Shibuda: Maaskofu muacheni Rais afanye kazi

Laurence

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
3,104
420
Ameyasema hayo huku akisisitiza kua kitendo cha maaskofu kuendelea kumuandama Raisi Jk mara kwa mara si cha kiungwana huku akiwa amefanya mambo mengi huku akiungwa mkono na BAKWATA huku wao wakisema Rais amefanya mambo mengi mazuri kwenye kipindi chake cha uongozi.

Source: Gazeti Jambo Leo
 
Hv huyu mzee ni Popo au ndege???? Mi huwaga simuelewagi na hakunaga mnafiki na mganga njaa kama huyu!!.
 
Ushauri wangu wa bure kwa Mh. Shibuda, maisha si lazima Siasa, anaweza kujaribu Taaluma, Shughuli nyingine.Maana haeleweki anasimamia upande gani, ni bora ungerudi CCM ulipotoka tujue moja unasimamia Ilani ya Chama tawala, CCM
 
Huyu njaa tu anatia aibu sana.

Mimi binafsi niliwahi kukutana nae wakati CCM wamemtema pale Dar City hotel ya paradise na nikaongea nae akiwa anamkandia huyo huyo Rais kwa matusi makubwa tena ya nguoni na kiswahili chake cha kama vile analiwa kisamaki, pia nilikuwa karibu sana na timu ya ITV iliyo muokoa baada ya kutuma muandishi aliyesafiri usiku mzima kwa gari ya kukodi kwenda kum-rescue baada ya CCM na huyo rais kutangaza kwamba amejitoa kwenye ugombeaji siku moja kabla ya uchaguzi na hakuwa na namna yoyote ya kujiokoa if not for ITV, huyu kweli anadhihirisha ya wahenga kwamba msitiri mbuzi binadamu atakuboa.

Anajikomba tu ndio asili yake, hana cha siasa wala nini, ni kujikomba tu na cha kusikitisha sasa wananchi wake hawana mbunge maana hii ni takataka, sasa CHADEMA wamejifunza, hizi takataka ni za kuchoma moto ama kuzichimbia tu ili mahali pawe safi, hivi kwa nini awasakame maaskofu anataka kupata sympathy ya waislamu na kutuzidishia vurugu za kidini, mbona waliposema Kikwete ni chaguo la mungu hakusema, na hicho anachosema serikali imefanya mambo mengi, hebu ayataje ni yepi.

Hafai kabisa huyu; wakati watanzania wanateseka na watu wanaunganisha nguvu kumuokoa mtoto wa kitanzania kwenye udhalimu wa hali ya juu yeye anaendekeza njaa na ubinafsi, hana kazi hana njia yoyote ya kupata kipato isipokua upambe ndio aponee humo, nawaonea huruma watoto wake kwa baba kama huyu
 
Kufa hafi, yaani yupo yupo tu! nadhani bado anawaza kugombea urais kwa tiketi ya ccm.
CHADEMA wanatakiwa kuchukua uamuzi mgumu kuliko ule wa NCCR
 
Ilikuaje alitaka kumng'oa hata kipindi chake hakijaisha ??

La msingi hilo sana mkuu na ndio unafiki wa huyu Shibuda unapojidhihirisha wazi,simpendi huyu mtu yani basi tuu lakn CDM kipindi kingine watizame watu wa namna hii
 
Mie mwenyewe nawashangaa sana maaskofu badala ya kukemea ufisadi ndani ya makanisa yao ambapo mafisadi wengi ndimo wanamo tokea na wao kuwakumbatia wanamwandama Rais. Hii yaonyesha maaskofu wana ajenda ya siri kwani kipindi cha BWM hatukuwasikia kabisa. Maaskofu fanyeni kazi yakuwafunza mafisadi ndani ya makanisa yenu waache uovu huo, kwani mafisadi wengi ni wakristo.
 
Hv huyu mzee ni Popo au ndege???? Mi huwaga simuelewagi na hakunaga mnafiki na mganga njaa kama huyu!!.

