Shida na matatizo tuliyonayo watanzania kwa sasa ni haki yetu-tusilalamike

mambomoto

JF-Expert Member
May 10, 2011
326
236
Nalazimika kusema hivyo kwa kuwa Watanzania tumekuwa watu wa kulalamika na kusahau na siku zinasonga mbele. Mtanzania ni mtu ambaye anaamini kila mtu ataubeba mzigo wake peke yake. Ndiyo maana hata linapotokea jambo muhimu lenye maslahi kwa taifa bila kujali chama, dini, kabila, rangi nk Watanzania tumekuwa wagumu sana sana kuungana na kuwa kitu kimoja. Isitoshe tumekuwa watu wa kulalamika chinichini na mwishowe tunanyamaza na siku zinasonga mbele katika hali mbaya na ya kukatisha tamaa mno. Maisha ndugu zangu yanapanda kila siku tena kwa makusudi utafikiri tunakisa nayo. Jambo la kujiuliza kweli watanzania miaka 50 tangu tupate uhuru hakuna afadhali ya maisha chini ya chama cha CCM???. Mbona wao wananeemeka na sisi tunateseka? Kweli ndugu zangu bila kujali tofauti zetu tunahitaji mabadiliko kama kweli tunataka kupona sisi na vizazi vyetu. Wakati wa uchaguzi wengi hatuna umakini wa nini tufanye. Kilio kingine ni baadhi ya wanawake wa Tanzania ambao ndiyo janga tulilo nalo kwa sasa katika kuikomboa nchi hii. Wanawake/ Mama zetu/ Dada zetu kweli mmekuwa mkituangusha sana wakati wa uchaguzi kwa Khanga, Vitambaa, T-shirt, Vilemba, Pilau amabazo mkishapewa tu mnaimba na kuimba kutwa nzima mwishoni mnauza uhuru wenu. Je leo hii matatizo ugumu wa maisha tulionao tumlilie nani?? Hii ni haki yetu hatupaswi kulalamika
 
Back
Top Bottom