Shocking! Kupunguza foleni, Amina Amour (mbunge) ashauri serikali iongeze ushuru!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Amini Usiamini, Leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu mbunge wa kuteuliwa nafikiri wa mji mkongwe bi AMINA AMOUR ameuliza swali bungeni kwamba Dar Es Salaam imekua na magari mengi na kwa hiyo msongamano umekua mkubwa, kwa nini serikali haioni ni busara na wakati muafaka sasa kuongeza ushuru ili kupunguza idadi ya mgari yanayoingia nchini.

Kwa taarifa,
For all vehicles with that are not more than 10 yrs old
Import duty 25%
Excise duty 10%
VAT 18%
Cumulatively this is 63% of CIF value! (Amina anataka zaidi ya hapa!)

Kama imezidi miaka kumi unapiga nafikiri 20 au 25% uchakavu yaani inakua kama 87% ya CIF

Jamani hii ndo aina ya wawakilishi tulionao mjengoni, solution ya foleni barabarani ni kuzuia watu kununua magari kwa kuongeza ushuru. Kwa hali ilivo sasa ushuru wa magari ni mkubwa sana lakini Amina anaona hautoshi.

Nimeshangaa sana! Sikutegemea kama mbunge anaweza kuwa na mawazo hovyo kiasi hiki, hawazi kabisa kuhusu kuboresha miundo mbinu...AJABU AND SHOKING!

source: TBC1
 
hajui kama posho yake inatokana na hizo kodi za magari. seriakali inapata kodi ya kutosha from CIF. najua serikali haiwezi kudhubutu. wao awatafute njia ya kitaaluma zaidi kuondoa tatizo la foleni Dar.
 
Usishangae hali hiyo mkuu! Hayo ni matokeo ya kupata wabunge kwa njia ya kiufahamiana
 
vituko kabisa ndio wanaotokana na chama cha gamba siye yetu macho na maskio kesho atasema watu wasinunue magari ili yaliyoopo yachakae na uwe mpango mzima wa kupunguza foleni dar.
 
Amefikiri hadi kichwa kikamuuma,akagundua Foleni ya Dar inasababishwa na kiwango kidogo cha Kodi kwenye Magari,Anahitaji pongezi na si lawama.Bila kauli kma hiyo kutolewa bungeni ingekuwa vigumu sana kwenu kutambua uwezo wa waheshimiwa kufikiri na kutafuta namna ya kutatua matatizo ya taifa
 
Ndugu Uswe alichosema huyo mama hajakosea kabisa , ni moja tu ya namna ya kupunguza foleni. Alichokosea ni kuwa bado public transport ni mbaya hivyo hata ukipandisha kodi huyu mtu anakuwa hana alternative zaidi ua kuendelea kuumia kutumia gari lake. Nchi zingine kwa mfano Brazil walifanya sana hiyo style lakini wakijua RBT zinasaidia na kuwa substitute. Tanzania huwezi ukaingia kwenye daladala na laptop yako ukajiona salama!
 
hahahaaaaaaaa i love this! kwamba kafikiriiiiiiiiiiiii hapo ndo kapata Jibu! duh!
 
Ndugu Uswe alichosema huyo mama hajakosea kabisa , ni moja tu ya namna ya kupunguza foleni. Alichokosea ni kuwa bado public transport ni mbaya hivyo hata ukipandisha kodi huyu mtu anakuwa hana alternative zaidi ua kuendelea kuumia kutumia gari lake. Nchi zingine kwa mfano Brazil walifanya sana hiyo style lakini wakijua RBT zinasaidia na kuwa substitute. Tanzania huwezi ukaingia kwenye daladala na laptop yako ukajiona salama!

Hapana Wabe, lete statistics please, Ushuru ulikuwaje Brazil na Idadi ya Magari ilikuwaje?

Unajua Idadi ya Magari yaliyopo Dar? hayafiki hata robo ya magari yaliyopo Nairobi. Pia Ushuru kwetu tayari ni mkubwa sana nimweka viwango hapo juu, Mwisho tatizo kubwa na Dar ni infrastructure na si wingi wa magari, magari ni kidogo sana ukilinganisha na idadi ya watu, wengi sana bado wanapanda daladala
 
  • Thanks
Reactions: WFM

Mkuu unazungumzia kupunguza foleni na ushuru wa magari?
au unazungumzia uwiano wa wingi wa magari na idadi ya watu?
 
Ulitegemea nini toka kwa mbunge zao la sekondari za kata aka shule za Lowasa aka Yeboyebo?
 
