Shitambala ajiuzulu uongozi wa CHADEMA Mbeya!

njaa ni adui wa haki, mtu yupo radhi kuwatosa wenzake kwa vipande vya sarafu. watu kama hawa wapo wengi tu na sasa ndiyo muda wa viongozi wasio waadilifu kutimka CHADEMA kwenda CCM kunganga njaa.

Msiogope kwani yeye ni nani? waliondoka kina xxxxxx na CHADEMA ikapeta. kumbukeni chadema ni wito na si mshiko, wanaotaka mishiko nafikiri waondoke mapema sisi tupo kuwatumia wananchi hasa maskini na si vinginevyo.

Tatizo la CCM wanafikiri wanaweza kuua demokrasia kwa kutumia PESA, never ever. Hiyo ni njia ya kupoza maumivu tu ni sawa na mtu unaumwa malaria then unatumia pain killler pills.
 
Sielewi kwanini chama kinaweza kujaribu kununua ubunge kwa kiasi hicho. Ni vigumu kuamini.. lakini vile vile sijaona kwanini hadi sasa haijawezekana kuwatega hawa watu wanaopita na kutoa ofa za namna hiyo.

a. Hakuna aliyetegwa akinunua shahada
b. Hakuna aliyetegwa akiuza kura
c. Hakuna aliyetegwa akinunua Ubunge

Vyote vinasadikiwa vinatokea.

MM
Unafikiri mtego unawezekana wakati wakutega na kutegua wanasimamiwa na Hosea (TAKUKURU) wa kusafisha mafisadi??????
 
Roho inaniuma roho, hii kazi ya mafisadi roho
CHADEMA kuhujumu roho, Roho inauma roho
Walianza ndogondogo roho, Chadema kuiuma roho
Mafisadi wamepanga roho, CHADEMA kuiua Roho

Enzi zile elfu mbili na tano roho, Mafisadi hawakuhofu roho
Chadema Bado changa roho, Tupambane nayo CUF roho
Mkakati waliweka roho, hiyo CUF kuimeza roho
Mafisadi wamepanga roho, Chadema kuiua roho

Wakaona hiyo Cuf roho kibindoni imetinga roho
Mkakati wakaweka roho Chadema kunanani roho
Japo changa Inatisha roho, Hiyo Chadema kwao mwiba roho
Mafisadi wamepanga roho Chadema kuia roho

Kwa mifano walifanya roho,vikaoni tukaona roho
Zito kabwe fukuzisha roho,ukumbini kama mwizi roho
Wakaona haitoshi roho mijadala wakazima roho
Mafisadi wamepanga roho, Chadema kuiua roho

Walianza naye Wangwe roho, mgogoro pandikiza roho
Mara kifo kimezuka roho, Wao Chadema Singizia roho!
Eti kifo chake kilipangwa roho, Chadema wahusika roho!
Mafisadi wamepanga roho, CHADEMA kuiua Roho

Mtego huo ukashidwa roho, watu wengi stukia hiyo roho
Wakaona wabadilishe gia roho,mtegoni waingize roho
Wakaaza naye Kabwe roho,Kwenye tume muingiza roho
Mafisadi wamepanga roho, CHADEMA kuiua Roho

Kwenye tuma kaingia roho,Zoto kabwe wameweza roho
Mijadala ikazuka roho,Zitto kabwe sio yule roho
Yao manenon akubali roho, Ya mageuzi ayapinga roho
Mafisadi wamepanga roho,Chadema kuiua roho

Pundepunde tukaona roho, mabadiliko taratibu roho
Zitto kabwe sio yule roho, Kauli zake za utata roho
Hazifanani nao mwazo roho, Mafisadi kufanana roho
Mafisadi wamepanga roho, Chadema kuiua roho

Dowans,EPA alipinga roho hapo, mwazo Zitto kabwe roho
Kwenye tuma ametoka roho, Zitto kabwe sio yule roho,
Mafisadi hoja zao roho, Zitto kabwe akubali roho
Mafisadi wamepanga roho, Chadema kuiua roho

