Shinyanga: Kiongozi wa CHADEMA aumizwa vibaya, akimbizwa hospitali

Lu-ma-ga.Tunakupenda bado tunakuhitaji nenda taratibu usitoboe sana bado tuna muda mrefu humu ndani punguza spidi jamaa yangu,bado nahitaji mchango wako,isipokua umekua na spidi tangu hii thread imekuwa hewani,hoja zako nzuri nakuunga mkono lakini twende taratibu.punguza kidoogo.

Kumwambia lumaga apunguze spidi ni kumtia uoga. Uoga ni mwiko kwa great thinkers. Lumaga funguka. Ulizaliwa siku moja na utakufa siku moja.
 
Sisi tulio nje tunapata sura ya nchi inayoyumba na kuelekea pabaya. Pengine hiyo ni taswira ya Forum tu, lakini kuna ukweli fulani.
Sasa ninachosema, bunge la Tanzania liko tayari kuona nchi inaangamia bila ya kuchukua hatua zozote? Hakuna kitu kinachoitwa 'vote of no confidence' dhidi ya rais. Juzi ni Zanzibar, leo Shinyanga, kesho..... na katika matukio yote wananchi ndiyo wanaoumia. Zile nchi tulizokuwa tunazicheka kwamba wanauana wenyewe kwa wenyewe, mambo yalianza hivi hivi!
 
Mungu wangu! Taarifa nyingine zinaumiza na kutia hasira!! Kwa hiyo mpaka sasa saa saba hii, polisi hawajafanya jitihada zozote? Na majeruhi anaendeleaje?? Tupeni update mlioko karibu. By the way polisi inabidi mjitathimin na huyo Nchimbi wenu, itafikia pahala tukio kama hili likitokea alafu polisi wasichukua hatua mapema, vijana tutaingia barabarani na kuzingira kituo husika ndo mtakuwa na adabu... Hata hamtutishi na mabom yenu ya machozi kwani ninakumbuku msemo mmoja niliwahi kuusikia kwenye picha ya SARAFINA kwamba"PEOPLE CAN DEFEAT THE ARMY"ni vema polisi mtimize wajibu wenu kabla hayajatokea mabaya zaidi.
 
Kumwambia lumaga apunguze spidi ni kumtia uoga. Uoga ni mwiko kwa great thinkers. Lumaga funguka. Ulizaliwa siku moja na utakufa siku moja.

Sikia mkuu umenielewa vibaya siwezi kumtisha hata kidogo jaribu kuangalia namna ambavyo lu-ma-ga alivyofunguka kwenye coment zake,amekwenda kwa spidi kubwa sana na kashusha vitu vizito ambavyo vinaonekana vina ukweli mkubwa ndani yake,sasa kwa mtu mwenye busara kama mimi na mtu ambaye.........nt.ndiyo maana nimemwambia kwamba a take time kidogo katika kushusha vigongo hivy,tunataka tuvione ndiyo lakini aende hatua kwa hatua.

kwa sababu ametiririka kwa kasi mnooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kazi ipo!. Pole sana kamanda hali si shwari sehemu nyingi, LAKINI INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU YUPO TUTASHINDA!!!. Hivi sasa mahali popote penye harakati za chadema kuna vitisho vya CCM!.. Leo nipo bagamoyo. Taarifa za kuaminika nilizopata: CHADEMA wameikalia kooni CCM katika kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Magomeni jimbo la Bagamoyo. Mpiganaji anayeongoza Jahazi hili nimemjua kwa jina moja BONI wa UBUNGO!.. Jana jioni CCM wamemlilia mkuu wa wilaya Bagamoyo Bwana Ahmed Kipozi na kamati yake ya usalama wa wilaya waidhibiti CDM kwa namna yoyote ili CCM ishinde!.. Usiku wa kuamkia leo wanachama wa CDM 6 wanaotembea nyumba kwa nyumba maeneo ya majikosti, kitame, nianjema, Bong'wa, Kidongo chekundu, Kimarang'ombe na sanzale wametishiwa maisha!. Kazi za CDM sasa zinafanywa kwa tahadhari kubwa na makundi ya kujilinda!.. Mgombea wa CCM anatokea MWANANYAMALA DAR Anakoishi na mkewe Khadija Kopa, Anaitwa YUSUFU, na MGOMBEA wa CDM anaitwa SETEBE.
ccm watahatarisha umoja na mshikamo wa taifa letu kwa ulevi tu wa madaraka!
 
