Show ya Lema vs Pinda featuring Makinda

chidide

Member
Nov 11, 2010
91
9
Soma hii ya Deus, Tanzania Daima, nimeipenda;

FEBRUARI 10 mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari, kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Jambo hili lilitokea baada ya Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (CHADEMA), kuomba apewe mwongozo wa spika “kuhusu utaratibu” aliohisi unakiukwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, wakati akitoa maelezo kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha Januari 5, mwaka huu.

Pinda alizungumzia vurugu hizo za Arusha wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua serikali ina msimamo gani kuhusu mauaji ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi wakati wa vurugu hizo.

Akijibu swali la Mbowe, Pinda alilieleza Bunge kwamba chanzo asilia cha vurugu hizo ni uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa umeya mjini Arusha, wakati “utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa”, kwa maana kwamba “Meya wa Arusha yupo kihalali.”

Kufuatia kauli hiyo na zingine zinazofanana nayo, Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika “kuhusu utaratibu” wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mbunge wa kawaida endapo kiongozi mkubwa wa nchi kama Waziri Mkuu amelidanganya Bunge.

Baada ya kuombwa mwongozo huo, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, Spika Makinda alisema: “Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; waziri mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?”

Kisha, Spika alimpa siku tatu Lema ili awasilishe kwa maandishi utetezi wake wa kuthibitisha kwamba waziri mkuu alisema “uongo” bungeni siku hiyo.

Katika muktadha huu, tunakusudia kufanya mambo mawili. Kwanza ni kuonyesha kwamba ni kweli kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema uongo bungeni ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Na pili tunataka kuonyesha kwamba, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema.

Waziri Mkuu alisema uongo: Meya wa Arusha si halali
Kwa lengo la kuonyesha kwamba Waziri Mkuu alisema uongo bungeni, inatosha kutoa ushahidi utakaokanusha usemi ufuatao kama ulivyotolewa naye bungeni: Kwamba, “Utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa”, kwa maana kwamba “Meya wa Arusha yupo kihalali.”

Hapa inatosha kabisa kuonyesha kwamba miongoni mwa wajumbe waliompigia kura ya ndiyo “Meya wa Arusha”, yupo angalau mjumbe mmoja ambaye hakuwa na haki ya kisheria ya kuingia na kupiga kura hiyo. Na huyo si mwingine, bali ni Mary Pius Chatanda, ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Mkoa wa Tanga. Utetezi unafuata.

Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya “Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) ” (Local Governments (Urban Authorities) Act) ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda atakuwa ni mjumbe mwenye sifa ya kisheria ya kupiga kura katika vikao vya Manispaa ya Arusha kama atatimiza sifa mojawapo kati ya sifa tano zifuatazo:

Kwanza, lazima awe ni miongoni mwa madiwani ambao ni “wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(a)). Chatanda hakuwa miongoni mwa madiwani ambao ni “wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa meya wa Arusha.

Pili, lazima awe ni “mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana” (Tazama ibara ya 19(2)(b)). Chatanda hakuwa “mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Tatu, lazima awe ni “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana” na kwa mpigo awe “ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(c)). Chatanda hakuwa “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Nne, lazima awe ni “Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais” na kwa mpigo awe “ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(d)). Chatanda hakuwa “Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Na tano, lazima awe ni miongoni mwa “wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI ambaye katika uteuzi wake [amezingatia] makundi maalumu kama vile watu wenye ujuzi maalum, watu waliotelekezwa na watu walio katika mazingira magumu.” (Tazama ibara ya 19(2)(e)). Chatanda hakuwa miongoni mwa “wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Hivyo basi, Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya “Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji)” ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda hakuwa na sifa yoyote ya kisheria ya kuingia katika kikao cha Manispaa ya Arusha na kupiga kura kama alivyofanya. Baraka za chama chake haziwezi na hazipaswi kubatilisha sheria za nchi.

Tena tusifananishe uwepo wa Mary Pius Chatanda na uwepo wa Rebecca Mngodo katika kikao kilichofanya uchaguzi wa Meya wa Arusha. Kufanya hivyo ni kufananisha maembe na machungwa. Mngodo ni mbunge viti maalumu aliyepatikana kupitia mkoa wa Arusha kupitia CHADEMA. Na hatimaye alipangiwa kazi na chama chake kufanyia kazi katika Mkoa wa Arusha. Kwa hiyo alikuwa na sifa zote za kisheria za kuwemo katika kikao kile.

Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema
Na sasa, tuone ni kwa nini Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema. Kabla ya spika kumnyima mwongozo “kuhusu utaratibu” wa kikanuni, spika alipaswa kufanya tafakari kadhaa kuhusu Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi yetu.

Kwanza, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(1) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za siku hadi siku zinazofanywa na vyombo vya dola katika Jamhuri nzima. Pili, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(2) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni “Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni”.

Tatu, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 62(2) na 66(1) za Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni mjumbe halali katika vikao vya bunge kupitia kofia yake kama mbunge wa kuchaguliwa.

Nne, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Waziri Mkuu (Mizengo Pinda), kama ilivyo kwa Mbunge mwingine yeyote, anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha tu.

Tano, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(3) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema) anaweza kusimama mahali pake na kuomba mwongozo “kuhusu utaratibu” uliokiukwa bungeni; na kwamba baada ya kuruhusiwa na Spika, anaaweza kudai kwamba, Mbunge aliyekuwa anasema kabla yake (kama vile Mizengo Pinda) ametoa maelezo ya uwongo kuhusu jambo au suala alilokuwa analisema bungeni.

Sita, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge anayeomba mwongozo “kuhusu utaratibu” uliokiukwa bungeni (kama vile Godbless Lema alivyofanywa), atakuwa na wajibu wa kutoa na kuthibitisha ukweli kuhusu jambo au suala hilo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge.

Saba, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(5) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika au Mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema), baada ya kutoa maelezo mafupi ya ushahidi unaotilia mashaka ya dhahiri kuhusu ukweli wa kauli juu ya jambo ambalo mbunge mwingine (kama vile Mizengo Pinda) amelisema Bungeni, anaweza kumdai Mbunge huyo (Mizengo Pinda), ambaye kauli yake inatiliwa shaka, atoe uthibitisho wa ukweli wa kauli yake na kama atashindwa kufanya hivyo, afute maelezo yake hayo.

Nane, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(6) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha ukweli wa kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda), atawajibika kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, papo hapo au katika muda atakaopewa na Spika kwa ajili ya kufanya hivyo.

Tisa, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(7) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda) atashindwa kufanya hivyo, anaweza kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake hayo, papo hapo au katika muda atakaokuwa amepewa na Spika kwa ajili ya kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake.

Na kumi, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(8) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, Mbunge aliyetakiwa kutoa uthibitisho wa ukweli wa kauli yake aliyoitoa bungeni (Mizengo Pinda) atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, na kama atakataa kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake, basi Spika atamwadhibu kwa kumsimamisha Mbunge huyo (Mizengo Pinda) asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.

Hivyo ndivyo Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) zinavyosomeka. Na huu ndio mwongozo aliopaswa kuutoa Spika Makinda. Lakini, baada ya kuombwa mwongozo husika, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, akaona kwamba ombi hilo ni utovu wa “adabu” wa “hali ya juu”. Kwa maneno yake mwenyewe, Spika alisema, “Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; Waziri Mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?”

Kwa hakika, lazima hapa tukubaliane kwamba spika alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Aliombe radhi Bunge na taifa kwa ujumla.

Simu: 0758341483/0684175182
Email: deus.jovin@gmail.com
 
Hata tukiacha hii, Pinda kisaha lidanyanya Bunge mara kadhaa -- moja ni pale alipoliambia kuwa mkataba kati ya serikali na RITES umevunjwa, kumbe bado kama alivyosema Wzaziri wa Mawasiliano Nundu alipokyutana na wafarnyakazi wa TRL wiki iliyopita.

Nundu aliumbuka pale mmoja wa wafanyakazi alimtolea kavu kavu kwamba mbona Pinda alisema mkataba ulivunjwa? Waziri akawa anakenua meno tu na kutizama chini.

