Shoprite closes more shops, but wont quit Tanzania market!

mimi hata sisikitiki hizi SM za makaburu zikifungwa ingekuwa Imalaseko au PATCO hapo ningesikitika
 
Tanzania ni zaid ya uijuavyo, but back on track...utamaduni wa kwenda supermarket hatuna hii nikutokana na fikra potofu kwamba SM ni ghali, pili tunaile tatizo la infiriority complex its like we think SM is for some people with certain status which is totally wrong. tunajibagua kutokana na aina ya maisha tuliyonayo.

kuhusu mlimancity, watu wengi wanadhani kule ni kwa mabishoo a.k.a wauza sura, lakini ukiingia SM mfano ya shoprite utakuta vitu ambavyo mtaani ni ghali kuliko pale, mfano maji ya kilimanjaro 1.5L mtaani ni 700tsh wakati pale ni 450. coca ya kopo mtaani ni 1000-1500 tsh lakini pale ni 750. so waTZ tunahitaji kupata elimu zaidi. faida nyingine SM bei hazina msimu, mfano msimu wa xmass au idd mtaani vitu huwa juu lakini pale always inabaki palepale. kingine kwenye SM huwa kuna sale ambapo bei hupungua kwa Percent flan kitu ambacho hakiwezi kutokea mtaani kamwe.

hizo ni hasara zilizotokana na kufungwa kwa SM, lakini faida mojawapo ni kupunguza lundo la bidhaa za southafrica ilifika stage hadi machungwa ni ya SA wkt pale Tanga yanaoza tu.

Matanzania wa kawaida haendi sokoni kununua maji.

Mtanzania wa kawaida anaenda sokoni kununua nyanya, vitunguu, mchele, etc.

Mtanzania wa kawaida si mjinga. Kama Supper Market mchele ni bei rahisi, watafurika hapo in no time. Kama nyanya zingekuwa bei rahisi SM, wangekwenda sana tu.

Labda hujui bei za bidhaa za watanzania wa kawaida, na unadhani nafuu kwako ndio nafuu kwa mtanzania wa kawaida.
 
Shoprite, wanatakiwa kuwa makini na hiring. Wabongo wengi uwezo wetu wa kufikiri ni leo tu kesho anajua mungu. Kuna siku nilienda Shoprite nikakusanya vitu vyangu kama vya Tshs 60,000. Nilipofika kaunta dada akanifuata na kuninong'oneza kuwa nimpatie mlinzi shs 20,000 halafu pale nilipie vitu vya Tshs 10,000 then niondoke, sasa nikawa sijamuelewa ana maanisha nini hasa mi nikakataa. Akasema wewe mbona mnoko?, Ila baadae nikaambiwa ndiyo mchezo wao. Sasa cha kujiuliza wewe unalipwa Tshs 200,000 kwa mwezi say, unaajira yako. unaiua kwa Shs Tshs 20,000 za leo kesho utaishije?.
 
RE SHOPRITE , NILIPOKUA ZAMBIA NA ZIMBABWE MIAKA TISA ILIOPITA NILIONA DU kweli sisi Watanzania kweli tuko nyuma wenzetu wana maduka ya kisasa kama western countries.
Nilirudi Tanzania na kuanzisha mini groceries huko Msasani ambayo mapaka leo hii ipo ingawa nilipata ushindani wa wadosi kuhakikisha naenda out of bussness , ila nilikua na wateja walionizoea na nilihakikisha , usafi ,a bei zangu ziko za ushindani wa hali ya juu.
Moja nililogundua ni kua watanzania bado hawako kwenye style ya kupenda style ya maduka makubwa. ( ni mentality ya kitanzania )
Pili nimeona mambo mawili , kwanza watanzania tunahitaji kumtukuza mkulima mtanzania kula product ya Tanzania , vipi tutanyanyua uchumi wetu , kumpa msafirishaji, rizki yake , mkulima soko la kuuza mazao yake ,a muuzaji wa duka aweze ku carry local prodcut , vipi watanzania tunafurahia product za nje wakati zetu zinaoza , mkulima wetu , anakufa njaa na familia yake , inakuaje tule chungwa la Afrika Kusini wakati lile la Tanga linaoza ?
Pia kuna mmoja humu netini kasema ikiwa wenzetu waliweza kumantain hizi uchumi super market huko Kenya kwa nini Watanzania washindwe ?
Ikiwa wewe uke Ulaya kwa nini usianze kununua ardhi na kuanza kupanda matunda na kuajiri wazalendo wa Tanzania na kuanza kuuza product zako kwa Watanzania au unangoja Wakenya akufanyie na wazungu halafu ulalamike wageni wanaiteka nchi yetu ?

Tulikua na good intention yautwala wa Awamu ya kwanza ya kujitegema kwa chakula vipi tunaruhusu mchele wa rahisi kutoka Vietnam, au Thailand unaingizwa kwa kodi ndogo wakati mchele wa Kutoka Mbeya unakosa soko ?
Na support serikali kutoa mikopo kwa wakulima wakubwa wa chakula ili taifa liweze kujitosheleza kwa chakula hii ni njia moja ya kujikomboa na kuongeza ajira katika sekta ya kilimo kilimo cha kisasa sio ile style ya kizamani ya Jembe.
 
Watanzania tumeathirika na kitu kinaitwa MASS CONSUMPTION, Watanzania tumekuwa watu wa kupapatikia sana vitu ambavyo ni artificial made na kuacha vitu ambavyo viko natural kwenye maeneo yetu. Watanzania tuko radhi kuacha mchicha na matembele yanayouzwa Bunju na Tegeta na kufunga safari ya kuja Mlimani City au Supermaket nyingine zozote kubwa.
Watanzania ukituuliza kwanini tunafanya hivyo tutakujibu uko kuna uchafuzi mkubwa wa mazingira kwahiyo mchicha wa uko una uchafu ya mikojo ya watu machupa yanaupwa uko ovyo, vinyesi vya watu na uchafu mwingine. Lakini hapa swali la kujiuliza nani anafanya huop uharibifu wa mazingira mpaka tunashindwa kula vyakula kutoka kwenye Ardhi yetu nzuri. Ni sisi wenyewe. Huu ni ujinga na ulimbukeni wa hali ya juu kwani tumekuwa dampo la bidhaa chafu na mbovu kutoka Ulaya na Amerika.
Watanzania elimu tunayopata bado haijatukomboa hata kidogo bado tuko kama matamauluku na matango pori kutokana na mkandamizo wa akili zetu katika kuwaza na kutatua matatizo yetu.
Sasa tunategemea Shoprite wafunge biashara zao wakati wamejijenga kwenye nchi ambayo ina makondoo na manyumbu wa kila aina wasioweza kujua kuwa wenzetu wa Ulaya na Amerika wanaendelea kutuletea starehe za kila aina ili watuteke akili zetu na kuendlea kufaidi ambacho wlikuwa wanakifaidi wakati wa ukolono lakini kwa sasa sisi ndio tunawaita ili watuue kabisa na kuchukua nchi yetu.
Ni ujinga wetu tu na tutaendelea kuwa wajinga hivi hivi kama hatutobadilika
Kwaherini
 
Back
Top Bottom