Askari Kanzu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 4,598
- 1,233
Hapa juzi kati Hillary Clinton alitembelea Tanzania na kukutana na Rais Kikwete na Mh. Membe pamoja na viongozi wengine. Kabla ya hapo Clinton alikuwa Zambia ambako alizisihi nchi za kiafrika kujitahadhari na wachina wenye lengo la kuleta "ukoloni mpya". Baada ya Tanzania Clinton alielekea Ethiopia na kukutana na viongozi wa AU. Akiwa Ethiopia Clinton alizitaka nchi za Africa kumtema Gaddafi na kuutambua uongozi wa waasi wa Libya walioko Benghazi (TNC). Nchi nyingi za ulaya ambazo zinaipa "misaada" Tanzania ikiwemo Uingereza, Ujerumani na hata Denmark wametangaza kuitambua TNC. Inavyoonekana kwa sasa ni kwamba USA wameanza kuwahamasisha viongozi wa Africa kukubaliana na matakwa ya USA, na NATO kwa ujumla, kuhusu Libya.
Naona kuna kila ishara serikali ya Tanzania ambayo imeshaingia kwenye mtego wa "misaada ya wafadhili" kukubaliana na matakwa ya USA. It is just a question of time!
Naona kuna kila ishara serikali ya Tanzania ambayo imeshaingia kwenye mtego wa "misaada ya wafadhili" kukubaliana na matakwa ya USA. It is just a question of time!