Shibuda: Wanaopinga posho ni madomokaya na wahuni

Mnamwonea tu Shibuda, mh.Selasini wa Rombo naye alisema kabisaaaaaa bungeni kuwa posho ni ndogo sana na wanaopinga wana ajenda zao za siri pia kina Regia na wengine wengi wa CDM posho wanazitaka sana ila wanasemea chini chini. Shibuda ni muwazi.
 
I wanna kill right now!??!!!? Life tight kuna mtumishi analipwa 146,000 Kwa mwezi afu ye posho ya laki mbili kwa siku haitoshi na huku bidhaa na huduma tunapata kwa bei moja. Yaani niko tayari kuwa recruited kwa wapambanaji watakaotaka kuingia msituni sanduku la kura halitatuokoa ikiwa wabunge wenyewe ndo hawa na vyama venyewe ndo hivyo Damn it

tuko pamoja
 
Kuwa na Shibuda ni mzigo mkubwa kama kubeba gunia la misumari.....mzee wa ujira wa mwiha!! Pumbavu!!
 
Tatizo, hii inakuwa kama kila mwana CDM anakuwa na mtazamo wake. Chama kinatakiwa kuifanya agenda ya chama. Baada ya hapo anayekuwa against anaweza kushughulikiwa fairly.
 
dah, katika Chadema kuna wabunge wawili siwaaminigi kabisa; Shibuda na Joseph Selasini. Hawa watu hawana hadhi ya Chadema na next election zifanyike jitihada za makusudi kuweka wagombea ubunge through Chadema wenye ubora.
 
I second this.
Mlishasikia akichangia kitu gani cha maana bungeni?
Yule lazima utetezi wa haki za binadamu unaopigiwa kifua na Cameroon, Clinton na Obama utakuwa unamhusu sana yule.

ha ha!
 
SHIBUDA ACHAFUA HEWA CHADEMA
MBUNGE wa Maswa Magharibi (CHADEMA), amechafua hali ya hewa ndani ya chama hicho baada ya
kuwaita viongozi wake na watu wa kada mbalimbali wanaopinga ongezeko la posho za wabunge kuwa ni domokaya wanaotafuta umaarufu wa kisiasa mbele ya jamii. Shibuda ambaye maelezo yake yaliwashangaza baadhi ya waandishi wa habari aliokutana nao jana jijini Dar es Salaam, alidai kuwa viongozi wa siasa wanaopinga ongezeko hilo la posho ni makuwadi wa watu wa nje ambao wameanza na suala hilo lakini si ajabu kesho wataunga mkono ushoga. Alisema tangu lilipotangazwa jambo hilo, kumekuwa na msukumo kwa baadhi ya wanaharakati, viongozi wa vyama vvya siasa pamoja na baadhi ya wabunge kutaka kuligeuza jambo hilo kuwa la kisiasa, ilhali ilani za vyama hazizungumzii jambo lolote kuhusu posho.

Mbunge huyo alisema hivi sasa kuna kundi la watu linafanya kampeni inayoweza kuchochea chuki kwa wananchi dhidi ya serikali na wawakilishi wao bungeni, huku wakitumia shida za wananchi kwa maslahi yao. Shibuda alisema baadhi ya wanasiasa wamekuwa mabingwa wa kutuhumu upande mwingine, wakati wao wenyewe hawajitazami usafi wao mbele ya jamii.


Katika kauli iliyoonekana kumwelekea zaidi Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Shibuda aliongeza kuwa wapo wanasiasa waliojidai kukataa kutembelea magari waliyopewa na serikali, hata kufikia hatua ya kuyarudisha, lakini wanaonekana wakitamba na magari ya kifahari. "Hapa kuna misukumo na hamasa ya kutuhumu upande wa kushoto bila wao kujitazama wana utakaso wa kiasi gani mbele ya jamii… kuna watu walikataa kutembelea magari na hata kufikia kuyarudisha lakini ukikutana naye anatembelea gari la kisasa na la kifahari je, huu ni uadilifu au ndiyo kutaka umaarufu usiokuwa na masilahi kwa Watanzania?" alihoji Shibuda.

Mbowe akiwa kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ndiye aliyekataa kupokea gari la kifahari alilopewa kwa mujibu wa nafasi yake na kuamuru lirudishwe serikalini. Tofauti na Mbowe aliyekataa gari kupinga matumizi makubwa ya fedha ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyekataa kupewa gari jipya akisema haoni sababu kwa vile lile alilokuwa nalo bado ni zuri na linafaa. Naye, kama ilivyokuwa kwa Mbowe, aliamuru lirudishwe serikalini ama liuzwe na fedha zielekezwe katika matumizi mengine ya kijamii.


Alisema kundi hilo linalopinga posho hizo, lingekuwa na uchungu kwa wananchi wake, lingeibua mikataba mibovu ili kuwasaidia Watanzania kunufaika na madini.
"Kupandishwa kwa huu ujira wa mwiha (posho), kwa wabunge ninaunga mkono hatua hii na kutokana na msimamo wangu ambao ni haki yangu, nipo tayari kwenda katika jimbo lolote au mkoa wowote nchini ili kutoa elimu kuhusu jambo hili," alisema Shibuda.

Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akitofautiana na msimamo wa chama chake alichojiunga nacho dakika za mwisho wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, baada ya kutoswa na chama chake cha zamani, CCM. Tangu ajiunge na CHADEMA, Shibuda amekuwa akitofautiana mara kwa mara na msimamo na maazimio ya chama hicho, hali ambayo iliwafanya baadhi ya viongozi na makada wake kutaka atimuliwe.
 
WABUNGE CCM WAFURAHIA ONGEZEKO LA POSHO

Wakati Shibuda akiwashambulia viongozi wake, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesherehekea kupandishwa kwa posho zao, wakidai kuwa wao ni watu wenye heshima ya mbunge wanaostahili kuishi na kufanya kazi katika mazingira mazuri na salama. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Rita Mlaki, alipongeza uamuzi huo kwa madai kuwa hutumia fedha nyingi awapo Dodoma kuliko anayolipwa na Bunge. Alisema nyumba aliyopanga huko Dodoma hulipa kodi ya sh 350,000 kwa mwezi, ingawa anaitumia kwa muda mfupi tu, hivyo fedha nyingi zinapotea bure. "Mafuta tunayopewa ni kidogo, fedha za madereva haziwatoshelezi, hivyo ni lazima nihakikishe dereva awapo Dodoma anaishi vizuri na kumlipia chumba kizuri…naupongeza uamuzi huu wa serikali," alisema.

Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, alisema mbunge si mtu binafsi, bali ni taasisi hivyo kama taasisi inahitaji fedha za kujiendesha.Simbachawene ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, alisema shughuli za mbunge si kama za mkulima, mfanyabiashara au mtu yeyote yule, hivyo zinahitaji kuenziwa na kuheshimiwa kwani hufanya shughuli nyingine za hatari ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yao. "Kama unasafiri kikazi, unahitaji usafiri mzuri, sehemu nzuri na salama ya kulala lakini mazingira salama zaidi kwa kuwa tunafanya kazi za hatari, tunakemea maovu na maovu hayo hufanywa na watu wenye uwezo, hivyo tunahitaji ulinzi wa kutosha. "Haiwezekani mbunge akalala nyumba ya wageni ya sh 5,000 au umkute anakula gengeni, lakini wakati mwingine watu wanatufuata wanahitaji misaada, fedha ni hizo hizo," alisema.

Aliwafananisha wabunge na wanafunzi 12 wa Yesu Kristo, kwa madai kwamba alipokuwa akiambatana nao haikumaanisha kuwa aliwadharau Wakristo wengine na kuwapenda wao tu, hivyo hata wabunge kuongezewa posho haimaanishi Watanzania wengine wanadharauliwa. Kwa mujibu wa Simbachawene, wabunge wa Tanzania ndio wanaolipwa posho ndogo sana ikilinganishwa na wale wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Nao wabunge wa vyama vya CUF na NCCR-Mageuzi walisema nyongeza hiyo si mbaya, lakini wakaishauri serikali kufanya uwiano wa nyongeza za posho kwa mihimili mingine ya dola, vinginevyo nchi haitatawalika. Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Mnyaa, alisema gharama za kuishi Dodoma ni kubwa na kwamba hadhi ya wabunge wa Tanzania ni tofauti na wabunge wa nchi nyingine hasa za Afrika kimasilahi. Alisema mbunge ni kioo cha jamii, hivyo aliwashangaa baadhi ya watu kuhoji nyongeza zao badala ya kuhoji vitu vya msingi. "Mbona wafanyakazi wengine kama wakurugenzi wanalipwa fedha nyingi sana, lakini haihojiwi na isitoshe fedha zetu zinarudi kwa wananchi hao hao. Mjadala huu una lengo la kuchonganisha wabunge na wananchi wao," alisema. Hata hivyo alisisitiza kuwa kupanda kwa maisha si kwa wabunge tu, bali hata na wananchi wengine, hivyo suala la kupandisha posho, mishahara na marupurupu liangaliwe kwa upana wake.

Mbunge wa Uvinza, David Kafulila, alisema ipo haja serikali ikaongeza viwango vya mishahara na posho nyingine kwa mihimili yote ya dola, yaani Bunge, Mahakama na serikali. "Suala hili liangaliwe kwa watumishi wote. Maisha magumu si kwa wabunge tu. Kuwe na mfumo mzuri wa kurekebisha mishahara kwa mihimili yote si Bunge pekee…Tanzania hakuna uwiano wa mishahara kwa mihimili hii," alisema. Kafulila alisema wabunge wanapo pa kusemea katika kudai masilahi yao, lakini wafanyakazi wengine hawana, hivyo aliishauri serikali kuandaa mfumo mzuri.
 
Mh Zitto naamini wewe huwa unapita humu,tunaomba hili mlichukue kama jambo muhimu,nazidi kupata mashaka sana na huyu Shibuda,maana atakuwa anatafuta habari na kuzipeleka CCM,sasa kinachotakiwa kufanya ni kulifukuza hili jitu linaloitwa shibuda.huyu sio mbunge kwa ajili ya wananchi na ni mbunge ambaye si wa CDM.haifai chadema hata siku moja.mfukuzeni huyu Shibude hatufai,ni vema tukalikosa jimbo kuliko kuwa na mbunge wa namna hii.
 
Mawazo ya mtu ndiyo serikali yake.Amewasilisha kile anachokiamini.Uzuri ni kwamba ametupa faida moja ya kumfahamu vizuri zaidi kwamba yeye ni mtu wa namna gani.
 
Kiburi alicho nacho Shibuda kimepitiliza mipaka hadi kufikia kuwashutumu viongozi wake wa CHADEMA kitaifa. Shibuda anajigamba hivyo hata kuhudhuria vikao vya wabunge wa CCM bila kukumbuka uchaguzi wa mwakajana alivyotiwa kapuni na CCM na kisha CHADEMA kumsaidia arudie hali yake ya kawaida. Shibuda akiondolewa CHADEMA uwezekano wa kurudi bungeni tena ni mdogo, bora apumzishwe ajue makali ya wananchi asiowaonea huruma.

Nadhani kwa sasa CHADEMA uvumilivu dhidi ya SHIBUDA umefikia ukingoni, kwani muda aliopewa ilikuwa nafasi kwake ajirudi na badala yake anaziji kujichafua. Kwa sasa Chadema wanapaswa kuchukua uamuzi mgumu tena ili kutuliza nerves ndani ya chama, maana huyu ni pandikizi babu kubwa ndani ya CHADEMA.
 
mi napenda mtu mwny siasa za kweli kama shibuda anasema analoamini si hawa wanaongata na kupuliza.japo siungi mkono wabunge kuongezewa posha

Hata camerun anasema anachoamini,vipi naye unampenda na hizi siasa zake?
 
Shibuda is of unsound mind, cdm has to take a serious action against this baboon otherwise itatugharimu mbele ya safasi, this man is not patriotic, he is financial oriented.
 
I wanna kill right now!??!!!? Life tight kuna mtumishi analipwa 146,000 Kwa mwezi afu ye posho ya laki mbili kwa siku haitoshi na huku bidhaa na huduma tunapata kwa bei moja. Yaani niko tayari kuwa recruited kwa wapambanaji watakaotaka kuingia msituni sanduku la kura halitatuokoa ikiwa wabunge wenyewe ndo hawa na vyama venyewe ndo hivyo Damn it

Yes! Hapa ndipo 45% tu ya watz tunapaswa kupafikia, na itatosha kabisa kuleta mabadiliko tutakapopaza sauti zetu kwa pamoja na kusema 'HAPANAAA'!
 
Back
Top Bottom