SHIBUDA: People's Power ni Kauli Mbiu ya TANU

Umeonaeh!

Shibuda ni lulu kwa CDM. Kamwe hawawezi kukubali kupoteza hichi kifaa cha nguvu...

ukijibishana na taahira wewe ni ........
Ukikimbizana na kichaa na wewe utakuwa ...........

Mwanangu kumbatia elimu kwani ni ..................
Hutakiwi kutumia mabavu kwa mtu kama shibuda kwani mtu mwerevu hutumia akili,elimu,tafakari na hekima katika kuhukumu. Suluhisho la shibuda liko njiani.

UMESAHAU KUWA HATA KUKAA KIMYA NI JIBU?TAFAKARI VIONGOZI WA CHAMA WANAVYOKAA JIBU WAMETOA JIBU GANI JUU YA SHIBUDA
 
Shibuda hajasema kwamba jina hilo liko kwa msajili wa vyama. Alichosema ni origin ya kauli mbiu ya People's Power. Anachofanya ni kuweka rekodi za historia sawa tu.

Ilikuwaje waliolithi TANU wana kauli yao ya MAFISADI'S POWER!
Waludie basi, mbona ni vingi cdm inaongelea vimetoka TANU.
 
Huyu baba ni kilaza kinyama, mbwatukaji asiye na hoja. Kama ilikuwa ni kauli ya TANU ndio iweje? TANU kilikuwa Chama cha Watanganyika wote, NYINYIEM imetelekeza misingi yake yote, si mbaya kwa wazalendo kurejea utu wetu.
 
Aisee video hii ilichukuliwa Mara tu baada ya SHIBUDA kushinda uchaguzi wa Maswa, Huyu ndiye shibuda that time, aliyeipenda CDM na Viongozi wake, anasema Kaulimbiu ya PW ilianzishwa Na waasisi Wa TANU, Na sasa CHADEMA wanaiendeleza Mpaka kieleweke, akimaanisha wananchi wana Nguvu kuliko Vikao vya viongozi, Akito mifano ya Mzee Chief Sarwatt wa Mbulu Na Mzee Slaa wa Karatu..
Nadhani madudu anayoyafanya Leo hii, akiona video yake hii nadhani anaweza hata akalia..
Mgonjwa mmoja wa akili, alipokuwa kwenye harakati za kuokota makopo, kuimbaimba nankufanya fujo, ndugu zake Kwa Bahati wakamwekea mkanda Wake wa video alipokuwa mzima kwenye mahafali yake ya kumaliza kidato cha nne..
Wakashangaa kumwona ametulia tulii akiuangalia mkanda , alivyokuwa akiimba, nasaha, zawadi alizopewa akalia sana mgonjwa yuke, alilia sana kiasi cha kuzimia, baada ya masaa nane faham zilimjia akapata akili tena, akashangaa alivyochafuka Na alivyovaa, akaenda kujisetiri Na tokea that day akawa mzima tena, nadhani Shibuda atendewe Kama mgonjwa mwenzake huyo, anaweza kupona..
 
Nanyie mmezidi kumtafsiri vibaya huyu kibudu, mbona hapa anaongea kama mtoto asiyejua baya na zuri? Tusimuhukumu kwakila jambo jamani tumsaidie na yeye ni mume wa mtu na ni baba wa watoto khaaaa
 
Huyo ndio mgombea urais! Ni bora akagombea huko huko anakojua! Make sioni kama anaweza kupata hata kura 50,000 Tanzania nzima!

Kura hizo umempa nyingi... hata za jimbo lake hazipati zote. Huyo mzee ameishiwa sera. Asubiri tu kuondolewa kwenye orodha ya wagombea wa CDM 2015.
 
Kwani nani kabisha...??? Hata hivyo hakuna historia yoyote inayoonyesha kuwa hiyo ilikua kauli mbiu ya TANU, ukisoma vitabu vingi vinaonyesha kuwa kauli mbiu zilizowah kutumiwa na TANU ni pamoja na “Uhuru na Kazi”, "Socialism and Rural Development", “Umoja ni Nguvu Utengano ni Udhaifu”, 'Uhuru na Umojaa'.... Kwa hiyo, hizo ni propaganda tu za SHIBUDA!!
 
Aisee video hii ilichukuliwa Mara tu baada ya SHIBUDA kushinda uchaguzi wa Maswa, Huyu ndiye shibuda that time, aliyeipenda CDM na Viongozi wake, anasema Kaulimbiu ya PW ilianzishwa Na waasisi Wa TANU, Na sasa CHADEMA wanaiendeleza Mpaka kieleweke, akimaanisha wananchi wana Nguvu kuliko Vikao vya viongozi, Akito mifano ya Mzee Chief Sarwatt wa Mbulu Na Mzee Slaa wa Karatu..
Nadhani madudu anayoyafanya Leo hii, akiona video yake hii nadhani anaweza hata akalia..
Mgonjwa mmoja wa akili, alipokuwa kwenye harakati za kuokota makopo, kuimbaimba nankufanya fujo, ndugu zake Kwa Bahati wakamwekea mkanda Wake wa video alipokuwa mzima kwenye mahafali yake ya kumaliza kidato cha nne..
Wakashangaa kumwona ametulia tulii akiuangalia mkanda , alivyokuwa akiimba, nasaha, zawadi alizopewa akalia sana mgonjwa yuke, alilia sana kiasi cha kuzimia, baada ya masaa nane faham zilimjia akapata akili tena, akashangaa alivyochafuka Na alivyovaa, akaenda kujisetiri Na tokea that day akawa mzima tena, nadhani Shibuda atendewe Kama mgonjwa mwenzake huyo, anaweza kupona..

Hii therapy nzuri sana. Tujaribu hii, ninaamini itasaidia...
 
Shibuda kweli kiboko....kana ametumwa basi kazi yake anaitendea haki. Nakumbuka alivyokuwa anajibizana na JK that time, na maandiko mengi.. Nikampendaje....nikajua ni shujaa mara nikamwona anamuunga mkono JK dom akichukua fomu, nikashangaa.
 
Kwa jinsi ninavyomjua shibuda alivyo connected na watu wa maswa hata akisimama kwa tiketi ya tpp maendeleo atashinda tu,si mliona
alivyoibwaga ccm licha ya fitna za makamba na kutupwa ndani kwa kesi ya kutungwa ya mauaji?kule
hawachagui chama wanachagua mtu wao

Hakuna marefu yasiyo na ncha....hata Gadafi alichokwa na wema wote aliowatendea wananchi wake.
 
Wanachagua chama acha kumdanganya.....fuatilia maswa yote mpaka meatu,upepo umevuma vipi?
Kwanza walikuwa wamemchoka ila CCM walikuwa wameichoka zaidi....."Ya maswa,tuachie wana maswa"

Wengi hawawajui watu wa Maswa na wala hawajawahi kutembelea vijiji vya Maswa, tusubiri 2015
 
Shibuda hajasema kwamba jina hilo liko kwa msajili wa vyama. Alichosema ni origin ya kauli mbiu ya People's Power. Anachofanya ni kuweka rekodi za historia sawa tu.

Hata wewe records zako hizo ni questionable! Tanu ilianzishwa 1954 wakati Ghana ya Osagyefo Dr. Kwame Nkrumah ilikuwa imebakiza miaka 3 tu kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa kiingereza, je una uhakika kauli mbiu hiyo hawakuitumia huko? je Tanu ndio mwanzilishi wake au waliiga pia? je wana hakimiliki yake ili wapigania ukombozi wengine wasiitumie? in what context did Shibu make that statement?? weka records straight!!
 
sijui huyu mswahili wa siasa mnatakia nini kwani amejaa sifa asizostahili na hana adabu kwa viongozi wake
 
Back
Top Bottom