Ingawa hizo 'danganya' zingine za pindi hazihusu suyalka hili, lakini linaonyesha jinsi kiongozi huyo mkuu wa shughuli za kiserikali alivyo muongo aliyebobea.

Lakini nafikiri kama kawaida yake, Makinda na Pinda watategemea tu uwingi wa Wabunge wa CCM kwani hawa wengi ni "yes' men.
 
Tunasubiri mkuu, yaani hapo patamu. Ndo kwanza kikao kimeanza, inabidi mtoto wa mkulima ajiuzuru nafasi yake kwani sina mimi sina imani naye. Ni mtazamo wangu.
 
Ni dhahiri pinda atakuwa amesema uongo,lakini kwa kuwapa maziwa haya mapema,wanataanza kuangalia jinsi ya kuchakachua huo ushahidi!
 
Pinda hana principles kabisa -- yupo yupo tu. Hawezi kujiuzulu, pamoja nakwamba ni vyema angejiuzulu.
 
Na vipi kuhusu spika anapodanganya je mbunge anaweza kuomba muongozo wa spika na kanuni inasemaje ju hilo kwani naonapia anna makinda kalidanganya bunge
 
ukweli unabaki pale pale waziright mkuu hajalidanganya bunge na hawezi kudanganya kwani katika uchaguzi wa wilaya ya hai chedema imemtumia mbunge ambaye siyo mkazi wa halimashauri hiyo
 
Kwa pInda hii ni rahisi: akibanwa sana anamwaga chozi, wabunge wanamhurumia, wanasahau madhambi yake, maisha yanaendelea..

Machozi juu:clap2:
 
ukweli unabaki pale pale waziright mkuu hajalidanganya bunge na hawezi kudanganya kwani katika uchaguzi wa wilaya ya hai chedema imemtumia mbunge ambaye siyo mkazi wa halimashauri hiyo

Mkuu hapo kwenye bold naomba ufafanue..., yeye anauwezo upi ambao binadamu wengine hawana ?
 
ukweli unabaki pale pale waziright mkuu hajalidanganya bunge na hawezi kudanganya kwani katika uchaguzi wa wilaya ya hai chedema imemtumia mbunge ambaye siyo mkazi wa halimashauri hiyo

Kwenye red: hawezi kwa sababu ni malaika au kwa sababu gani? Hoja ya waziri mkuu kutoweza kudanganya inawezekana? unaweza kusema hakudanganya lakini siyo hawezi kudanganya. Ndugu yangu hapo uelewe kuwa ulichosema hakina maana
 
ukweli unabaki pale pale waziright mkuu hajalidanganya bunge na hawezi kudanganya kwani katika uchaguzi wa wilaya ya hai chedema imemtumia mbunge ambaye siyo mkazi wa halimashauri hiyo

Watu wengine vilaza kweli kweli, mpaka mlishwe: Tatu, lazima awe ni “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana” na kwa mpigo awe “ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(c)). Chatanda hakuwa “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana”. Wa Chadema anatoka mkoa wa Arusha.
 
Soma hii ya Deus, Tanzania Daima, nimeipenda;
amka2.gif

FEBRUARI 10 mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari, kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Jambo hili lilitokea baada ya Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (CHADEMA), kuomba apewe mwongozo wa spika "kuhusu utaratibu" aliohisi unakiukwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, wakati akitoa maelezo kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha Januari 5, mwaka huu.
Pinda alizungumzia vurugu hizo za Arusha wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua serikali ina msimamo gani kuhusu mauaji ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi wakati wa vurugu hizo.
Akijibu swali la Mbowe, Pinda alilieleza Bunge kwamba chanzo asilia cha vurugu hizo ni uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa umeya mjini Arusha, wakati "utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa", kwa maana kwamba "Meya wa Arusha yupo kihalali."
Kufuatia kauli hiyo na zingine zinazofanana nayo, Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika "kuhusu utaratibu" wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mbunge wa kawaida endapo kiongozi mkubwa wa nchi kama Waziri Mkuu amelidanganya Bunge.
Baada ya kuombwa mwongozo huo, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, Spika Makinda alisema: "Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; waziri mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?"
Kisha, Spika alimpa siku tatu Lema ili awasilishe kwa maandishi utetezi wake wa kuthibitisha kwamba waziri mkuu alisema "uongo" bungeni siku hiyo.
Katika muktadha huu, tunakusudia kufanya mambo mawili. Kwanza ni kuonyesha kwamba ni kweli kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema uongo bungeni ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Na pili tunataka kuonyesha kwamba, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema.
Waziri Mkuu alisema uongo: Meya wa Arusha si halali
Kwa lengo la kuonyesha kwamba Waziri Mkuu alisema uongo bungeni, inatosha kutoa ushahidi utakaokanusha usemi ufuatao kama ulivyotolewa naye bungeni: Kwamba, "Utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa", kwa maana kwamba "Meya wa Arusha yupo kihalali."

