Shibuda out

wanaJF

kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) iliyokutana tarehe 30/4/2011 imeamua kumtoa shibuda kwenye nafasi ya kukaimu nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa shinyanga, lakini kwnye kikao hicho nusura zichapwe kati ya lema na zitto baada ya lema, kumjia juu zitto ya kuwa mambo yote hayo ya shibuda kayasababisha yeye pale shinyanga kwa kuwaambia baraza la uongozi la mkoa kumteua shibuda kuwa kaimu mwenyekiti wakati katiba ya chama inasema kaimu mwenyekiti anapaswa kutokana na baraza la uongozi la mkoa,

huku shibuda akiwa si mjumbe wa baraza hilo, ndipo aliposimama zitto na kupinga kauli hizo ndipo wabunge na wajumbe wa kamati kuu walipo kuja juu na kumkumbusha zitto juu ya shibuda ya kuwa aliwatukana wabunge na akaambiwa aombe radhi akakataa na mpaka sasa hajaomba kwanini zitto unamtetea huyu jamaa, aliuza mjumbe huyo ambaye ni swahiba wa zitto bwana Msafiri mtemelwa

Wakae wasuluhshe na kuweka maslah ya taifa mbele cio kuonyeshana nani anamisuli.
 
Nchi hii hakuna chama bali mikusanyiko ya wasaka tonge tu!! Haya jioneeni. CCM wanaparurana na kuvuana magamba huku CHADEMA wanataka kupigana. Mimi ni mshabiki wa LEMA kama LEMA ila si Chama lakini sasa naanza kujiuliza juu ya ukomavu wake kisiasa manane kauli zake zimekuwa za ngumi mbele!!

Niliwahi kusema kuna siku mtakuja tafuta refenrece JF.Jiulize Lema ana cheo gani kitaifa ?.Zitto ni naibu katibu mkuu sauti yake ni sauti ya CHADEMA kitaifa Lema ni mbunge wa Arusha tu naomba kujuzwa na kusahihishwa kama ana wadhifa mwingine zaidiya ubunge?. Lema kaikuta CHADEMA imara baada ya kazi nzuri na kubwa iliyofanywa na Zitto na Dr Slaa.

Hakika kama wangekuwa wanapinga kwa hoja ni vema na haki ila kwa kutaka kupigana!! Mimi binafsi naogopa naona kuna bundi ameeingila CHADEMA na mwisho wake yasije yakawa yale ya NCCR-Mageuzi kule Tanga ambapo watu walitokea madirishani na wengine kujichimbia chini ya meza. CHADEMA kuweni makini msije mkawa historia. Hizo chokochoko si dalili njema hata kidogo

Mkuu tusije kuwasingizia CCM siku mambo yakienda kombo !.

Sasa wewe kipimo cha kujua kuwa huu ni ukweli au ni uongo ni upi? Si unaelezwa kinachoendelea? We brain yako ikoje. Aliyekuwa ndani ya kamati kaeleza kilichotokea we unasema sio kweli. Aya tuambie wewe ukweli ni upi?

Mkuu umesahau chama chetu hakifanyi makosa.
 
zitto kakataa kutumiwa na wakanda wa kaskazini. hawamsahau kwa hilo wamejaribu kumfanya wangwe wameshindwa.

kaka zitto jihadhari hilo kundi lina wauaji na huyo lema ni jambazi.
 
zitto kakataa kutumiwa na wakanda wa kaskazini. hawamsahau kwa hilo wamejaribu kumfanya wangwe wameshindwa.

kaka zitto jihadhari hilo kundi lina wauaji na huyo lema ni jambazi.
tumia kichwa na sio mat@ko kufikiri
 
LEMA ANAITAJI MAFUNZO YA UONGOZI NA UHUSIANO KWA JAMII, hakuna mtu anayetaka TYSON kuongozi nchi hii hayo mambo tuliwahachia ccm , huko ndiko kuna komandoo, tyson , tingatinga na majina yenye kero kama hayo
mimi namkubali sana mkuu LEMA ila sasa kazidi kidogo, hii sio somalia



Taari iwe ya kweli au la... Hivi haiwezekani kweli kumsaidia Lema afahamu kwamba siyo kila kitu ni munkari na fights?

Niliwahi kusema kuna siku mtakuja tafuta refenrece JF.Jiulize Lema ana cheo gani kitaifa ?.Zitto ni naibu katibu mkuu sauti yake ni sauti ya CHADEMA kitaifa Lema ni mbunge wa Arusha tu naomba kujuzwa na kusahihishwa kama ana wadhifa mwingine zaidiya ubunge?. Lema kaikuta CHADEMA imara baada ya kazi nzuri na kubwa iliyofanywa na Zitto na Dr Slaa.



Mkuu tusije kuwasingizia CCM siku mambo yakienda kombo !.



Mkuu umesahau chama chetu hakifanyi makosa.

Wakae wasuluhshe na kuweka maslah ya taifa mbele cio kuonyeshana nani anamisuli.
 
Zitto anatakiwa amshukuru lema kwa kumweleza wazi tena kwenye kikao halali cha chama. Kuna watu kadhaa kwenye hiyo kamati wanamchukia zitto lakini wanamchekea kisha wanamshambulia kupitia JF kwa majina bandia.

Better an enemy who attacks you than a friend who flatters you. Kumbukeni alivyotoswa Bagamoyo na rafiki zake hadi akalazwa agha khan.

Lakini zitto amekua sasa, aache siasa za kuchakachua kanuni ili kupitisha maswahiba kwa ajili ya kujiimarisha ndani ya taasisi. Aache mambo aliyoyafanya DARUSO, amekua sasa.
 
<br />
<br />


Wewe ni Mkuki Moyoni au Mkuki Makalioni kwa hiyo unakusumbua unashindwa kukaa chini na kufikiri!!
Unawezaje kumfananisha Shibuda na Mbowe,on what grounds? Na kuhusu Slaa,huyo mwanamke aliyemchukua Slaa ni wa kwako? Au mkuki umepita kwenye hako kashimo katikati ya makalio yako kwa hiyo unakutekenya?
Kama mwanamke anakutambua wewe ni Mume wake kwa nn aende kwa mwanaume mwingine? Stop writing bulshit!! Just for ur information,Dr.Slaa is expecting a baby from Josephine in the next couple of dayz!!
Na wewe ukikaa legelege watu si tu watakuchukulia mkeo bali watakuja hata kulala naye kwenye hikohiko kitanda chako!
It is ur duty to protect ur wife,Kwanza mwanaume lijali hawezi kulalamika hadharani akichukuliwa Mke,ni Aibu na Matusi!!
Dr.Slaa is a great man and an African Legend!!

Tumaini Jipya najua umejibu kitarabu Mkuki Moyoni kama alikuja. Lakini nakuomba tuende taratibu mkuu naona umenda mbali sana ingawaje Mkuki Moyoni naye
 
HEKO WAHESHIMIWA ZITTO NA LEMA KWA UKOMAVU WENU KIDEMOKRASIA:
HATA SIKU MOJA WALA MSIOGOPE KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA KATIKA HOJA BILA CHUKI WALA MIZENGWE

Waheshimiwa Zitto, Lema na kamati kuu zima, napenda niwapongeze tena saaana kwa jinsi mnavyohakikisha kwamba NEMBO YETU YA 'DEMOKRASIA' kweli inafanya kazi kiukweli ndani ya chama katika vyombo vyetu vyote vya maamuzi.

Huo ndio ukomavu wa kidemokrasia, uwazi wa kuendesha mambo kuonyesha utayari wa CDM kuongoza taifa bila kwepo TABAKA LA WATEULE ndani ya chama ambao kauli zao hazipingwi. Nawapongeza pia kukataa kubariki maamuzi ya barabarani katika kuteuana ukaimu mwenyekiti huko Shinyanga. Mhe Shibuda sasa ajindae tu kuingia kwenye kinyang'anyiro katika kukijenga chama huku kwa ushirikiano zaidi.

Ndio demokrasia ndani ya vyama inapokomaa na baada ya hapo wote wawili kuendelea kusalimiana na kuendeleza harakati za kufanya kazi kwa pamoja zaidi kutetea maslahi ya umma wa Tanzania.

Nasema ni ndani ya CHADEMA tu ndimo kulimo kiwango hicho cha juu cha demokrasia na misingi ya maadili ya vipi kushika uongozi KWA KUZINGATIA ITIKADI YETU YA 'NGUVU NA MAMLAKA YA UMMA' katika kila tulitendalo na maamuzi tunayoingia.

