Shikamooni!

Tisha-TOTO

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
1,175
604
Shikamooni Wakuu,
Jina langu si hoja. Adabu iko palepale kwenu wakulu...

Shalom!
 
.....umetumia vipimo gani kujua huku ndani wote ni jijeba kuzidi wewe?
n wei....karibu kijiweni TOTOs!
 
Karibu sana
Lakini imajini unapewa kipaza sauti ubungo Stand halafu unaamkia watu wote... habari zenu ingekuwa muafaka zaidi.
Tena, Karibu sana Tishwa -Toto ;)
 
Kiranga na wewe .....hahaaaaaa nicheke tu mie?? maana yake nini kwanza 'shikamoo'?

Maana yake "nakushika miguu yako" au "niko chini ya miguu yako". Ni salamu iliyoanza kutumika katika enzi ya utumwa, watwana na watumwa wakiwaamkua mabwana zao, yaonyesha nani mtwana/mtumwa na nani bwana.

Ndiyo maana kuna wazee wengine wanaoielewa maana yake ukiwaambia hawasemi "marhaba" wanasema "ahsante" au wengine wanakataza kabisa kuamkiwa shikamoo.

Kama unaelewa historia ya biashara ya utumwa, na unaelewa historia ya shikamoo, na una utu wa ku sympathize na weusi walivyoteswa, huwezi kukubali shikamoo.
 
afadhali umenifumbua macho maana kuna wababa wengine ukiwaambia shikamoo wakisema asante najua ndio wale wale.......fataki
 
Shikamoo ni chakula ya babako sisi hakitufai!!
Niwie radhi kama nimekukosea mkuu na wakuu wengine wote. Kupotea njia ndio kuijua. Naomba mnielimishe kidogo namna gani iliyo bora ya kuonyesha heshima unapowaamkia unaowaheshimu?

Shalom!
 
Heshima haina umri ni kwa anaye staili. Hata kama mfal,e ana miezi sita lazima tupinde mgongo
 
Wakuu mimi Mfipa, kutokea Sumbawanga,
Sijavibeba vichupa, hivyo mimi siyo mwanga,
Tabanana hapahapa, Dar pande za Keko Mwanga,
Msinicheke ushamba, mnitoe tongo-tongo!

Kwa kweli ushamba umo, naomba kuvumiliwa,
Nasabahi kwa shikamoo, kumbe hili kosa kubwa!
Nahitaji pata somo, kutoka kwenu wakubwa,
Msinicheke ushamba, mnitoe tongo-tongo!

JF ni bahari, iliyojaa hazina,
Najisikia fahari, kuwakuta waungwana,
Ninawatakia heri, ya mwaka mpya mwanana,
Msinicheke ushamba, ila mnipige shule!!
 
wewe mdogo wake katavi?,,,,haya mashairi yako ngoja mwanakijiji aje akujibu
 
Wakuu mimi Mfipa, kutokea Sumbawanga,
Sijavibeba vichupa, hivyo mimi siyo mwanga,
Tabanana hapahapa, Dar pande za Keko Mwanga,
Msinicheke ushamba, mnitoe tongo-tongo!

Kwa kweli ushamba umo, naomba kuvumiliwa,
Nasabahi kwa shikamoo, kumbe hili kosa kubwa!
Nahitaji pata somo, kutoka kwenu wakubwa,
Msinicheke ushamba, mnitoe tongo-tongo!

JF ni bahari, iliyojaa hazina,
Najisikia fahari, kuwakuta waungwana,
Ninawatakia heri, ya mwaka mpya mwanana,
Msinicheke ushamba, ila mnipige shule!!
Wee ni mfipa kweli? Mbona una mashairi ya kimwambao? Au ndio ile pwani ya Lake Rukwa??!
 
Uniwie radhi, mie wa mwamba rukwa
Hata kama si shwari, sie hakujakuchuchwa
Mmjj akija jamvini, mbona hapatakuchwa
Mmmmmm nini nini, hata kule utaumwa
 
Back
Top Bottom