Hapa inatosha kabisa kuonyesha kwamba miongoni mwa wajumbe waliompigia kura ya ndiyo "Meya wa Arusha", yupo angalau mjumbe mmoja ambaye hakuwa na haki ya kisheria ya kuingia na kupiga kura hiyo. Na huyo si mwingine, bali ni Mary Pius Chatanda, ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Mkoa wa Tanga. Utetezi unafuata.
Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya "Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) " (Local Governments (Urban Authorities) Act) ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda atakuwa ni mjumbe mwenye sifa ya kisheria ya kupiga kura katika vikao vya Manispaa ya Arusha kama atatimiza sifa mojawapo kati ya sifa tano zifuatazo:
Kwanza, lazima awe ni miongoni mwa madiwani ambao ni "wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]" (Tazama ibara ya 19(2)(a)). Chatanda hakuwa miongoni mwa madiwani ambao ni "wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]". Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa meya wa Arusha.
Pili, lazima awe ni "mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana" (Tazama ibara ya 19(2)(b)). Chatanda hakuwa "mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana". Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Tatu, lazima awe ni "Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana" na kwa mpigo awe "ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]" (Tazama ibara ya 19(2)(c)). Chatanda hakuwa "Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana". Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Nne, lazima awe ni "Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais" na kwa mpigo awe "ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]" (Tazama ibara ya 19(2)(d)). Chatanda hakuwa "Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais". Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Na tano, lazima awe ni miongoni mwa "wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI ambaye katika uteuzi wake [amezingatia] makundi maalumu kama vile watu wenye ujuzi maalum, watu waliotelekezwa na watu walio katika mazingira magumu." (Tazama ibara ya 19(2)(e)). Chatanda hakuwa miongoni mwa "wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.
Hivyo basi, Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya "Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji)" ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda hakuwa na sifa yoyote ya kisheria ya kuingia katika kikao cha Manispaa ya Arusha na kupiga kura kama alivyofanya. Baraka za chama chake haziwezi na hazipaswi kubatilisha sheria za nchi.
Tena tusifananishe uwepo wa Mary Pius Chatanda na uwepo wa Rebecca Mngodo katika kikao kilichofanya uchaguzi wa Meya wa Arusha. Kufanya hivyo ni kufananisha maembe na machungwa. Mngodo ni mbunge viti maalumu aliyepatikana kupitia mkoa wa Arusha kupitia CHADEMA. Na hatimaye alipangiwa kazi na chama chake kufanyia kazi katika Mkoa wa Arusha. Kwa hiyo alikuwa na sifa zote za kisheria za kuwemo katika kikao kile.
Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema
Na sasa, tuone ni kwa nini Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema. Kabla ya spika kumnyima mwongozo "kuhusu utaratibu" wa kikanuni, spika alipaswa kufanya tafakari kadhaa kuhusu Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi yetu.

