadi kisa kimekwisha halafu shujaa anatokea? Fikiria kuwa umeangalia movie nzima na matukio yote muhimu yametokea na filamu imeshaandikwa "the end" halafu credits zina roll down halafu shujaa anatokea na kuanza kuelezea jinsi ambavyo angeweza kupambana na maadui au jinsi gani maadui walivyoshindwa! Kwanza itabidi ujiulize kama ni shujaa kweli na kama ni shujaa basi unajiuliza ni shujaa wa kitu gani!

Nilichojifunza ni kuwa shujaa hatokei mwisho wa filamu kupewa sifa!

MMM
 
Nionavyo mimi huyo ni mcheza shoo,anangoja mpaka watu waanze kusinzia ndo anzishe manjonjo ya kuwaamsha ili mradi awe kinara kati ya wacheza shoo wenzie.na mtu namna hii kwa michezo ndo mwenyewe
 
Kwa vile movies ni sanaa na zinaendeshwa kwa kanuni za usanii, basi labda inawezeka!!

Je, kila kitu ni usanii??


Babu DC!!
 
ni kweli muu shujaa hakwepi majukumu ya kusonga mbele anatakiwa mwanzo mwisho ... hata movie za kihidi shujaa hujulikana ndotoni
 
Ha ha ha!huyu shujaa atakuwa JK na movie ya DOCTORS!!

no nafikiri huyu shujaa atakuwa ni yule aliyewapola mali characters wengine wakati movie liko hewani alafu baada ya THE END anataka kuwarudishia mali zao!
 
...hiyo itakuwa ni style mpya ya utengenezaji wa movie...kumbuka "TANZANIA HAKUNA KISICHO WEZEKANA"...
 
Shujaa wetu alikuwa mchezaji wa akiba akaingia baada ya filimbi ya mwisho na kujitangazia ushindi.
 
Hii imezidi hata filamu za kihindi maana hata kama ni kudanganya uhusika hapa umezidi
Huyu shujaa wa makaratasi kabisa
 
Shujaa infact aliibukuia kwenye premiere ya movie.............aka sign autographies za washabiki
 
Umeamua kufurahisha Jamvi eeenh? Hapo ndipo ninapokushangaa MM. Utasemaje sterling katokea mwishoni,picha imekwisha, wakati unajua fika wale jamaa walitususia zile ofisi kwa muda usiojulikana, (potelea mbali hata tungekufa Watz. wakabakia wao tu), hadi waliposhikwa na kiu, wakaenda kupata juice pale kwa huyo sterling, ndipo Watz. tukarudishiwa zile huduma muhimu? Ulikuwa Ulaya mwenzetu hukuona?
 
...mmm! hapa inaonekana shujaa nae alikuwa upande wa watazamaji,akashtuka movie imesha na yeye ndo akajitokeza...
 
Umeamua kufurahisha Jamvi eeenh? Hapo ndipo ninapokushangaa MM. Utasemaje sterling katokea mwishoni,picha imekwisha, wakati unajua fika wale jamaa walitususia zile ofisi kwa muda usiojulikana, (potelea mbali hata tungekufa Watz. wakabakia wao tu), hadi waliposhikwa na kiu, wakaenda kupata juice pale kwa huyo sterling, ndipo Watz. tukarudishiwa zile huduma muhimu? Ulikuwa Ulaya mwenzetu hukuona?

Wacha kusema uwongo,hakuna aliyekunywa juice,alikunywa sterling tu

8E9U2768.JPG
 
Back
Top Bottom