Shibuda out

Nilikuwepo kwenye kikao mwanzo hadi mwisho. Mengi yanayoandikiwa hapa ni hisia zinazotokana na mazoea. Tatizo ni kwamba tumezoea siasa za ndiyo mzee, kitu ambacho hakipo CHADEMA. Ndani ya vikao vya CHADEMA tunajadiliana sana, mvutano ni mkubwa, tena wakati mwingine kwa ukali hadi mwafaka unapopatikana. Na mwafaka hupatikana kwa kuzingatia uzito wa hoja na ushahidi wa kutosha. Kwa sababu ya mazoea ya siasa za ki-CCM za funika kombe mwanaharamu apite, watu wakiona CHADEMA wakivutana kihoja wanatafsiri kwamba ni mgogoro au tatizo.

Ukweli ni kwamba kwenye kikao kulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo mbalimbali. Mwisho wa siku tumefikia mwafaka na maamuzi yamefanyika kidemokrasia na amani ni tele.

Kuhusu Shinyanga, ni kwamba ukaimishaji haukufuata taratibu na kanuni za Kikatiba. Viongozi wetu wa Shinyanga walikiri kosa lao na wamekubaliana na maamuzi ya kutengua uteuzi huo hadi hapo taratibu zitakapofuatwa. Tofauti ni hio tu, kwamba CHADEMA huchukua hatua madhubuti na mapema, badala ya kufunika kombe mwanaharamu apite.

Hivyo, ndugu zangu wapenzi wa mabadiliko katika nchi hii msinyong'onyee, there is total peace in CHADEMA and the struggle continues.
Kitila hatuna imani na wewe kabisa!!!!!!!!
Wewe umekuwa ukitumiwa na kambi ya "NORTH ONLY" kuhalalisha udikiteta ndani ya Chadema. Kumbuka wewe ndiye uliyekuja na vigezo tata vilivyopelekea kuchaguliwa kwenye viti maalumu watu familia au kanda moja.
Nadhani na wewe upo kwenye payroll ya wale mabepari wawili!
 
Kwa hili naungana na wewe toka lini CCM mkawa na imani na uongozi wa Chadema, ungesema una imani naye ningekupinga.
 
wala hatukuhitaji upofu huu wa mawazo,wewe unamwona Zitto haeleweki na wenzake kwa sababu tu eti ana vision ya miaka10 mbele,yawezekana ila anatakiwa awe bayana ili vision yake ieleweke ama la hatuitaji vision private ya mtu mmoja tunahitaji vision moja ya chama kimoja inayoeleweka

alafu kabla haujaandika hebu tumia akili yako ndogo kujihoji,ni nani alikwambia kweli Dr.na Mbowe hawamtaki Zitto?ulitegemea ni nani atamwamini katika baadhi ya matendo yake yanayofahamika bayana?

Acha utoto,hata angelikuwa ni ndugu yako wa kuzaliwa hauwezi kumwamini tena kama mwanzo mpaka pale atakapo omba msamaha na kubadilika,na labda tu unadhani ni kwa nini mara hii Zitto alikabiliwa na upinzani pale jimboni kwake tofauti na ilivyokuwa awali,go and have a research,NYAMBAFUUUUUUUUUUUUUUU

ni kwel walikuwa wagombea kumi. Source mchakato majimbon tbc 1.
 
Kupingana kwa Hoja ndiyo,ndiyo tofauti iliyopo kati yaCHADEMA na CCM

kuna post yang niliiweka mpema jana, kuhusu misimamo wanajf wawe waelewa bac kuhusu cdm, inaongozwa kwa katiba na kanuni zake, hivyo suala la shibuda halina maana, mimi jana nimeongea nae na kutumia makada wa ccm lakin bado nia yake ipo pale pale na kasema atagombea nafasi hiyo kwani kwa sasa ana kaimu na hajapewa barua ya kuzuiwa kuendelea na kazi. Na akasema hawez kuzuia watu wasiseme ila cdm shy wanaiman naye sana kuibomoa ccm na hana mapenzi tena na ccm.
 
Yaani wewe umejiunga JF wiki tatu zilizopita mara tayari umeshaiona forum hii ni kijiwe na unategemea mtu yeyote mwenye akili asikuone kwamba hasa ndio umejiunga humu kuishushia hadhi JF?????

Ama kweli ishi uyaone maajabu ya dunia!!!!!!!!!!!!!!

