Shivji apinga Afrika Mashariki kuikodolea macho Marekani

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
PROFESA Issa Shivji amepinga msimamo wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kutaka nchi za Afrika Mashariki kuweka malengo ya kupata chochote kutoka Marekani kutokana na kuongozwa na Rais Barack Obama .

Amesema itakuwa fedheha kama nchi za Afrika Mashariuki zitabweteka na kusubiri fadhila kutoka Marekani na kwamba kwa vyovyote vile hakuna kitakachotolewa Marekani bure.

Juzi, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala akizungumza kwenye kongamano la jinsi ya kunufaika na utawala wa Rais Obama alisema Afrika Mashariki ni lazima inufaike na uongozi wa rais huyokwa kuwa ni mwwenye asili ya Afrika Mashariki.

Kamala alisema Afrika Mashariki ingalie ni vitu gani ambavyo vitaiwezesha Marekani kuisaidia ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu kudumisha amani na demokrasia ya kweli.

Lakini Shivji alisisitiza kwamba ni bora Afrika Mashariki ikajitegemea ili kuepuka kutawaliwa kiuchumi na Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Shivji alisema Afrika Mashariki isitegemee kunufaika na uongozi wa Barack Obama kutokana na ukweli kwamba hakuna sera iliyobadilika nchini Marekani na kwamba Obama anaendeleza Sera za Bush.

"Suala hili tutapoteza uhuru wetu, kwanini tutegemee Marekani kutuamlia mambo yetu, Marekani ni nani ?, sanasana Marekani watatusaidi silaha za kijeshi, je tunataka kujenga bara letu kijeshi? "alihoji Shivji ambaye ni Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

"Mbona kipindi cha chama cha TANU hakikuwa chini ya taifa lolote na tuliendelea mpaka tukapata CCM sasa hapo

"Kwa kifupi mimi nataka Marekani iwe mbali na Afrika Mashariki, Afrika isitegemee mjomba , ikitaka kupata maendeleo ipigane yenyewe kama ni kudumisha amani tudumishe kwa manufaa yetu wenyewe sio Marekani ije"alisema.

Hata hivyo, alisema wasomi wa Afrika Mashariki wanapaswa kulaumiwa na kujilaumu wenyewe kwa kutowaelimisha watu juu ya ubaya wa kutegemea wafadhili kwa kuwa bara letu kihistoria ndefu.

Source:http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17852
 
Juzi, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala akizungumza kwenye kongamano la jinsi ya kunufaika na utawala wa Rais Obama alisema Afrika Mashariki ni lazima inufaike na uongozi wa rais huyokwa kuwa ni mwwenye asili ya Afrika Mashariki.

Oh Africans..Africans...Africans...Yaani kweli wanaandaa 'kongamano" la jinsi ya kunufaika na utawala wa raisi Obama? Na huyo "Dk" Kamala kweli alisema lazima Afrika Mashariki inufaike na uongozi wa Obama kwa vile babake alitokea Kenya? Ingekuwa vyema tukapata nukuu kamili ya alichosema "Dk" Kamala.

But even the whole idea of having a symposium on how to benefit from the Obama administration is.....(you fill in the blank). I'm fighting myself not to go in on these negro muthafuckas. I guess my signature says it all.
 
Well said kamanda....Miafrika ndivyo tulivyo we can't think for ourselves!
 
Huyu 'dr' Kamala ni design ya akina Nchimbi,Nagu,Makongoro etc.
Shame anatuwakilisha EAC ,yeye na so called ,'dr' Nangale.

Naona Wakenya na Waganda wanatuona sisi ni fake of fakers
 
OMG yaani badala ya ubunifu wa jinsi ya kujiboresha tunawania misaada, duh kwa mwendo huu tutafika kweli???!!!
 
Ila binafsi sishangai kwa huyu waziri kusema haya yanayosemwa alisema. Kwa sababu si Waafrika wa Afrika Mashariki tu wafikiria hivi bali hata kipindi kile Obama alipoenda Ghana, raisi wao mstaafu John Kufour alihojiwa na essentially akasema kama hayo yanayodaiwa kusemwa na Kamala. Hata Marekani wanugu wengi walikuwa wanadhani na kuna baadhi ambao bado wanadhani kuwa Obama atafanya mambo kuwasaidia wao kwa sababu ni nusu mzungu nusu mweusi.
 
HAkuna haja ya kumsema Dr. Kamala maana ni yeye anajumuisha tu dhana ya Miafrika NdivyoTulivyo ... Julius JF Senior Expert Member
 
Oh Africans..Africans...Africans...Yaani kweli wanaandaa 'kongamano" la jinsi ya kunufaika na utawala wa raisi Obama? Na huyo "Dk" Kamala kweli alisema lazima Afrika Mashariki inufaike na uongozi wa Obama kwa vile babake alitokea Kenya? Ingekuwa vyema tukapata nukuu kamili ya alichosema "Dk" Kamala.

But even the whole idea of having a symposium on how to benefit from the Obama administration is.....(you fill in the blank). I'm fighting myself not to go in on these negro muthafuckas. I guess my signature says it all.

You have said well Julius but please people hebu nisaidieni kuitafsiri hii heading
"African Development Policy Goals and Strategies: Implications of the Obama Presidency"
Kwa sababu hii ndiyo ilikuwa heading ya kingamano hili ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Kenya. Sidhani kama lengo au tafsiri ni jinsi ya kunufaika na utawala wa Obama bali ni kuangalia implication ya utawala wa Obama katika malengo na mipango ya maendeleo ya Africa. Kwa uelewa wangu mdogo nilielewa kuwa utawala wowote wa nchi ambazo zimekuwa zikitupatia misaada mbalimbali una affect maendeleo ya Africa iwe ni Bush au Obama kufuatana na zile priority areas zao.

Kwenye kongamano hili Dr. Kamala nakumbuka alitaja maeneo kama nane ambayo utawala wa Obama umejaribu kuyapa kipaumbele na maeneo hayo yote yana theme kuu za African peace and Security. Dr. Kamala alijaribu kuelezea namna ambavyo tunawezatoa ushirikiano katika kutekeleza malengo haya ikiwa ni pamoja na kupanga mipango yetu katika kuaddress hizi areas ili kuunganisha nguvu na Obama.
Si nia yangu kuwapinga mitazamo yenu but nilitaka kutoa ufafanuzi wa yaliyojiri pale kwenye kongamano na pia kuwezakupata uelewa zaidi juu ya hii hoja.
 
Back
Top Bottom