Mwisho, chama bila mikiki mikiki ya ndani lakini kwa misingi ya disciplined democratic space exercising tayari ni marehemu mtarajiwa kama kilivyo CCM ambako tofauti tu ya maoni kesho yake mtu anakolimbwa kwa kile anachokiamini.




Cdm hawakufanya home work yao wakati wa uchaguzi so. kwakuwa hawakuwa na dola walipaswa kutafuta wagombea safi lakini badala yake walisubiri hadi kura za maoni za ccm zimalizike ili wsachukue makapi na shibuda ni matokea ya cdm kushindwa kujiaandaa kwa uchaguzi uliopita. nawasilisha lakini nawapa salamu zanngu great thinkers
 
zitto kakataa kutumiwa na wakanda wa kaskazini. hawamsahau kwa hilo wamejaribu kumfanya wangwe wameshindwa.

kaka zitto jihadhari hilo kundi lina wauaji na huyo lema ni jambazi.
The more i read this post the more i think Jenifa anaumwa
 
zitto kakataa kutumiwa na wakanda wa kaskazini. hawamsahau kwa hilo wamejaribu kumfanya wangwe wameshindwa.

kaka zitto jihadhari hilo kundi lina wauaji na huyo lema ni jambazi.

Jina zuri la kike lakini akili za kishetani. Kasome globalpublishertz wanaofikiria kama wewe, hapa hupawezi.
 
Nashangaa leo Shibuda anaonekana hafai wakati ametoa mchango mkubwa kuifikisha Chadema hapo ilipo mkoani Shinyanga. Wale wanaotilia shaka uaminifu wa Shibuda kwa Chadema ni wanafiki wasiopenda kuambiwa ukweli kwenye vikao, tusishangae yakaendelea hadi kufukuzana kama yale ya Marehemu Chacha Wangwe.
 
Taarifa iwe ya kweli au la... Hivi haiwezekani kweli kumsaidia Lema afahamu kwamba siyo kila kitu ni munkari na fights?

Wakati mwingine hii kufuata protocol inapoteza muda nguvu lazima itumike...wewe unafikiri bila nguvu TUNISIA, MISRI ingekuwa huru?? hao hao wanaoamini juu ya demokrasia mbona wapo LIBYA wanapigana???? LEMA USIFE MOYO MTU AKIJA MBELE KINAFIKI MPE NGUMI mwishowe wataelewa nini unataka. Hatutaki unafiki hapa.
 
Niliwahi kusema kuna siku mtakuja tafuta refenrece JF.Jiulize Lema ana cheo gani kitaifa ?.Zitto ni naibu katibu mkuu sauti yake ni sauti ya CHADEMA kitaifa Lema ni mbunge wa Arusha tu naomba kujuzwa na kusahihishwa kama ana wadhifa mwingine zaidiya ubunge?. Lema kaikuta CHADEMA imara baada ya kazi nzuri na kubwa iliyofanywa na Zitto na Dr Slaa.
Mkuu Ngongo

Chadema ni Chadema kamwe haitokuja kufanana na CCM, mambo ya nani alikuwa mwanzilishi au ni mwanachama wa lini ndiyo yanayoimaliza CCM kwa kulazimisha kina January, Nape, Vita kuwa viongozi hata kama hawana uwezo kwa vile tu wazazi wao walikuwa waanzilishi. Kusema Lema kaikuta CDM hakuna maana yeyote katika uwajibikaji ma CEO wanaajiriwa si kwa kigezo cha nani katangulia kwenye kampuni, sisi wanachama wa CDM tunaangalia nani anakisaidia chama leo kisonge mbele na si nani alikuwa mwanachama mwaka 1995.

Kwa nini wengi leo wanamuongelea Lema zaidi na si waanzilishi wengine, ni kwa sababu matendo yake yanaonekana, mfano tumefanya mikutano kanda ya Ziwa takribani miezi miwili wengine(baadhi) hawajaonekana wanakuja kuonekana siku ya msiba na kuzusha controversial zisizo na msingi, kwa hilo tu linaweza kuleta walakini kwa wapenzi na mashabiki wa chama.