Mara uenyekiti mara urais roho, Huyo ndio Zitto kabwe roho
Na mzozo ukazuka roho,Chadema tikisika roho
Zitto kabwe Freeman roho, kunanini kati yao roho
Mafisadi wamepanga roho,Chadema kuiua roho

Yamesikika maneno roho, Mafisadi walihonga roho
Zitto kabwe ahusishwa roho, Siamini macho yangu roho
Kachukua mlungula roho, Zitto kabwe naambwiwa roho
Mafisadi wamepanga roho, Chadema kuiua roho

Wenye viti makatibu roho,Chadema matatizo roho
Nje ndani ndani nje roho, Makatibu nao pia roho
Wenyeviti usiseme roho, Chadema kunanini roho
Mafisadi wamepanga roho Chadema kuiua roho

Kwamfano wa Shitambala roho, Wasiwasi wanishika roho
Kuna nini mtu huyu roho,maneno mengi yamezuka roho
Huko Mbeya kubalika roho, Mbona sasa ipo hivyi roho
Mafisadi wamepanga roho, Chadema kuiua roho

Kuna nini Tanzania roho, nchi yatu inayumba roho
Mafisadi wanania roho, Tanzania kuiuza roho
Wanachi ni vipofu roho, wananchi bado tambua roho
Mafisadi wamepanga roho, Chadema kuiua roho

Roho imetumika ikimaanisha nini kwenye utenzi wako?? Sipati flow inayoeleweka kwa kutoelewa matumizi ya neno Roho!!
 
Milioni 600 hata ningekuwa mimi nisingekataa kuzipokea (utani). Ni vigumu kuamini kiwango kikubwa kama hicho kinaweza kutolewa lakini bila kufanya utafiti wa kutosha katika siasa tunajizuia kukanusha . Naomba nijizuie kukanusha.




Aliyekuwa Mweneykiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya mwanasheria SAMBWEE SHITAMBALA amejiuzulu nafasi hiyo!

Anakabiliwa na shutuma za kupokea 600million toka kwa CCM na akuuuza ubunge kwa mchungaji wa CCM.
Shitambala Amedai kila akitaka kujieleza juu ya tuhuma hapati ushirikiano kutoka kwa mwenyekiti taifa bwana Mbowe.

Hili sasa ni pigo kwa CHADEMA - MBEYA
 
Chitambala ni mtu maarufu sana Chadema hawakutegemea ataanguka na ndicho kilichompoza huyu bwana lakini kwenye siasa lolote laweza kutokea kama ilivyotokea kwa Lawrence Masha waziri wa mambo ya ndani wa zamani.
 
Nikumtoa huyo ili chadema isiingie katika mkumbo wa kifisadi kama ccm, samaki mmoja akioza unamtupa asiozeshe wengine katika fungu
 
Viongozi wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wametoa kauli zinazokinzana juu ya tangazo la Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, la kujivua rasmi uongozi kutokana na kashfa anazotupiwa za kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi.

Akizungumza leo asubuhi kwa njia ya simu, Katibu wa CHADEMA mkoani Mbeya, Eddo Makata, amesema kauli aliyoitoa Shitambala ilikuwa ni ya jazba kwani ni mapema mno kuanza mifarakano wakati wananchi wanawategemea kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.

“Jamii hivi sasa imeegesha nyoyo zake ndani ya CHADEMA na inahitaji nguvu zake za kuleta mabadiliko na siyo ,” amesema Makata.

Ameongeza kuwa hadi sasa hawajapokea barua maalumu ya kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo na endapo watapokea chama kitakaa kikao na kutoa tamko rasmi.

Hata hivyo, Shitambala ametoa hoja tofauti wakati akizungumza na gazeti hili, akidai kuwa yeye ni mwanasheria hivyo CHADEMA Taifa wanapaswa kuzungumzia tuhuma hizo kama zina ukweli ili kulinda heshima yake.

Amesema kutokana na shughuli zake za kikazi anaogopa kuwa kauli hizo zinaweza kumwangusha kikazi na kumtenga na ndugu pamoja na rafiki zake.

