SHINIKIZO:John Tendwa jiuzulu

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
watazania mnaopenda kuona haki inatendeka mmtakubaliana na mimi kuwa kuna umuhimu wa msajili wa vyama ndg john Tendwa anatakiwa kujiuzulu mara moja.

Kauli zake mbalimbali katika chaguzi mbalimbali zimeonyesha kuwa ni adui namba moja wa haki.

Mara nyingi amesikika akitoa kauli kandamizi kwa vyama vya upinzani.
Pia ameonekana ni mtu asiyejua wigo wa majukumu yake.
Mara nyingi anaingilia majukumu ya tume ya uchaguzi,vyombo vya usalama au mamlaka za kimila kama tulivyoona huko arumeru mashariki.

Wakati umefika kwa wale wote wanaotumia vyeo vyao kukandamiza haki wawajibike au wakutane na tsunami la nguvu ya umma.
 
Naona saa hizi anaona aibu kwa kauli zake alizotoa, ukijifanya mwelevu sana mwisho unakuwa mjinga sana.
 
Pamoja na kauli zake,Mungu akisema NDIYO, hakuna anayezuia!
Abadilishe style!!!
 
Nafikiri anahitajika kutoengemea chama chochote ndipo kazi yake ataifanya vizuri na anapaswa kujua pia watu wengine wamejaliwa uelewa mkubwa wa kupambanua mambo.
 
Tendwa alimtishia lema dhidi ya washili
Tendwa aliwataka wananchi kupiga kura na kuondika vituoni kinyume na matakwa ya kisheria!
 
Anapaswa kusoma alama za nyakati, kwa sasa vijana hatuna mchezo wala mzaha, tunapigania kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa kundi la wanyang'anyi waliopewa utawala na Tume ya uchaguzi.
 
Anapaswa kusoma alama za nyakati, kwa sasa vijana hatuna mchezo wala mzaha, tunapigania kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwa kundi la wanyang'anyi waliopewa utawala na Tume ya uchaguzi.
nimeshuhudia vijana wasio na kadi za chadema wakipiga kampeni,waklinda kura na wakikubali kuumizwa kwa mabomu bila malipo yoyote.
 
Tendwa naye sijui nani huwa anamtenda mara oooh Washiiri wamempiga marufuku Lema kufika Arumeru mara ooooh Washiiri chagu lao Sioi huyu jamaa mnafiki sana. Vizee kama hv inabidi tuvipumzishe kwa amani mahala pa moto amen
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom