JACADUOGO2.
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 930
- 217
Tatizo hapa ni Zitto na Lema au ni Shibuda? Na waliomteua Shibuda kukaimu nafasi hiyo hawakujua sheria kuhusu taratibu na kanuni za Chama?
CDM mwaongoza kwa siasa za majitaka, nyie ni shari tu! mara mnataka kupigana. Hiki chama hakina future.
mkuu ni kweli kabisa aliyenena hapo juu yupo sahihi, leo nusura lema na zitto zipigwe pale lema alipo mwambia zitto ukweli kuwa aache kutumiwa na hata kaa afanikiwe kwenye mipango yake hiyo na kuwaacha wajumbe wote midomo wazi kila mmoja akishangaa kijana lema asivyo mumunya maneno na kuamua kumtolea uvivu zitto
Atakufa yeye badala ya Chadema.Kwa kweli Huyu Zitto haeleweki, kila controversial ya CDM lazima ahusike. Isije ikawa amepandikizwa kuiua CDM.
Mkuu ungetoa hoja na si kumtukana mwenzio Mkuki Moyoni!! Hujaonyesha ukomavu wa kupingana kwa hoja. Tukiendelea hivi kuna siku tutataka milango ifungwe ili tupigane humu ndani ya jamvi!!
TAARIFA HII SIO YAKWELI, IPO KICHONGANISHI, haya mambo sio rasmi, tuweni makini. Jf itakuwa sasa kibanda cha kahawa!
Najaribu kujiuliza pale mwana CCM anapomtetea Shibuda sipati jibu, lakini for your information unaowaandikia hapa JF wanaweza kuwa na IQ kubwa pengine kuzidi yako.Jamani nashindwa kuelewa,jamaa kama kasema ukweli ndio ulivyo,je, kwa nn unampangia maneno ya kuonge,eti asiongee ya ndani yaliyotokea.na mbona hilo la shibuda out umelipokea...je sio la ndani? halafu huyu dogo huyu Lema anamwambia zitto katumwa...hahaaa ni shida kweli kweli na huyu asipokaa sawa mwisho wa siasa zake za upepo uko karibu sana, au na yeye anatumwa na Mbowe? huu ni ulimbukeni tu unamsumbua lema .....na kama watu hawana nidhamu wataambiwa tu,kisa cha zito kumtetea shibda ni haki yake ya upenzi na uwezo wake wa kuona mbali,je mbowe anahofia shibudaa kumng'oa cheo na kukirudisha chama kanda ya ziwa?tusubiri tutaona mengi...mmejaribu kumchafua shibuda magazetini na jf lakini jueni shibua anaheshimika na kukubarika kuliko huyo slaa na mbowe..kwanza hawawezi kuwa marais wa nchi hii,mfanyabiashara na mwizi wa wake za watu....lema umechemka dogo...bado unasafari ndeeefu sanaaa.
Alitumia uhuru wa kutoa mawazo yake hivyo si vema kulaamu, mbona ya CCM huwa inaandikwa kwa utaratibu kama huu na kujadiliwa tena kwa kicheko.
Kikubwa ninahokiona ni kwamba ndani ya Chadema kuna watu wanajiona wao ndiyo wao na baadhi ya wengine kila wakisemaau kufanya kitu wanaonekana kama wasaliti / wamekosea kama ambavyo comrade Zitto anavyoandamwa na hasa kwa kuwa kwa kiasi fulani haelewani na Slaa na Mbowe kifikra, maana Zitto ana vision kubwa hivyo anaangalia na kuchambua mambo kwa mtazamo wa hali ya juu na kuona miaka kumi mpaka ishirini ijayo.
unapokataa jina lako kwe Jf unataka 2kuelewe vipi wewe dogo?
TAARIFA HII SIO YAKWELI, IPO KICHONGANISHI, haya mambo sio rasmi, tuweni makini. Jf itakuwa sasa kibanda cha kahawa!
