Shoka la TRA latua CHADEMA

Hawa TRA ile consultancy fee ya Idd Simba (Milion 285) kutoka Simon group wamechukua kodi? Vipi CCM,CUF, TLP wamewadai ngapi????????

Unategemea nini kama mtumishi wa TRA anakuwa Meya kupitia CCM na bado yuko kazini?
 
Hivi TRA haina namna ya kumkamata mkwepa kodi mpaka wafanye uchunguzi wa namna hii? Kama ndio, basi zoezi hili lifanyike kwa vyama vyote vya siasa na vile ambavyo si vya siasa, pia na wafanya biashara wote hasa wale wakubwa. Tena uchunguzi kwa vyama vingine vya siasa itumike independent company!

TRA ianzishe system ambayo itatoa information mara mlipa kodi anapokwepa kulipa kodi, la sivyo tunapoteza pesa nyingi sana.

Je, na wale wenye kuweka bei mbili kwa bidhaa moja - yaani say 2000 bila receipt ila ukitaka na receipt 2500 wanawashughulikia vipi?

Kuna wakati naona bora kutokulipa kodi kwa sababu mwisho wake ni kuongeza maisha bora kwa mafisadi na mendeleo ya nchi kwa ujumla hayaonekani. Kodi kwa maendeleo ya nchi na huduma bora, sasa iweje nilipe kodi kwa ajili ya maendeleo yasiyo ya nchi na huduma mbovu?
 
Katika hlo la kodi,hakuna kumumunya maneno,CHADEMA ilipe kodi na faini fasta and then iwamulike na vyama vingine kulipa kodi,the earlier the better.

Msipolipa mapema magamba wataifanya kuwa ni agenda kwenye majukwaa hali ya kuwa wao pia hawalipi..nina imani kuwa chadema ina uwezo wa kufanya maamuzi fasta hata kama ni magumu mf.kule arusha, kutolipa kodi si sahihi ingawa hatuoni faida ya kodi zetu, tunawakusanyia mafisadi.
 
Hapa nani alaumiwe? TRA au CHADEMA? Kwani TRA imekuepo kuanzia lini na majukumu yake siku zote ilisahau au ilikuwa wapi tangu 1992 - 2011? Waache unafiki!

Wote walaumiwe. Chadema kwa kutokulipa kodi kama inavyotakiwa kisheria na TRA kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa miaka 19 ambayo Chadema walikuwa hawalipi kodi.
 
chama kinachotaka kwenda ikulu hakilipi kodi? halafu wanataka wapewe dhamana waongoze taifa hili! wapuuzi!!!
 
Monday, 08 August 2011
NA HAMIS SHIMYE
, Gazeti la Uhuru

Ukitaka habari yako isomwe na kama source ni gazeti la uhuru. SOERCE usiiweke mwanzoni maana watu wengi waliacha kusoma habari zinazotokea gazeti la Uhuru.
 
hizo ni habari za gazeti la uhuru.ndo maana hajataja chanzo.

Gazeti la Uhuru halina Waandishi wa Habari? kama ni la CCM I really don't care what I care about is Chadema to be charged by TRA; but there are damn so many loopholes to CCM Business Men, CCM affiliate Industries and People who get's unwanted TAX exceptions...
 
Jamaa yangu aliye makao makuu ya CCM Lumumba ananitayarishia document ya kuonyesha kuwa CCM nayo hailipi kodi katika mambo yao mengi sana -- mishahara ya baadhi ya watendaji wake, kodi za majengo, viwanja mbali mbali chama hicho inavyovimiliki etc. Hii itamwagwa kwenye gazeti moja la kila wiki hivi karibuni.

Wananchi msihofu kabisa kuhusu hili, ni ukweli kabisa na itaonyesha kuwa kama vile TAKUKURU, Polisi, etc, TRA nayo inatumiwa na CCM.
Usiwe na shaka tunalijua hilo kuwa TRA ni kibaraka wa CCM. Ila tu tunaomba utuwekee hizo taarifa hapa jamvini.
 
mheshimiwa mtoa hoja, unajua mshahara wa mbunge????kwanza source ya habari ni uhuru of all news papers?du umeishiwa! let them do what they want ili wadhoofishe mkombozi wa watanzania!

Tushasema, chadema ikibidi tutawachangia sisi wananchi ili kukamilisha ndoto za watanzania ambao wameteseka ndani ya nchi yao nzuri cha ajabu hata somalia wana nafuu ambao wanategemea mchanga wa kutengeneza vioo!
 
Chadema wafanye maamuzi magumu na ya msingi kama kule Arusha walipe hiyo faini na waendelee kulipa Kodi na issue hii haiwezi kutuondolea imani tuliyonayo kwa Chadema maana hata sisi wenyewe huwa tuna mapungufu ila inapotokea ukaambiwa mapungufu yako unajirekebisha na mambo yanaendelea. ingawa wengi wetu hatuoni faida ya kodi tunayolipa.

Mimi nafikiri TRA wameshamalizana na Chadema sasa tunaomba taarifa za kodi za vyama vyote ukianzia na ccm, hiyo ndiyo itatuonyesha kweli TRA wapo kwa maslahi ya wananchi 40 milllion na sio kwa manufaa ya ccm. na wakifanya hivyo kwa haki kweli nitawaheshimu.
 
njia ya mwongo ni fupi kwa hiyo wala msishangae miaka yote hiyo TRA ilikuwa wapi kama ni kweli inamaana hata nyie mnatakiwa kushotakiwa maana hamjui majukumu yenu
 
njia ya mwongo ni fupi kwa hiyo wala msishangae miaka yote hiyo TRA ilikuwa wapi kama ni kweli inamaana hata nyie mnatakiwa kushotakiwa maana hamjui majukumu yenu
<br />
<br />
Mwenye akili timam anajua lengo la hawa watu,usijali!
 
CCM wameanzisha vita ya kutupiana mawe hali ya kuwa wanaishi kwenye nyumba za vioo.lets see the end of it.
 
Kama vipi chadema anzisheni harambee wapenda mageuzi wachangie mkalipe kodi.ths shouldnt be an issue,lipeni then mu demand transparency kwa vyama vingne namna wanavyolipa kodi
 
Back
Top Bottom