Kwanza, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(1) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za siku hadi siku zinazofanywa na vyombo vya dola katika Jamhuri nzima. Pili, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(2) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni "Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni".
Tatu, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 62(2) na 66(1) za Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni mjumbe halali katika vikao vya bunge kupitia kofia yake kama mbunge wa kuchaguliwa.
Nne, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Waziri Mkuu (Mizengo Pinda), kama ilivyo kwa Mbunge mwingine yeyote, anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha tu.
Tano, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(3) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema) anaweza kusimama mahali pake na kuomba mwongozo "kuhusu utaratibu" uliokiukwa bungeni; na kwamba baada ya kuruhusiwa na Spika, anaaweza kudai kwamba, Mbunge aliyekuwa anasema kabla yake (kama vile Mizengo Pinda) ametoa maelezo ya uwongo kuhusu jambo au suala alilokuwa analisema bungeni.
Sita, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge anayeomba mwongozo "kuhusu utaratibu" uliokiukwa bungeni (kama vile Godbless Lema alivyofanywa), atakuwa na wajibu wa kutoa na kuthibitisha ukweli kuhusu jambo au suala hilo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge.
Saba, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(5) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika au Mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema), baada ya kutoa maelezo mafupi ya ushahidi unaotilia mashaka ya dhahiri kuhusu ukweli wa kauli juu ya jambo ambalo mbunge mwingine (kama vile Mizengo Pinda) amelisema Bungeni, anaweza kumdai Mbunge huyo (Mizengo Pinda), ambaye kauli yake inatiliwa shaka, atoe uthibitisho wa ukweli wa kauli yake na kama atashindwa kufanya hivyo, afute maelezo yake hayo.
Nane, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(6) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha ukweli wa kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda), atawajibika kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, papo hapo au katika muda atakaopewa na Spika kwa ajili ya kufanya hivyo.
Tisa, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(7) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda) atashindwa kufanya hivyo, anaweza kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake hayo, papo hapo au katika muda atakaokuwa amepewa na Spika kwa ajili ya kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake.
Na kumi, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(8) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, Mbunge aliyetakiwa kutoa uthibitisho wa ukweli wa kauli yake aliyoitoa bungeni (Mizengo Pinda) atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, na kama atakataa kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake, basi Spika atamwadhibu kwa kumsimamisha Mbunge huyo (Mizengo Pinda) asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.
Hivyo ndivyo Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) zinavyosomeka. Na huu ndio mwongozo aliopaswa kuutoa Spika Makinda. Lakini, baada ya kuombwa mwongozo husika, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, akaona kwamba ombi hilo ni utovu wa "adabu" wa "hali ya juu". Kwa maneno yake mwenyewe, Spika alisema, "Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; Waziri Mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?" Kwa hakika, lazima hapa tukubaliane kwamba spika alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Aliombe radhi Bunge na taifa kwa ujumla.

h.sep3.gif

Simu: 0758341483/0684175182
Email: deus.jovin@gmail.com

juu

Mimi naona kama utetezi ndo umeegemea kwa Marry mtashindwa vibaya, Hebu tupeni defination ya neno mkazi, kabla hamjaenda mbali. Ili mtu awe mkazi inambidi awe ameishi maeneo hayo kwa kipindi kipi? je neno mkazi lilotumiwa hapo linahusiano gani na mkazi kwa maana ya mimi mtanzania na mkazi foreigner utofauti wake upo vipi?
 
Anaweza akachomoka kwa sababu kuna kundi kubwa nyuma yake linalomuunga mkono likiongozwa na madame spika.
 
Kwa hawa majuha naowajua, hata kama CDM itakuwa na ushahidi mkubwa kiasi ani hawatakubali kushindwa, bt is gud maana watakuwa wanazidi kuuchochea moto huku mtaani
 
ukweli unabaki pale pale waziright mkuu hajalidanganya bunge na hawezi kudanganya kwani katika uchaguzi wa wilaya ya hai chedema imemtumia mbunge ambaye siyo mkazi wa halimashauri hiyo

Huu uoga na umbumbumbu wa watanzania unatugharimu sana.. Pinda ni binadamu na anaweza kulidanganya bunge kwa makusudi au bahati mbaya. Hamaki na vitisho anapoguswa kiongozi wa serikali ni kujenga nidhamu ya woga ambayo ni silaha kubwa ya madictator na viongozi wasiopenda kuambiwa ukweli. Huyu mama bunge lishamshinda...
 
Back
Top Bottom