Shimo gani linalokukera?

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,301
Habari za asubuhi wapendwa,

Leo nimeamua kuja na swali hili kutaka kujua shimo gani la barabarani linalokukera. Mimi binafsi nakerwa sana na shimo lililopo makutano ya barabara ya bibi titi mohamed na morogoro na lile kwenye barabara ya united nation kwenye kona ya kuingia muhimbili.

Nasdhani kwa mashimo yaliyopo kwenye barabara zetu hakuna haja ya kuweka matuta kwani yanasaidia kupunguza speed kwa kiasi kikubwa na kuchangia foleni kwa wale wasiopenda kuwahi kurudi majumbani hii ni faraja kwao.
 
Mmh, kaka, mbona yako mengi mno? Mimi naishi ukonga, kuanzia kanisa la Lutheran mpaka baada ya Mombasa hapo kati ni mashimo (au sijui uwazi, manake nikisema mashimo nayapandisha chati).

Hayo ya kona ya kuingia muhimbili, nafikiri ni sehemu ya barabara, hakuna mpango wa marekebisho.
 
Jana nilipita ile barabara ya uhuru, pale buguruni sokoni/police lile sio shimo bali barabara imekatika, harafu hakuna juhudi zozote zinazofanyika kunusuru ile hali
 
Wekeni na picha ili kuweka msisitizo na pengine watasikia na kuona maana hayo mashimo ne kero ya Taifa, kila barabara hukosi shimo!
 
Fungeni tyre za sport au mtembelee defender 110 mtasahau mashimo but remember to hold your breath.
 
Bora ya mashimo, kuna bump ya hatari sana pale kati ya Bar ya maarufu ya LENANA na barabara inayopanda kwenda Ilboru Sec.
Yaani hapo hata ukikwepeshaje chombo lazima sampu isuguane na hiyo bump..... ha ha haaaa!
 
Wekeni na picha ili kuweka msisitizo na pengine watasikia na kuona maana hayo mashimo ne kero ya Taifa, kila barabara hukosi shimo!


We we nae unakuwa kama Thomaso picha za nini sasa kwani wewe hutumii hizo barabara agrrrrrrrrrr
 
Kuna shimo lipo hii barabara wanayotengeneza kigogo wanaita sijui randa bar kitu kama hicho hilo shimo ni balaa halafu linamaji kiherehere chote cha kukwepa foleni ya morogoro kiliniisha maana hapana na haka kavitz kangu nusu kazame hapo
 
Barabara nyingi ni mahandaki sio mashimo
kama barabara ya TANESCO ilipokuwa office ya Tigo zamani
 
Mwanza....Makutano ya kenyatta na Pamba Road.....Kama unapanda na kama unashuka kwenda barabara zote hizo.....usipokuwa makini ream yote ndani,Njia ya kuelekea nyegezi...kuna sehemu imetengenezwa porpose ya ku pumzikia magari makubwa ,pale kuna vitu kama vents hivi zile zinakuwa juu ya mtalo....ebana zimevunjika vinjia ni mwaka wa tatu sasa naziona ziko vile sasa kwa wale wanao penda kukwepa ila bumps pale kwa kupita kushoto au kulia ukitokea mjini au nyegezi...habari yao wanaipata....

Kuna rafiki yangu aliacha deaf ya Land Cluser pale kwa kujisahau kuwa pale kuna mashimo.
 
Jana nilipita ile barabara ya uhuru, pale buguruni sokoni/police lile sio shimo bali barabara imekatika, harafu hakuna juhudi zozote zinazofanyika kunusuru ile hali

Duh, lile linakera hadi basi kama lile la UN pale wanapopasema jamaa
 
Kuna hili shimo sijui tuite handaki? Lipo hapa mtaa wa upanga karibu na haidar plaza yaani ni nouma unaweza hata ukajificha usionekane. Hivi wahusika wa kufanyia ukarabati wameenda likizo?
 
Duh, lile linakera hadi basi kama lile la UN pale wanapopasema jamaa

Sasa hilo la UN road si bora lipo barabara ya ndani ndani lile la bibi titi mohamed na morogoro rd linatia aibu kwani kila mgeni anaeingia TZ akitokea airport kama atakuwa anaenda holiday inn, movenpick, kempinsk, new africa au southrn sun lazima aliingie na kuambiwa karibu tanzania hakuna matata
 
Last week nilipita mbagala nikielekea rufiji...YALE NI BALAA...hapafai,, ni mbagala rangi 3 pale mwisho...mh!
 
Back
Top Bottom