anaitwa BONIFACE JACOBO diwani tokea ubungo,hilo ni jembe la ukweli mkuu!...harakati zake zilionekana tangu mapema akiwa form2 kule upareni kwenye shule moja ya wasabato. Ki ukweli ni mpambanaji wa kutetea haki, tumuombee aongoze jahazi vema na MUNGU amkinge na hivyo vitisho!
 
La msingi ni kumbukumbu ziwekwe kwa matukio yote ya mauaji au vitendo vinavyokiuka haki za binadamu na CCM na serikali hawataki kuvishughulikia kwa sababu za kisiasa na ubabe wao. Kisha baada ya 2015 wahusika washughulikiwe. Mbona wa NAZI wa vita kuu ya pili bado wanakamatwa mpaka leo?hilo litakuwa fundisho kwa
Wa kutenda maovu kwa kutegemea dola iliyopo madarakani.
 
Yana mwisho. Kwani wahenga walisema hakuna marefu yasiokuwa na ncha.

Ni kweli mkuu lakini,tutakuwa tumeumizwa sana na hata kupoteza maisha sisi wenyewe kama siyo wapendwa wetu,hebu

Mungu auwahishe huo mwisho maana inaumiza sana mambo yanayotendeka sasa na wanaotakiwa kuwajibika hawajari

kwasababu tu yanatokea kwa mtu fulani na siyo mtu fulani kwakweli inahuzunisha sana!.....
 
Hivi yale mashitaka ya kule The Hague yaliyofunguliwa na mama Helen Bi Simba yamefikia wapi? Maana Magamba yanazidisha umafya wa kutisha sasa.
 
Ugonjwa huu ulianza polepole. Zimekuweko habari magazetini na hapa JF miaka ya nyuma kidogo kwamba vijana wa CCM walifanya "semina" ya maandalizi ya uchaguzi mkuu kule Singa Chini (Moshi). Alikwenda Katibu Mkuu wakati ule (Makamba) akawahamasisha kwa kuwaambia "dola ni yao, hakuna mtu anaweza kuwafanya lolote".

Kisha walihutubiwa na Rais Kikwete ambaye naye aliwapa ujumbe huo huo aliotoa Makamba.

Semina ilipokwisha vijana hao waliandamana, na walipofika KCMC kuna watu waliwanyoshea ishara ya vidole viwili. Walikasirika wakapiga watu hovyo hovyo hospitalini. Polisi walikuweko lakini hawakufanya lolote.

Yanayotokea ni mwendelezo wa hayo waliyoambiwa. Na hakuna anayewafanya lolote.

Shimbo alipotoa vitisho CDM ilishirikisha mabalozi wa nchi za nje, na mafanikio yalionekana.

Nashauri uongozi wa juu wa CDM uandike barua kwa wawakilishi wa kimataifa Dar, na kwa Tume Ya Haki Za Binadamu. Barua itoe muhtasari kamili wa ukiukwaji wa haki za binadamu unaotokea sasa Tanzania, na izitake jumuiya za kimataifa na nchi wahisani kutoa tamko kukemea hali hii.

Wengi wanasema "tunaelekea pabaya". Hatujafika kweli?

Pamoja na hayo yote, tusikate tamaa. Makaburu waliua sana lakini wakasalimu amri. Mubarak wa Misri alijaribu sana kubaki madarakani kwa kuua lakini anasubiri kufia kifungoni.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwanini wanayafanya haya sasa? Na kwanini hawajui kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho kwa maana imesemwa auaye kwa upanga naye atauwawa
 
Back
Top Bottom