Shinyanga: Kiongozi wa CHADEMA aumizwa vibaya, akimbizwa hospitali

Huyu GAKI alikuwa jambazi wa magari sana miaka ya 1990-1995 amepata pesa baada ya yeye na swahiba wake salumu mbuzi kupewa network wakati JK akitafuta kuingia ikulu, pia wamekiibia sana chama cha ushirika na kuwadhurumu mameneja wa shirecu.kifupi viongozi wa ccm shinyaga wote ni wafanyabiashara HARAMU utajiri wao ni questionable wana-shy town wanahitaji kufanya kweli si kupiga kura na kuondoka kama walivyofanya kwa maselle kumpa ujiko asiostahili.Uchaguzi wa mwawaza lazima uwafute machozi wana CDM kwa kupokwa ushindi wa marehemu shelembi.
mamaaa ndo ccm wanayoitetea watu hapa jf mpaka wanatukanana, ccm haifai hata kuwa chama cha upinzani kwa hali hii.
 
wakuu,

habari nilizozipata punde ni kuwa mwenyekiti wa chadema tawi la mwawaza katika manispaa ya shinyanga (jina sijalipata vema) amechomwa mkuki usiku wa kuamkia leo mpaka utumbo ukatoka nje. Amekimbizwa hospitali muda si mrefu ili kuyanusuru maisha yake.

Mwandishi aliyechukua tukio hilo ameanza kusumbuliwa sana na watu wanaohisiwa kuwa viongozi wa ccm ili kuiharibu kamera yake.

chanzo: mashuhuda walio eneo la tukio



tutangulize pole kwa mashaka makubwa kama hayo
pili tupeane uhakika wa hzo taarifa
wanasiasa watayagharim maisha yetu hadi lini??
 
Habari mbaya sana hii lakini hiyo ndio hali halisi kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wa raia vimeshindwa kutimiza wajibu wake. Na hiyo ni baada ya kukubali kubinafsishwa kwa ccm hali inayopelekea ccm kufanya kila aina ya maasi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

Nadhani huko tunakoelekea tutalazimika kutafuta mbinu za kujilinda sisi wenyewe, hasa tunapokuwa katika michakato ya uchaguzi kwani matukio ya kuvamiwa, kujeruhiwa na kuuwawa kwa viongozi wetu nyakati za uchaguzi yamekuwa yakiongezeka kila kukicha.
Hakuna jambo la hatari kama suala zima la usalama(security) linapokuwa politicized!!watu wnakosa imani na security system iliyopo waanza kujichukulia sheria mkononi!
 
nIMEWAHI KUKAA SHINYANGA HUYU CHARLES SHIGINOnamfahamu ni mtu katili sana hana ubinadamu hata kuongea kwake.Niliwahi kuishio naye ngokolo nilikuwa namuogopa sana na hata mali za dukani kwake alizokuwa anauza zote zilikuwa questionable.nashangaa leo eti ni kiongozi wa ccm,kama hali ndiyo hiyo cdm should be very careful.Mashishanga should exercise care and caution hasa wakati wa kuhesabu kura. Shigino ni katili asiye na ubinadamu shy towners they know outright
Huyu bwana,alishinda kura ya maoni udiwani CCM kata ya Ngokolo SHY mjini,lakini lakini jina lake lilikatwa kwa kwa kujua wapinzani wake wataitumia kashfa aliyonayo ya ujambazi. Cha ajabu,eti amekuja kupewa ukatibu wenezi!!
 
Hao CCM Shinyanga walikuwa hawajajua maana ya peoples Power sasa kupitia upuuzi huu chamoto watakiona ngoja makamanda watie timu patifuke haswa!!
 
Get well soon Kamanda,Mungu wetu ni mwema na wadhalimu anazidi kuwaumbua,kama chaguzi ndogo hata za madiwani wanaua hivi huko mbeleni itakuwaje??Namsubiri TENDWAAAA ataropoka nini safari hii.
 
Tunakoenda ni kama ya majirani, tutaishia kwenye mauji ya kimbari!!!

Lord have Mercy on us.
 
Kazi ipo!. Pole sana kamanda hali si shwari sehemu nyingi, LAKINI INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU YUPO TUTASHINDA!!!. Hivi sasa mahali popote penye harakati za chadema kuna vitisho vya CCM!.. Leo nipo bagamoyo. Taarifa za kuaminika nilizopata: CHADEMA wameikalia kooni CCM katika kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Magomeni jimbo la Bagamoyo. Mpiganaji anayeongoza Jahazi hili nimemjua kwa jina moja BONI wa UBUNGO!.. Jana jioni CCM wamemlilia mkuu wa wilaya Bagamoyo Bwana Ahmed Kipozi na kamati yake ya usalama wa wilaya waidhibiti CDM kwa namna yoyote ili CCM ishinde!.. Usiku wa kuamkia leo wanachama wa CDM 6 wanaotembea nyumba kwa nyumba maeneo ya majikosti, kitame, nianjema, Bong'wa, Kidongo chekundu, Kimarang'ombe na sanzale wametishiwa maisha!. Kazi za CDM sasa zinafanywa kwa tahadhari kubwa na makundi ya kujilinda!.. Mgombea wa CCM anatokea MWANANYAMALA DAR Anakoishi na mkewe Khadija Kopa, Anaitwa YUSUFU, na MGOMBEA wa CDM anaitwa SETEBE.
 
Hakika taifa letu liko mashakani, wimbo wa amani unatoweka pole pole, tuwe na kiasi.... tutafakari! pole sana kamanda tuko pamoja
 
Sasa sisiem ni nini wanaitaka jamani?
Wameshindwa kusoma alama ya nyakati??

MUNGU MWENYE MAMLAKA JUU NA CHINI,TUNAKUTAJA TENA MAANA INATUPASA BWANA,TUKAKUONE UKIWAADHIBU HAWA MAFISADI KWA MKONO WAKO MUNGU WETU! Usitupite Bwana kwani hakika mwenyewe unaona ndg zetu wanachofanyiwa na wanyang'anyi wa madaraka!

Mkono wako wenye mamlaka ukaonekane MUNGU wetu!
 
Kwanza kabisa nampa pole huyo ndugu yetu anayepigania maisha yake hospitali.

Pili napenda niseme wazi kuwa kumekuwa na uzembe hali ya juu kwenye kushughulikia matukio ya watu kujeruhiwa au kuuwawa kwa sababu za kisiasa. Hii inaweza pia kuwa ni mkakati makusudi. Swali ni kwamba, wanaofanya haya wanatoa wapi ujasiri huo? Jibu mnaweza kuotea.

Kwa yeyote ambaye yuko behind haya matukio ya kinyama ajue kabisa kuwa hakuna aliyeweza kuzuia mabadiliko pindi wananchi wanapoamua kwa dhati. Historia ni mwalimu mzuri sana. Iko siku yatawakumba.
 
Back
Top Bottom