wanaJF
kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) iliyokutana tarehe 30/4/2011 imeamua kumtoa shibuda kwenye nafasi ya kukaimu nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa shinyanga, lakini kwnye kikao hicho nusura zichapwe kati ya lema na zitto baada ya lema, kumjia juu zitto ya kuwa mambo yote hayo ya shibuda kayasababisha yeye pale shinyanga kwa kuwaambia baraza la uongozi la mkoa kumteua shibuda kuwa kaimu mwenyekiti wakati katiba ya chama inasema kaimu mwenyekiti anapaswa kutokana na baraza la uongozi la mkoa,
huku shibuda akiwa si mjumbe wa baraza hilo, ndipo aliposimama zitto na kupinga kauli hizo ndipo wabunge na wajumbe wa kamati kuu walipo kuja juu na kumkumbusha zitto juu ya shibuda ya kuwa aliwatukana wabunge na akaambiwa aombe radhi akakataa na mpaka sasa hajaomba kwanini zitto unamtetea huyu jamaa, aliuza mjumbe huyo ambaye ni swahiba wa zitto bwana Msafiri mtemelwa
ili balaa gani kati ya zito na lema,
duh mbona mapema au mkuu umechakachua hii kitu,
kuna haja ya kuwa makini na kutumia busara, kama haya yanatokea
chama kiko hatarini na hekima ya wazee inatakiwa kukinusuru chama,
na kanuni za chama zinatakiwa kufuatwa, ili zinapokosewa kuna haja ya kuongea kwa kuheshimiana
ila hii habari yako ninaifanyia uchunguzi kama ina ukweli,
HEKO WAHESHIMIWA ZITTO NA LEMA KWA UKOMAVU WENU KIDEMOKRASIA:
HATA SIKU MOJA WALA MSIOGOPE KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA KATIKA HOJA BILA CHUKI WALA MIZENGWE
Waheshimiwa Zitto, Lema na kamati kuu zima, napenda niwapongeze tena saaana kwa jinsi mnavyohakikisha kwamba NEMBO YETU YA 'DEMOKRASIA' kweli inafanya kazi kiukweli ndani ya chama katika vyombo vyetu vyote vya maamuzi.
Huo ndio ukomavu wa kidemokrasia, uwazi wa kuendesha mambo kuonyesha utayari wa CDM kuongoza taifa bila kwepo TABAKA LA WATEULE ndani ya chama ambao kauli zao hazipingwi. Nawapongeza pia kukataa kubariki maamuzi ya barabarani katika kuteuana ukaimu mwenyekiti huko Shinyanga. Mhe Shibuda sasa ajindae tu kuingia kwenye kinyang'anyiro katika kukijenga chama huku kwa ushirikiano zaidi.
Ndio demokrasia ndani ya vyama inapokomaa na baada ya hapo wote wawili kuendelea kusalimiana na kuendeleza harakati za kufanya kazi kwa pamoja zaidi kutetea maslahi ya umma wa Tanzania.
Nasema ni ndani ya CHADEMA tu ndimo kulimo kiwango hicho cha juu cha demokrasia na misingi ya maadili ya vipi kushika uongozi KWA KUZINGATIA ITIKADI YETU YA 'NGUVU NA MAMLAKA YA UMMA' katika kila tulitendalo na maamuzi tunayoingia.
Mwisho, chama bila mikiki mikiki ya ndani lakini kwa misingi ya disciplined democratic space exercising tayari ni marehemu mtarajiwa kama kilivyo CCM ambako tofauti tu ya maoni kesho yake mtu anakolimbwa kwa kile anachokiamini.
Si kwamba Zitto moyo wake hauko CDM hapana ila ana asili ya kujiona yeye na mawazo yake ni bora zaidi kuliko ya wengine, naelewa si vibaya kutofautiana kimawazo lakini kama wewe ni kiongozi wa chama cha watu consensus ikifikiwa (majority) ni busara kukubaliana na kuheshimu maamuzi ya wengi, yeye hilo hana atalazimisha wazo lake hata kwa ku-lobby watu wengine alimradi afanikishe anachokitaka hata kama anaona wazi litaharibu image ya chama au mahusiano yake na wengine kwa kisingizio cha free opinion. Matokeo yake anaonekana mbinafsi na asiyejali matokeo yeyote kwa chama.Haya mambo yanayo ongelewa yawe ya ukweli au uongo ukweli utabaki palepale kwamba"ZITTO ANAIIMBA CHADEMA LAKINI MOYO WAKE UPO MBALI NA CHADEMA".nasema hivyo kwa sababu hakuna mgogoro wowote ninaoukumbuka ambao ulitokea cdm zitto asihusishwe.kila baya chadema zitto yupo.na hii hali itaendelea hivi hadi atakapojiengua mwenyewe CDM.zitto hana msaada wowote chadema zaidi ya kuleta migogoro.kadili siku zinavyoenda umaalufu wa cdm unapungua kigoma.je ni kwanini?
Alitumia uhuru wa kutoa mawazo yake hivyo si vema kulaamu, mbona ya CCM huwa inaandikwa kwa utaratibu kama huu na kujadiliwa tena kwa kicheko.
Kikubwa ninahokiona ni kwamba ndani ya Chadema kuna watu wanajiona wao ndiyo wao na baadhi ya wengine kila wakisemaau kufanya kitu wanaonekana kama wasaliti / wamekosea kama ambavyo comrade Zitto anavyoandamwa na hasa kwa kuwa kwa kiasi fulani haelewani na Slaa na Mbowe kifikra, maana Zitto ana vision kubwa hivyo anaangalia na kuchambua mambo kwa mtazamo wa hali ya juu na kuona miaka kumi mpaka ishirini ijayo.