Kuhusu cheo kuwa Zitto ni Naibu Katibu na Lema hana cheo hiyo ni by default na si kitu cha kudumu kinaweza kubadilika wakati wowote, sidhani leo Katibu Mkuu wa CDM Slaa akiulizwa achague mtu wa kumsaidia kati ya Zitto na Lema kama atarudia makosa ya zamani, kumbuka hata kule Bagamoyo wabunge walimpigia Zitto kura ya kutokuwa na imani naye akaokolewa na kamati kuu.
 
MKUU UNAONGEA UPUPU, HAYO UNAYOYAONA KWENYE TV HUKO LIBYA SIO HALI TULIYONAYO KWA SASA KUMBUKA HIVI NI VITA NDANI YA CHAMA, KWA HIYO UNATAKA CHAMA KIFE AU WEWE NI chadema kwa umaarufu wa mtu
Wakati mwingine hii kufuata protocol inapoteza muda nguvu lazima itumike...wewe unafikiri bila nguvu TUNISIA, MISRI ingekuwa huru?? hao hao wanaoamini juu ya demokrasia mbona wapo LIBYA wanapigana???? LEMA USIFE MOYO MTU AKIJA MBELE KINAFIKI MPE NGUMI mwishowe wataelewa nini unataka. Hatutaki unafiki hapa.
 
nadhani issue siyo kwamba shibuda hafai, anafaa sana, ila si kwa cheo hicho cha mkoa... the guy is unrealiable
 
Kama jambo hili ni la kweli mimi sipingi watu kutofautiana mawazo.Hatuwezi kuwa na mawazo uniform.ukitaka watu wawe na mawazo yanayofanana wakati wote umetaka watu hao wasifikiri.
Jambo la msingi ni viongozi hawa kuondoa jazba wanapotofautiana na kuhakikisha kanuni zinafuatwa ili kuepuka migongano isiyo na tija kwa chama.
Binafsi simuamini SHIBUDA hata tone ila utaratibu wa kumpinga au kumtetea usije ukatufikisha kwenye ile NCCR ya MREMA.
 
Kwanza, nipo reluctant kuchangia kwasababu sijaelewa sana inapozungumzwa "nusura zichapwe kati ya lema na zitto". Je walikuwa karibu,mmoja akawa anaelekea kum-chapa mwenzie (physical confrotation), au ulikua ni mnyukano mkali wa hoja? The later,to me, is just a plus,kwa hao vijana kwani wanatutoa ule utando wa zidumu fikra za fulani halafu masengenyo nje ya vikao. The former, obviously is a shame na wazee lazima walifanyie kazi hilo UPESI! Ufafanuzi zaidi hapa toka kwa insiders please!
Kwenye red,
Mukuu nakuheshimu sana,lakini wakati mwingine unapoandika maneno kama haya bila kusubstanciate,kwa member mwenye reputation kubwa kama yako,unajikosea heshima mwenyewe! Pengine mistari mitatu tu ingetosha kueleza ni kwa vipi na kwa nini unadhani Zitto "haelewani kifikra na Slaa na Mbowe". Na kuhusu vision ya Zitto kuwa 20 years ahead eti ndio iwe sababu ya tofauti hizo,pia umejikosea heshima mwenyewe tena mkuu. Kwa kuwa napenda kujiheshimu nitajaribu kuweka hoja:

  1. Hata angekua na vision ya 2070,naamini Mh. Zitto anaelewe kuwa hapaswi kujimilikisha agenda yake binafsi kama mganga wa kienyeji,na badala yake atumie busara zake kuifanya kuwa agenda ya chama. Hizi sio zama za one-man-show na CDM ni kubwa kuliko Zitto!
  2. Mh. Zitto ni muhimu akahekimika beyond fikra za "maamuma" kwamba anaweza kutengwa au kuchukiwa katika chama eti kwasababu ya ukanda, au udini au udugu au chochote cha kipumbavu kifananacho na hayo! Badala yake ajihoji,(kama ni kweli anahisi kutotendewa haki) ni vipi amefika hapo pamoja na mengi ambayo amekifanyia chama. Je ni zile habari za mawasiliano na Rostam ana UWT? Je ni kuongezeka kusikoelezeka kwa mali zake? Hizi zote ni tuhuma tu sio?Au ni kule tu kugoma kumgomea rais bungeni? Na kwa kuwa anaipenda CDM kuliko mimi,basi atafute suluhu ya haya au yeyote mengine,ili chama kipone na yeye pia. Akitaka kuwa shozniga kwa kupambana na wote ili aibuke hero mwishoni mwa picha, katikati ya mizoga ya CDM na uongozi wake, atakua amemtumikia nani?
  3. Kuanguka kwa Zitto au Lema, au wote wawili kwenye siasa (na haki ya kweli kwa mwendo huu anguko li karibu) halitakua tu pigo kwao,bali kwa vijana wote wa kitanzania ambao walianza kupata tumaini la ukombozi kupitia wao.
Kuhusu kutolewa kwa Shibuda, nadhani ni right and very thoughtful move ya CDM though it never goes without PAINS. Which means, it should also never go with one genuine question unanswered.....How was he elected/appointed in the first place?
Alitumia uhuru wa kutoa mawazo yake hivyo si vema kulaamu, mbona ya CCM huwa inaandikwa kwa utaratibu kama huu na kujadiliwa tena kwa kicheko.
Kikubwa ninahokiona ni kwamba ndani ya Chadema kuna watu wanajiona wao ndiyo wao na baadhi ya wengine kila wakisemaau kufanya kitu wanaonekana kama wasaliti / wamekosea kama ambavyo comrade Zitto anavyoandamwa na hasa kwa kuwa kwa kiasi fulani haelewani na Slaa na Mbowe kifikra, maana Zitto ana vision kubwa hivyo anaangalia na kuchambua mambo kwa mtazamo wa hali ya juu na kuona miaka kumi mpaka ishirini ijayo.
 
TAARIFA HII SIO YAKWELI, IPO KICHONGANISHI, haya mambo sio rasmi, tuweni makini. Jf itakuwa sasa kibanda cha kahawa!

Nashukuru sana ndg kwa kuliona hili. Mi nimekuwa nikisoma post 1 baada ya nyingine, tena nyinine kutoka kwa watu wanaojulikana kutoa hoja za msingi hapa jf. Nimeshangazwa na watu kurukia na kujadili kwa hisia kabisa taarifa hii isiyo na kichwa wala miguu.
 
Wanajamii Forums, kweli John Shibuda kadiri ya msimamo wake alioonyesha tangu awe mbunge wa Chadema hamuoni kama Kaingia Chadema kwa ajili ya ubunge na wala si kwa mapenzi ya chama. Yeye hata alivyojieleza bungeni bado ni mpenzi wa CCM.

Zito Kabwe naye ni ndumila kuwili na kila inapotokea jukumu la viongozi wa Chadema kwenye mikutano au maandamano haishiwi visingizio, lakini kwenye kamati za bunge anakolipwa posho matatizo yote ya kifamilia huisha.

Shibuda si muafaka kwa sasa kuwa mwenyekiti wa mkoa, anahitaji kubaki chini ya uangalizi maalum kwa manufaa ya Chadema na wananchi.

Safi sana mkuu maelezo yako yamekaa vizuri,tunashukuru.
 
Nimekuwa nikifatilia hii issue ilivyo letwa hapa jamvini lakini kadri inavyoendelea nazidi kuwa na mashaka kama alivyo changia mshindo hapo hasa maelezo ya awali.....
inawezekana Lema na Zitto wametofautiana kweli na sio kitu cha ajabu kwani hata kwenye familia zetu vitu kama hivi vipo sana tu....
lakini nina wasiwasi na mleta mada alivyoileta maana ameileta kiuchonganishi na mimejaribu kupitia thread zake zote alizo wahi kuanzisha ni za lema, hii inaonyesha yuko karibu sana na lema na mabadiko mengi yanaonyesha anamchukia sana Zitto:

1. Shibuda out

2. Lema awasha moto tena chuo cha uhasibu

3. state house yapanga kumuangamiza lema

4. Lema awasha moto Igunga

5. Lema afunika Nzega

6. Meya feki wa arusha aomba ulinzi wa polisi nyumbani kwake.

7. Meya feki wa arusha aomba ulinzi wa polisi nyumbani kwake.

8. Godbless Lema kuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA
 
Back
Top Bottom