Ameongeza kuwa ameshangazwa na kitendo hicho kwa kuwa amefanya kazi kubwa ya kukitangaza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu na wamefanikiwa kuibuka na ushindi kutokana na kupiga kampeni katika jimbo la Tunduma na Mbeya Mjini.

“Wanachama ni wepesi sana kujenga hoja zisizo za msingi na kuzisambaza, hivyo wamenituhumu kuwa nimechukua fedha ili kulihujumu jimbo lichukuliwe na CCM, jambo ambalo si la kweli na naomba tume huru iundwe na ilitolee tamko suala hilo,” amesema.

Hata hivyo, amesema amekuwa akilalamikiwa na wanachama wa mkoa huo kuhusu kuwapigia debe ili wapate viti maalumu angalau kimoja, ingawa katika mikoa ya Kigoma, Dar es Salaam na Kilimanjaro vilinyakuliwa viti kibao.

credit : Christina Gauluhanga na Stella Aron/DarLeo


http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz160LHKpli
 
kama kila ulichotuambia ni kweli,basi inasikitisha sana ila wanaharakati tusirudi nyuma,mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.
 
Aliyekuwa Mweneykiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya mwanasheria SAMBWEE SHITAMBALA amejiuzulu nafasi hiyo!

Anakabiliwa na shutuma za kupokea 600million toka kwa CCM na akuuuza ubunge kwa mchungaji wa CCM.
Shitambala Amedai kila akitaka kujieleza juu ya tuhuma hapati ushirikiano kutoka kwa mwenyekiti taifa bwana Mbowe.

Hili sasa ni pigo kwa CHADEMA - MBEYA

Pigo gani, wakati msaliti na mtu mwenye njaa kama mchwa ameondoka mwenyewe kwenye chama safi. Kumbuka huyu mtu alishapewa mara mbili kugombania kiti hicho.
 
Kweli nimeamini CHADEMA ni Chama Cha Demokrasia, yaani ukiwa na tuhuma za kuhujumu Chama au Taifa viongozi wake wanajiuzulu ili kupisha mchakato wa uchunguzi.

Laiti kama viongozi wa CCM wangekuwa kama Ndugu Shitambala, wanasiasa wangejiongezea heshima.

 
Pigo gani, wakati msaliti na mtu mwenye njaa kama mchwa ameondoka mwenyewe kwenye chama safi. Kumbuka huyu mtu alishapewa mara mbili kugombania kiti hicho.

Ina maana ukiwa mgombea wa chadema ni marufuku kushindwa, lazima kura zitoshe? Hatari sana kwa demokrasia.
 
CDM wanafaidi sana hela za CCM maana hata mbowe amepokea mpaka Tshs 200 million toka kwa Sabodo wa CCM kwa ajili ya kujenga CDM. na hata baadhi ya wabunge waliochaguliwa inasemekana walikula hela kidogo kama yule wa nyamagana.
uvumilivu unatakiwa hapa ili kupata ushahidi wa kutosha kabla ya kumlaani mtu. pesa ni tamu sana na everybody can be tempted ila bila ushahidi si busara kumsakama mtu
 
Hivi tunaota au ndiyo kila linalosemwa liaminiwe tu bila ya kulidadisi.Mtu atoe milioni mia sita kwa ubunge halafu ndiyo iweje?Hata madili yote ya miaka 5 yatalipa kweli labda apewe wizara ya miundo mbinu au madini na hapo kila mkataba akubali kuitosa nchi.

Unashangaa 600m? Mbona hapa A-town ilitumika 2bil. Na mtu bado akakosa? Think twice. Lazima kuna ki2. Huwa tunasema madiwani hawana mishahara, lakini cha ajabu baada ya miaka 2 utamkuta anamiliki ghorofa, mkoko wa maana, nk.
 
sisiem tunaichukia kwa tabia hyo mama.sasa iweje na cc CDM tukae na watu wa namna hyo? tutakuwa wanaa tuu! huyo anatakiwa asepe kabisa
 
Aliyekuwa Mweneykiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya mwanasheria SAMBWEE SHITAMBALA amejiuzulu nafasi hiyo!

Anakabiliwa na shutuma za kupokea 600million toka kwa CCM na akuuuza ubunge kwa mchungaji wa CCM.
Shitambala Amedai kila akitaka kujieleza juu ya tuhuma hapati ushirikiano kutoka kwa mwenyekiti taifa bwana Mbowe.

Hili sasa ni pigo kwa CHADEMA - MBEYA

Mimi sishangai sana kwa sababu huyu bwana nilikuwa nategemea atafanya kitu kama hiki(kuchukua mlungula). Huyu bwana alipata kuwa mwajiliwa wa JWTZ kama mwanasheria wa Jeshi. Alifukuzwa kazi kwa kuwa alikuwa anachukua pesa upande wa pili na jeshi linashindwa kesi. So sishangai!!
 
Tarehe 3rd January 2009, niliandika hivi kuhusu Shitambala baada ya fomu yake ya kugombea ubunge kutupiliwa mbali katika uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini.

''..................Lakini pia inawezekana uongozi makini upo, ila navyomjua Shitambala ni mtu wa kujisikia sana na mwenye dharau kwa wattu wasio na elimu, maana hiyo LLM aliyoipata Uingereza inamchanganya sana.

Tatizo la kuota wagombea ndio hilo, chama hakina mfumo mzuri wa kupata wagombea. Tuwaulize CHADEMA, Shitambala alijiunga na chama lini na wapi, kadi yake ni na namba ngapi?, na lini alirudisha kadi yetu ya kijani?''

Huyu bwana asijifanye kujiuzulu arudishe kabisa kadi ya CDM (kama anayo), kuna ushahidi usio shaka kuwa alivuta kitu (sina uhakika) na amount lakini bila shaka ni fungu zuri kuhalalisha yeye kuukosa ubunge.

Tatizo ni kuwa hata kama uongozi wa juu wa CHADEMA ungeamua kuupuzia tuhuma hizi kama ulivyofanya wakati ule, hadhi ya chama huko Mbeya ingeporomoka maana ni stori mtaani kuwa jamaa alivuta mshiko.

kama mameno yapo, kujiuzulu ni heshima kwa chama, maisha yataendelea, chama ni watu na wapo.....
 
KAMA NI KWELI AMEFANYA HIVYO NA AONDOKE HATUTAKI MAJAMBAZI CHADEMA, NI HERI KUBAKI NA WACHACHE WA UHAKIKA KULIKO MAJITU MENGI YA KUJA KUTUHARIBIA 2015. GO! SHITAMBALA GO!:wave::wave:
 
Kweli nimeamini CHADEMA ni Chama Cha Demokrasia, yaani ukiwa na tuhuma za kuhujumu Chama au Taifa viongozi wake wanajiuzulu ili kupisha mchakato wa uchunguzi.

Laiti kama viongozi wa CCM wangekuwa kama Ndugu Shitambala, wanasiasa wangejiongezea heshima.

HIVI KAMA HUYU KITAMBAA ALIKUWA NAGOMBEA KWA MASLAHI BINAFSI, NA SASA CCM WAMEMFUPISHIA SAFARI YA KUPATA HUO MSHIKO ATAKAA CHADEMA KUFANYA NINI, AMESHAPATA ALICHOPATA NDIO MAANA KASEPA HAKUNA CHA UADILIFU WALA NINI HAPO, AMENIKERA:A S-cry:
 
Chitambala ni mtu maarufu sana Chadema hawakutegemea ataanguka na ndicho kilichompoza huyu bwana lakini kwenye siasa lolote laweza kutokea kama ilivyotokea kwa Lawrence Masha waziri wa mambo ya ndani wa zamani.

KAMA UNAVYOSEMA KWENYE SIASA LOLOTE LAWEZA KUTOKEA, BASI HATA HIYO 600M INAWEZEKANA AMEPOKEA:A S-alert1:
 
Back
Top Bottom