Elections 2010 Shibuda kujiunga na Chadema?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Shibuda ambaye alijitoa kuwania kiti cha urais hivi karibuni kumpisha Rais Kikwete, anadaiwa kuwa katika wakati mgumu wa kuamua hatima yake kisiasa kutokana na matokeo ya kura za maoni na shinikizo jipya la kumtaka ajiunge CHADEMA.

"Kweli watu wengi wamenifuata kunishawishi nijiunge CHADEMA, lakini ni mapema mno kwa sasa maana hata matokeo kamili hatujayapata na hivi sasa ndio tunaenda wilayani kupata matokeo, lakini mimi siku zote naamini kugombana na sheikh au askofu, si kugombana na msikiti au kanisa," alisema Shibuda bila kufafanua.
 
...
"Kweli watu wengi wamenifuata kunishawishi nijiunge CHADEMA, lakini ni mapema mno kwa sasa maana hata matokeo kamili hatujayapata na hivi sasa ndio tunaenda wilayani kupata matokeo...

hiyo nukuu umeitoa wapi?
au ni wewe ndio umeitunga na kutaka dunia iamini katika nadharia/ndoto yako?
tupe thread...
no research no right to speak.
 
Minda

Kilichoandikwa hapo kimetoka kwenye gazeti la Tanzania Daima leo. gonga www.freemedia.com usome kwenyewe.

Hata hivyo, binafsi sikubaliani na kila anayeshindwa kura za maoni kukimbilia CHADEMA. Hivi hizo sera za chama kazisoma lini? Tusijegeuza CHADEMA kuwa dodoki (maneno ya mwalimu) kuzoa kila mwenye njaa. Nimemuelewa Marando aliyesema wazi kwamba anaingia CHADEMA si kwa nia ya kugombea cheo chochote, bali kupigania mabadiliko ya kweli.
 
CHADEMA iwapokee wale tu ambao wana uwezo na uchungu wa kweli na nchi hii. Na hao wawe wale ambao wametupwa kwenye kura za maoni kwa mizengwe ya CCM au shinikizo la mafisadi.
 
Back
Top Bottom