Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Inadaiwa kwamba tukio la awali la serikali yoyote duniani kupambana na ushoga ni lile lililotokea kule Marekani Julai 6, 1969. Mapambano kati ya Polisi wa nchi hiyo yalitokea kwenye kitongoji cha Greenwich jijini New York, kwenye baa iliyokuwa ikifahamika kama Stonewall. Baada ya kuwepo kwa taarifa ya baa hiyo kuwafuga mashoga, polisi waliandaa shambulizi kwa kisingizio cha kumkamata mwenye baa na wanywaji kwa kuendesha biashara ya pombe bila leseni.
Shambulizi dhidi ya baa hiyo lilifanywa saa 6:00 usiku hadi saa 8:00 ikiwa ni saa mbili za kamata kamata. Polisi wa awali ambao walikuwa ni wachache walikaribia kuzidiwa nguvu na mashoga ambapo ilibidi waombe msaada wa kuongezewa nguvu, vinginevyo mashoga hao huenda wangewaumiza au kuwadhuru zaidi. Katika mpambano huo Polisi wanne walijeruhiwa na mashoga kadhaa pia ambapo 13 walikamatwa. Ndani ya baa hiyo inadaiwa kwamba kulikuwa na zaidi ya mashoga au mashoga na wapenzi wao wapatao 200. Baa hiyo inadaiwa kwamba ilikuwa ikiendeshwa na kundi la kigaidi la Mafia.
Habari za shambulizi hilo iliandikwa kwenye gazeti la New York Daily News, la Julai 6 hiyo hiyo, lilinukuu baadhi ya kauli za mashoga hao. Baadhi ya wale walionukuliwa ni pamoja na Erick na Jackson ambao walikuwa ni wachumba na Bruce na Nan ambao pia walikuwa ni mke na mume. Mashoga hao walinukuliwa na gazeti hilo wakilaani shambulio hilo kwani walisema lilikuwa limevuruga harusi iliyokuwa ifanyike Julai 7, yaani siku inayofuata kati ya Erick na Jackson.
Mama mmoja anayeishi jirani na eneo hilo, Shirley Evans aliliambia gazeti hilo kwamba, mashoga kwenye baa hiyo walikuwa ni watu waungwana sana na kamwe hakuwahi kusikia vurugu au ugomvi ndani ya baa hiyo. Kwa hiyo kuvamiwa kwao na Polisi alikuona kama uonevu tu.
Kumbuka hiyo ilikuwa ni mwaka 1969, wakati huku kwetu hata uchangudoa lilikuwa ni jambo la aibu sana na la kushangaza.