Shocking News; Kweli ndio tumefika huku?

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
Kuna jamaa anafanya kazi kama lab technician. Kaniambia kuwa watu wanaokuja kupima damu % kubwa wana ngoma. Nikamwambia toa mfano.

Akaniambia leo kapima wadada wajawazito sita. Na wanne kati yao wana virus vya UKIMWI na umri wao ni kuanzia miaka 18-23.. So guys watch out. Na hao wadada wote wameolewa.

So jiulizeni mko wangapi? It really shocked me. Jamani tuache haya mambo tutaisha hasa kwenye ndoa huko mmmh!!! Haya
 
Mkuu Black Bat, think you mean Lab Technician,

Duh?! Sidhani kama ni sahihi sana yeye(ndugu yako/Lab Technician) kukueleza matatizo ya clients wake, inapunguza usiri(confidentiality),

Pili inawezekana isiwe sahihi sana(False positive results) hutokea, na hovyo kuhitajika kupima tena.

Mkuu mbona wasema, "JIULIZENI mko wangapi?" Hii kitu yetu sote!!

ILA ukweli utabaki pale pale mkuu, tujihadhari(ambao hatujapata) ili tusiambukizwe, na wenye VVU kuzingatia ushauri na tiba.
 
Mkulu kisha sema viherehere vinawaponza...... Hawatendi maisha yao wanatamani vya wenzao
 
Mkuu Black Bat, think you mean Lab Technician,

Duh?! Sidhani kama ni sahihi sana yeye(ndugu yako/Lab Technician) kukueleza matatizo ya clients wake, inapunguza usiri(confidentiality),

Pili inawezekana isiwe sahihi sana(False positive results) hutokea, na hovyo kuhitajika kupima tena.

Mkuu mbona wasema, "JIULIZENI mko wangapi?" Hii kitu yetu sote!!

ILA ukweli utabaki pale pale mkuu, tujihadhari(ambao hatujapata) ili tusiambukizwe, na wenye VVU kuzingatia ushauri na tiba.

Anamjua Black Bat ni kiwembe kwa vibinti, ili kumbadilisha ndio maana kampa hiyo taarifa. Lab Tech naamini hakutaja majina ya wagonjwa hadharani hence hana kosa
 
Anamjua Black Bat ni kiwembe kwa vibinti, ili kumbadilisha ndio maana kampa hiyo taarifa. Lab Tech naamini hakutaja majina ya wagonjwa hadharani hence hana kosa

Definetly hakutaja majina na najua hawezi kuyataja kwani ana kiapo. Mimi sio kiwembe
 
Kwa hiyo hapo kavunja miiko ya usiri? Hii situation ni exceptional la sivyo tutaangamia wote tukificha mambo kama haya

Walioweka confidentiality si wajinga.

Kitendo chako wewe kuja JF kusema mnaongea na nduguyo Lab Techcician kuhusu afya za watu tayari kinaondoa confidence miongoni mwa watu kwamba habari zao zinawekwa kwa faragha inayotakiwa.

Wengine watasema umesema tu kwamba hajataja majina kwa sababu kusema kataja majina ni soo, ila majina kataja, na wao wataogopa kwenda kupima.

Kukataa kwao kwenda kupima kutaongeza maambukizi.

Unaposema "tutaangamia wote" kwa simplistic approach ya kufikiri kuvunja faragha ndiyo jibu, unaweza kujikuta unapalilia kuangamia wote kwa sababu ya kuondoa imani ya watu juu ya uwezo wa system ku keep mambo ya afya zao confidential.
 
Nimekujaje fastaaa! Mada kama hizi nazikwepaga kwepaga! Mambo haya ukifikiria sana utakuwa HUTOKI NJE YA NYUMBA!!! Na hivi huwezi kumjua kwa KUMTIZAMA!!!!!! Eee Mola Utusaidie!
 
Walioweka confidentiality si wajinga.

Kitendo chako wewe kuja JF kusema mnaongea na nduguyo Lab Techcician kuhusu afya za watu tayari kinaondoa confidence miongoni mwa watu kwamba habari zao zinawekwa kwa faragha inayotakiwa.

Wengine watasema umesema tu kwamba hajataja majina kwa sababu kusema kataja majina ni soo, ila majina kataja, na wao wataogopa kwenda kupima.

Kukataa kwao kwenda kupima kutaongeza maambukizi.

Unaposema "tutaangamia wote" kwa simplistic approach ya kufikiri kuvunja faragha ndiyo jibu, unaweza kujikuta unapalilia kuangamia wote kwa sababu ya kuondoa imani ya watu juu ya uwezo wa system ku keep mambo ya afya zao confidential.
Kiranga kwahiyo hata taarifa tunazopewa za maambukizi mapaya au Tanzania ina wagonjwa kadhaa wa ukimwi nayo ni makosa?
 
Last edited by a moderator:
ndugu yako anajua maadili ya kazi yake?

Confidentiallity iko wapi?

Anyway na yeye mwenyewe kajipima au anajua kubwabwaja ya wenzie tu?

Maadili ya kazi hakuna kabisa siku hizi
 
hili la kuathirika ni kubwa kuliko tunavolitazama juu juu!la msingi ni kutambua wajibu wetu na kuutimiza,iwe ni kwa wenye ndoa au wasio na ndoa!it i:shock:s very scary!
watu tunaongelea ukimwi kama vile swala la mbaali yani kama vile halituhusu flani hiv,sipmly becoz tunaamini kwa wakati huo linapozungumziwa hatuna!lakini kiuhalisia dah!
 
Nilitaka kuuliza hivyo hivyo...sioni umuhimu wa usiri kwenye hili as long as hajataja jina.
Ndio tabu ya mifumo yetu yaani hata barua ya Ofisa Mtendaji wa kata inagongwa Muhuri wa siri. mimi naona huyo ndugiu yake yuko sahihi kwa kumpa hali halisi na age ambazo ndio more risk.

Siri ni yale majina yao tu na si vinginevyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom