Shida ya Maji/Umeme Shinyanga

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Baada ya Mikoa ya Shinyanga na Tabora Kuwa katika gizani kutokana na hitilafu Kwenye transfoma inayopeleka umeme katika mikoa hiyo, sasa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wamekumbwa na uhaba mkubwa wa maji.

Habari kutoka huko zinasema dumu la maji (lita 20) limefikia shilingi 800 kwa leo na pia mawasiliano ya simu za mkononi yamekuwa magumu kwa walio wengi.

Kuna hatari kuwa magonjwa ya milipuko kama kipindu [indu yakaingia katika manispaa ya shinyanga ambayo huko nyuma ilikuwa na historia ya uswahiba na magonjwa na kuhara, hadi hapo baadhi ya watendaji wa Idara ya Afya walipoadabishwa.
 
Back
Top Bottom