Kwa taarifa,
For all vehicles with that are not more than 10 yrs old
Import duty 25%
Excise duty 10%
VAT 18%
Cumulatively this is 63% of CIF value! (Amina anataka zaidi ya hapa!)

source: TBC1
[/COLOR] [/COLOR]
hayo liyoandika nina uhakika hawezi kuyajua yanahusu nini, na si yeye pekee bali na wenzie humo ndani, maana hata mkulu anaamini msongamano ni sign ya matajiri kuongezeka sasa unategemea nini???? Kumbuka na wale tuliodhani wana upeo na ufahamu wa kutosha wamepitisha budget ya 1b (sijui wamezipaje) kujenga barabara ya Loliondo na umewaona walivyochangamkia kikombe kwa staili yao. Hapo ndipo nchi ilopofikia!
 
Mkuu unazungumzia kupunguza foleni na ushuru wa magari?
au unazungumzia uwiano wa wingi wa magari na idadi ya watu?

Nachosema wabe, si kweli kwamba magari ni mengi dar es salaam na hakuna sababu ya kuongeza kodi eti kupunguza uingizaji.

Tunaposema magari ni mengi (kama alivyodai Amina Mbunge) kipimo ni nini? mi nilifikiri kuna ratio flani, kwamba tunalinganisha idadi ya watu na idadi ya magari, kama mji una wakati milioni nne mari yaliyosajiliwa yako laki mbili na kitu hatuwezi kusema magari ni mengi.

wabe unachotaka wewe ni kipi, kwamba tutumie tu kiswahili, wingi unaanzia mbili na kuendelea kwa hiyo tukiwa na magari mawili au matatu au manne barabarani basi tuna magari mengi au?
 
Yeah mtu kama huyo maimuna mnategemea aseme nini. Ubunge wenyewe kaupatia mezani utegemee aseme nini? Tuna vilaza kwelikweli bongo yetu!
 
Amini Usiamini, Leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu mbunge wa kuteuliwa nafikiri wa mji mkongwe bi AMINA AMOUR ameuliza swali bungeni kwamba Dar Es Salaam imekua na magari mengi na kwa hiyo msongamano umekua mkubwa, kwa nini serikali haioni ni busara na wakati muafaka sasa kuongeza ushuru ili kupunguza idadi ya mgari yanayoingia nchini.

Kwa taarifa,
For all vehicles with that are not more than 10 yrs old
Import duty 25%
Excise duty 10%
VAT 18%

Cumulatively this is 63% of CIF value! (Amina anataka zaidi ya hapa!)

Kama imezidi miaka kumi unapiga nafikiri 20 au 25% uchakavu yaani inakua kama 87% ya CIF

Jamani hii ndo aina ya wawakilishi tulionao mjengoni, solution ya foleni barabarani ni kuzuia watu kununua magari kwa kuongeza ushuru. Kwa hali ilivo sasa ushuru wa magari ni mkubwa sana lakini Amina anaona hautoshi.

Nimeshangaa sana! Sikutegemea kama mbunge anaweza kuwa na mawazo hovyo kiasi hiki, hawazi kabisa kuhusu kuboresha miundo mbinu...AJABU AND SHOKING!

source: TBC1

hesabu kweli ni homa ya taifa, loh! unashindwa hata kujumlisha? kazi kwelikweli alafu mkiongea mnaongea kwa jazba vitu vyenyewe hamvijui... pole sana
 
Nimesikitika sana kwa mawazo ya huyu Mwakilishi. Kwanza tanzania imejitoa kabisa kwenye swala la public transport barabarabi. Ilitakiwa hizo kodi zinazolipwa ziboreshe miundombinu na huduma hiyo ambayo haifanyi hivyo serikali. Pili tatizo siyo magari kuwa mengi, miji yetu haipo kwenye mpango mzuri na vilevile networking ya barabara zeti ni ndogo sana na sehemu nyingine hakuna. Unakuta barabara moja ndiyo pekee kwenda katikati ya mji. Ukiangalia Saporo (Japani) ini mji mdogo kuliko Dar na una magari zaidi ya milioni tatu, ila bado hakuna msongamano. Nahisi mainjinia wetu wanalijua hili, na wengine wamesoma ng'ambo na kujionea. Ila kutokana na kutegemea wanasiasa wetu kutuamulia mambo bila kutumia jopo la wataalamu ili kuweka sawa mipango mbalimbali kwa pamoja, utamaduni huo hatuna. Mfano mzuri ni malumbano ya Serikali na taasisi nyingine juu ya uwamuzi wa kuruhusu kutengenezwa kwa barabara kubwa (High way) inayokatiza Mbuga ya Serengeti.
 
Back
Top Bottom