Mbona sku nyingi sana JF imekuwa kijiwe
 
Nilikuwepo kwenye kikao mwanzo hadi mwisho. Mengi yanayoandikiwa hapa ni hisia zinazotokana na mazoea. Tatizo ni kwamba tumezoea siasa za ndiyo mzee, kitu ambacho hakipo CHADEMA. Ndani ya vikao vya CHADEMA tunajadiliana sana, mvutano ni mkubwa, tena wakati mwingine kwa ukali hadi mwafaka unapopatikana. Na mwafaka hupatikana kwa kuzingatia uzito wa hoja na ushahidi wa kutosha. Kwa sababu ya mazoea ya siasa za ki-CCM za funika kombe mwanaharamu apite, watu wakiona CHADEMA wakivutana kihoja wanatafsiri kwamba ni mgogoro au tatizo.

Ukweli ni kwamba kwenye kikao kulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo mbalimbali. Mwisho wa siku tumefikia mwafaka na maamuzi yamefanyika kidemokrasia na amani ni tele.

Kuhusu Shinyanga, ni kwamba ukaimishaji haukufuata taratibu na kanuni za Kikatiba. Viongozi wetu wa Shinyanga walikiri kosa lao na wamekubaliana na maamuzi ya kutengua uteuzi huo hadi hapo taratibu zitakapofuatwa. Tofauti ni hio tu, kwamba CHADEMA huchukua hatua madhubuti na mapema, badala ya kufunika kombe mwanaharamu apite.

Hivyo, ndugu zangu wapenzi wa mabadiliko katika nchi hii msinyong'onyee, there is total peace in CHADEMA and the struggle continues.

Dr.Mkumbo,
Vipi kule Nzega Dr.Slaa alipojichukulia sheria kumsimamisha Katibu wa wilaya bila idhini ya vikao halal?Bado CDM kuna double standards,hii ni CCM style mkifumbia macho mtaua chama
 
Bomu kabisa,

Mbona huwa mnalalamika wabunge wa ccm kwa wingi wao wanavyotimiza katiba kwa kupitisha miswaada mnayoita mibovu, hua kwanini mnaiita miswaada mibovu wakati huwa wametekeleza kwa kufuata katiba na huwa wanapiga kura kama katiba inavyotaka.

Kumbe ninyi mkipiga kura ndo katiba, na wa ccm wakipiga kura huwa wana ni matumbo yao? bogus kabisa.

Mnaweza kuwa mko sahihi, kama ilivyo ccm kwa wingi wao kupitisha utumbo, hebu tutajieni wajumbe wa chadema tuone kama nao hawako biased kwa ukanda .
 
Kwa usahihi ni kwamba maamuzi yalishatenguliwa na kamati kuu na baraza kuu lenye sauti ya mwisho tukaridhia pendekezo la kamati kwa kwa sababu hayakufuata desturi ya kitanzania na kanuni za chadema. Sababu za kutengua ni hizi kwa ufupi sana zilizo wasilishwa katika baraza kuu na kamati kuu.
Haiwezekani wengine wanazika na wengine wanajaza nafasi ya anyayezikwa kwa wakati mmoja. Desturi ya wapi?
Pili, Ni majuzi tu Shibuda alitoa kauli tata Bungeni huku akisifia CCM. Kauli ile ilwaumiza wengi sana nikiwepo mimi mwenywe.
Tatu, alipewa kazi rahisi sana ambayo ingemchukua kamat dk 10 kumaliza tatizo hili akitaka. Kazi hiyo ni kuandika barua ya kuwaomba radhi wabunge wa chadema. Hakufanya hivyo. Je, huyu awe msemaji wa mkoa wa Shinyanga unaoamka kwa kasi kubwa kutaka mabadiliko?
MAAMUZI YALIVYOFIKIWA.

Kamati kuu Mjumbe 1 alipinga, 3 waliabstain, na 18 waliunga Shibuda kuondolewa.
Baraza kuu,
Waliunga mkono hoja kwa asilimia mia moja bila kubadili chochote.
kwa hiyo, hii si maamuzi ya Slaa au mbowe au Zitto ama mtu yeyote bali vikao husika.
Nimeona nitoe taarifa hii maana naona wengine wanapotosha watu humu ndani.

Mkuu shukrani kwa haya maelezo. Umesema sababu kuu ni mbili: hayakufuata desturi ya kitanzania na kanuni za chadema. Kwenye desturi umesema si vyema wakati watu wanazika wengine wanagawana vyeo (Uroho wa madaraka)!!! Lakini sijaona kanuni za CHADEMA zinazomnyima nafasi Bwana Shibuda kukaimu hiyo nafasi.
 
Back
Top Bottom