Shibuda ni mganga njaa pale alipo anajua kuwa amekalia kuti kavu Chadema hivyo anataka kujipendekeza kwa mkweree ili arudi ccm COME NEXT GENERAL ELECTION!!! Alivyokuwa mpumbavu anafikiri mkweree amesahau matusi aliyokuwa anamtukana alipotaka kugombea urais kwa tiketi ya ccm; mkweree ni mtu wa visasi sana sidhani kama atakuja kumsamehe huyu zuzu, ngojeni mtaona.
 
Ushauri wangu wa bure kwa Mh. Shibuda, maisha si lazima Siasa, anaweza kujaribu Taaluma, Shughuli nyingine.Maana haeleweki anasimamia upande gani, ni bora ungerudi CCM ulipotoka tujue moja unasimamia Ilani ya Chama tawala, CCM

Yupo kazini (siyo ya kisiasa) kwa mitaa hiyo.
CHADEMA wamemcontain vizuri, anatafuta mahali pa kupumulia. Anapotoa pumzi ndiyo hayo unayoyasikia.
 
until recently i regarded him as crazy... but mmmmh he is stupid as well!
 
Ha haa haa! Guys you are very funny! Hivi lengo la mtoa mada ilikuwa tumjadili Mh. huyu (personality yake) au tufanye upembuzi yakinifu kwa maneno aliyoyasema.

Mi binafsi naona maneno aliyoyasema yana Mashiko kwa sababu siku za karibuni kumezuka wimbi la viongozi wa dini (Nikimaanisha wakristo na waislamu) kuidadavua Serikali kila kukicha sasa najiuliza hiviii siku serikali nayo ikiacha kazi zake za msingi (MISSION) na kuanza kuzidadavua dini hizi kwa staili ya mipasho kama wanavyofanya wao patatosha kweli!!

My take : kila mmoja afanye kazi zake za msingi kama ni kuikosoa Serikali vipo vyama vya Upinzani na Wanaharakati wengine sio kazi ya taasisi za kidini.
 
Njaa inamsumbua hata kwenye kuongezwa posho za wabunge alikuwa anapayuka na kuonyesha njaa yake hadharani
 
Huyu njaa tu anatia aibu sana.

Mimi binafsi niliwahi kukutana nae wakati CCM wamemtema pale Dar City hotel ya paradise na nikaongea nae akiwa anamkandia huyo huyo Rais kwa matusi makubwa tena ya nguoni na kiswahili chake cha kama vile analiwa kisamaki, pia nilikuwa karibu sana na timu ya ITV iliyo muokoa baada ya kutuma muandishi aliyesafiri usiku mzima kwa gari ya kukodi kwenda kum-rescue baada ya CCM na huyo rais kutangaza kwamba amejitoa kwenye ugombeaji siku moja kabla ya uchaguzi na hakuwa na namna yoyote ya kujiokoa if not for ITV, huyu kweli anadhihirisha ya wahenga kwamba msitiri mbuzi binadamu atakuboa.

Anajikomba tu ndio asili yake, hana cha siasa wala nini, ni kujikomba tu na cha kusikitisha sasa wananchi wake hawana mbunge maana hii ni takataka, sasa CHADEMA wamejifunza, hizi takataka ni za kuchoma moto ama kuzichimbia tu ili mahali pawe safi, hivi kwa nini awasakame maaskofu anataka kupata sympathy ya waislamu na kutuzidishia vurugu za kidini, mbona waliposema Kikwete ni chaguo la mungu hakusema, na hicho anachosema serikali imefanya mambo mengi, hebu ayataje ni yepi.

Hafai kabisa huyu; wakati watanzania wanateseka na watu wanaunganisha nguvu kumuokoa mtoto wa kitanzania kwenye udhalimu wa hali ya juu yeye anaendekeza njaa na ubinafsi, hana kazi hana njia yoyote ya kupata kipato isipokua upambe ndio aponee humo, nawaonea huruma watoto wake kwa baba kama huyu

Umetumia lugha kali,lakini hamna namna nyinine nzuri ya kumuelezea huyu bwana.
 
Back
Top Bottom