He he he....tena anaapa kwa jina la mungu na la mizimu yote ya kwao...lolHehehe, mtenda akitendwa huhisi kaonewa! Kuna mwanaume anapigiwa simu anakuta missed call 10 afu anasema simu haikuita kabisa! Khabari yake banaa!
Hivi Balck Berry nazo zinapoteza network?
a cheater always a cheater hata umnunulie laini za dunia nzima akiamua ku cheat ata cheat tu.
Mkuki kwa nguruwe kwa binadam mchungu, mnavyowatendea wadada mnafikiri ni vizuri au wao hawaumii? mnawapanga kama wako kwenye foleni za Dar, ukipigiwa uko kwa huyu unajifanya nimfanyakazi mwenzio anakusumbua hupokei, ukienda kwake mwingine akapiga ni hivyo hivyo. Huyu dada alikuwa sahihi kwani hata yeye kwa Fred hayuko peke yake, kwanini yeye Fred awe peke yake
Hii ishu sio kwa wadada tu,Haya maneno nimeyasikia kwa masikio yangu mwenyewe toka kwa dada mmoja aliyekuwa akienda kwa buzi lake ili hali jamaa yake akiwa anamfuatilia kwa simu. Rafiki yake alipoona shostito wake hana mbinu za kumuepuka huyo mpenzi wake 'halali', akamshauri aizime simu yake ya TIGO ili awe free na huko alikokuwa akiupeleka 'mzigo' kwa njemba mwingine. Atakufanya ukose kuonana na John wakati ulimuahidi siku nyingi leo tungeenda kwake. Aaah! Huyu Fred naye yaani anavyokung'ang'ania, halafu ndoa yenyewe kila siku anakupiga kalenda. Nenda tu kwa John mwaya, pengine anaweza kuwa wa maana kuliko Fred. Na kweli rafiki yule akazima simu huku akikenua mdomo. Mie nikabaki hoi, huku nikiwa nimepata funzo, kwamba huu ubabaishaji wa mtandao wa simu wa TIGO kumbe unachangia pia watu 'kuibiwa mali' zao kiulainiiii. Jamani wanaume, sio kila unapomkosa mpenzio kwa mtandao wa TIGO ukadhani eti ni kwa sababu ya ubabaishaji wa huo mtandao. Inawezekana wakati mwingine mtandao uko ok, ila simu imezimwa makusudi kuepuka 'usumbufu' wako. Unaibiwaaaaaa kwa kisingizio cha TIGO, ebbo!