Shibuda: CHADEMA nifukuzeni muone!

Amesema pia Ukimpeleka mwanamke chongo kwa Membe kwa jinsi alivyo na maneno matamu na ya uongo atakwambia huyo mwali sio chongo! Souce: Shibuda.

Maneno mengine sio mazuri kwa wanajamii fulani. Hivi wanawake wenye chongo watafurahishwa kutolewa mifano kama hii? Hata kama ana hoja, atafute mifano mbadala na siyo ya kuwafedhehesha wanajamii wenzetu.
 
Humuelewi Shibuda ww, Shibuda anawapiga madongo CHADEMA kwa mafumbo, na watu kama nyie hamuwezi kumuelewa hata siku moja
Kama hajakitaja CHADEMA kila mtu anaweza kutafsiri awezavyo! Kwa mfano naweza kutafsiri kwamba kwa kuwa CCM walipambana naye Maswa hawamwezi tena kwa kuwa anapendwa na Wana-Maswa!Unless kama uliingia kichwani kwa Shibuda huwezi kubishana na mimi!
 
Kichama Shibuda hana nguvu, anaweza kuwekewa mkakati, akafukuzwa uanachama na kupoteza hata ubunge.

Kinachwapa watu maswali hapa ni, Shibuda anathubutu vipi kuwa na kiburi hiki? Je, kashajichukulia siri nzito za CHADEMA kiasi cha kuweza kubwabwaja bila kuogopa huku akijua kwamba inawawia vigumu CHADEMA kumfukuza kwa kuwa wanajua ana siri za uongozi wa juu wa chama?
issue siyo siri za chama kumfukuza ubunge siyo rahisi kama unavyo dhani kumbuka CUF walishindwa kumfukuza ubunge mbunge wa Viti maalum toka TANGA alipo sema ataendelea kumtambua rais wa Zenji kwa Sababu yeye yupo bara hivyo siasa za Z'BAR hazimuhusu
 
Akifananisha chama hicho na utelezi wa mlenda.
Aonya kamati kuu iliyojadili haina ubavu kumtimua.
Atamba wakithubutu hilo wataona cha mtema kuni.
Adai kukataa posho ni sera za chama kilichoshinda.
Adaiwa kukutana na madiwani,Arusha wapanga siri.

Source gazeti la taifa letu:ijumaa julai 22- julai 28
www.ippmedia.com
Aondoshwe tu!!! Kwani walipokuwa wabunge 11 mbona mambo yalienda.!!!
 
Chadema wanamuogopa Shibuda kwa kuwa wanahofia nyadhifa zao katika chama zilizokaa kikabila na kikanda. Shibuda ni zaidi yao wote kwa siasa, hawamuwezi.

sina hahika kama elimu uliyonayo (japo siijui) kama uliipata kihalali, unatarajia kuolewa lini?
 
Na mara hii wabunge wa Chama Chetu walimshangilia? Au wanamsubiri awaponde CDM ndo washangilie?
 
Akifananisha chama hicho na utelezi wa mlenda.
Aonya kamati kuu iliyojadili haina ubavu kumtimua.
Atamba wakithubutu hilo wataona cha mtema kuni.
Adai kukataa posho ni sera za chama kilichoshinda.
Adaiwa kukutana na madiwani,Arusha wapanga siri.

Source gazeti la taifa letu:ijumaa julai 22- julai 28
www.ippmedia.com

Hapa uongozi wa cdm mnatakiwa muonyeshe kuwa utofauti wenu na magamba. Kama hamuwezi kuchukua uamuzi hata kama unawagharimu basi tutawafananisha na magamba tu. Jambo hapa liko wazi. Fukuza kibuda, na madiwani Arusha wakishikulia msimamo wao baada ya kuhongwa na magamba nao fukuza vile vile. Hapo tutajua ninyi ni tofauti na magamba. Vinginevyo tofauti haitaonekana. Take care
 
Chadema isimtimue shibuda kwan analeta mgongano wa mawazo unaokifanya chama kukomaa ktk kukabiliana na matatizo kama hayo.
 
Kama hajakitaja CHADEMA kila mtu anaweza kutafsiri awezavyo! Kwa mfano naweza kutafsiri kwamba kwa kuwa CCM walipambana naye Maswa hawamwezi tena kwa kuwa anapendwa na Wana-Maswa!Unless kama uliingia kichwani kwa Shibuda huwezi kubishana na mimi!
Yote2 yawezekana jibu sahihi anaro shibuda
 
huyu jamaa si ni yule aliyetaka kugombea urais against kikwete kupitia ccm kinyume na makubaliano ya chama. Unategemea nini zaidi kama alidiriki kupingana na maamuzi ya chama ndani ya ccm. Atawaharibia kokote atakakoenda
Kusema ukweli hizi kauli za Shibuda zimekosa adabu. Kwa mpenda maendeleo na anaethamini watu waliomchagua na chama alichotumia kufika Dodoma huwezi kuwakejeli maneno ya dhihaka namna hiyo. Huyu ana agenda ya siri na CCM ya kukibomoa CDM. Lakini madamu tumesha mjua ya kuwa ni mbayumbayu hakuna haja ya kuhangaika nae ila CDM mtafute mbinu ya kumchomoa aondoke. Chadema kinapendwa hatakikiamua kuchukua maamuzi maguni hakita yumba, tena ndio kitajiimarisha zaidi na watu wataendelea kukiamini. Watanzania wana kiu ya maendeleo sio propaganda za hawa walevi wa madaraka wanatusumbua na kodi zetu tunazolipa.
 
Kwa misemo yake Shibuda namfanisha na muheshimiwa mmoja alikua pia mjengoni anaitwa Mudhihiri wa Mudhihiri, ni maarufu sana hawa jamaa kwa kughani mashairi!
 
Back
Top Bottom