Shibuda awashukia mawaziri wa JK

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi (CHADEMA) Bw.John Shibuda, amesema utendaji mzuri wa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, unavurugwa na baadhi ya
mawaziri aliodai ni mzigo ambao hawana utashi na ari ya kuwatumikia wananchi na taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili mjini hapa, Bw.Shibuda alisema Bw. Pinda ana wakati mgumu katika kipindi cha uongozi wake kutokana na watendaji wabovu wasioitakia mema nchi.

Alisema uwajibikaji ni sera nzuri iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Marehemu Mwalimu Julius Nyerere, lakini viongozi waliopo wanatumia msemo huo kama wimbo ambao wanashindwa kuutekeleza kutokana na kugubikwa na ubinafsi.

"Baadhi ya wasaidizi wa huyu mtoto wa mkulima ni mzigo kwa taifa letu, hawafai kabisa kuwa viongozi walipaswa kufukuzwa na kuondolewa katika uongozi..hawana nia njema na nchi yetu,"alisema Bw.Shibuda na kuongeza;

"Nchi hii inatakiwa kuongozwa na viongozi waadilifu wenye utashi na uchungu na nchi yetu,"alisema Bw. Shibuda.

Alifafanua kuwa baadhi viongozi kuanzia wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa,mawaziri na watendaji wengine serikalini walipaswa kutimuliwa uongozi kwa kuwa hakuna wanachokifanya.

Alisema kuwa bashasha ya waziri mkuu inapotea siku hadi siku, kutokana na kugubikwa na mawazo ya ugumu wa kazi zinazomkabili mbele yake kwa kuwa baadhi ya wasaidizi wake wamemtupia majukumu peke yake.

Akitolea mfano kauli hiyo Bw.Shibuda alisema kuna sera ya Kilimo Kwanza iliyorithiwa kutokana na falsafa za Kilimo ni Uti wa Mgongo , Siasa ni Kilimo na mengineyo mfano wa haya, lakini hakuna hata kiongozi mmoja ndani ya CCM ambaye anamuunga mkono waziri mkuu katika kupigania
wakulima hali inayomfanya muda wote kukosa raha.

"Suala hili la kilimo limetelekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Bw.Pinda, wengine ni propaganda kisiasa, wanachokijua ni kupiga vita maandamano ya CHADEMA," alisema na kuongeza kuwa, wakulima wanataka kusikia maneno yenye tija kuhusu kukosekana kwa pembejeo za kilimo,na namna ambavyo serikali imejipanga kuwapatia wakulima pembejeo kwa njia rahisi.

Akitolea mfano wa ziara za CCM zinazofanywa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Bw.Nape Nnauye, kwamba zimelenga kuendelea kuwapumbaza wananchi juu ya kile kinachozungumzwa kuwa wapo viongozi mafisadi ambao hata hivyo hawachukuliwi hatua za kisheria zaidi ya
kuzungumza majukwaani.

Bw.Shibuda ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Bunge Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama alisema kuwa iwapo zingefuatwa sheria kama zile zinazofuatwa China na kwingineko,watu hawa wangepigwa risasi na kutoweka kabisa duniani na suala la kuzungumzia ufisadi lingekoma na kugeuka historia kwani hakuna mtu ambaye angethubutu kuhujumu mali za wavuja jasho.

Alisema ziara za CCM kwa wananchi hazigusi matatizo yatokanayo na ukosefu wa pembejeo na jinsi serikali ilivyojipanga kupatia ufumbuzi tatizo la wakulima, bali kinachozungumzwa ni propaganda za kukipiga vita CHADEMA kutokana na jitihada zake za kuwaamsha wananchi kujua
mustakabali wao.
 
Craaap!! Hivi huyo Pinda kalifanyia nini taifa mpaka awe mtendaji bora??? Pinda na awe wa kwanza kujizuru
 
Shibuda anapaswa asimtenge Pinda na serikali yake manake yeye ndio kiongozi,kwa sababu ndio kiongozi wao
 
Hapa Shibuda amekonga nyoyo za wengi na mimi nafikiri kwamba ministers ought to do alot more. Wengi ni watu ambao unajiuliza wamekuwaje mawaziri. Hao wakuu wa wilaya na mikoa ndiyo usiseme.
 
Hongera sana shibuda, huyo nepi yeye anajua kupiga kelele za kuadaa wananchi sioni anachofanya.Hawezi kupambana na nguvu ya umma ataishia kupata haibu na kuzalauriwa, chadema wanafanya kazi nzuri ona mambo wanayofichua bungeni unaona kabisa jamaa wanaakili na kujali wananchi.ccm mwisho wao unakuja
 
Tanzania imeshafanywa shamba la bibi,propaganda nyingi utendaji 0,kuanzia juu mpaka chini mkuu mwenyewe kageuka mtalii,kila kukicha anaangalia nchi ya kwenda.
 
Hapa Shibuda amekonga nyoyo za wengi na mimi nafikiri kwamba ministers ought to do alot more. Wengi ni watu ambao unajiuliza wamekuwaje mawaziri. Hao wakuu wa wilaya na mikoa ndiyo usiseme.

Tuangalie hizo syllogism hapa chini:

Mawaziri wote ni wabovu
Waziri Mkuu ni waziri
Waziri Mkuu ni mbovu

Viongozi wote serikali ni wabovu
Rais ni kiongozi mkuu wa serikali
Rais ni mbovu

Ni ukweli usiopingika kuwa kama tunataka kusema mawaziri wote na viongozi wote katika serikali ni wabovu basi hatuwezi kuwakwepa waziri mkuu katika ubovu kwa upande wa mawaziri na rais kwa upande wa viongozi.

Kama tunamaanisha ubovu wa baadhi ya mawaziri na baadhi ya viongozi labda tunaweza kuwakwepa waziri mkuu na rais. Hata hivyo bado wanaweza kuingia katika ubovu kwa kutumia kofia ya baadhi.

Hata hivyo iweje siku zote tuseme kuwa waziri mkuu anaangushwa na mawaziri kwa upande mmoja na rais anaangushwa na viongozi wengine wa serikali. Je, huyo waziri mkuu na rais wanajipambanua vipi na ubovu wa viongozi walio chini yao ambao baadhi yao waliwateua? Iweje walitoa maelekezo katika majukumu yao wa kazi na katika semina elekezi halafu leo tuwabebeshe lawama mawaziri na viongozi wengine huku tuwakwepa hao wa juu?
 
Tuangalie hizo syllogism hapa chini:

Hata hivyo iweje siku zote tuseme kuwa waziri mkuu anaangushwa na mawaziri kwa upande mmoja na rais anaangushwa na viongozi wengine wa serikali. Je, huyo waziri mkuu na rais wanajipambanua vipi na ubovu wa viongozi walio chini yao ambao baadhi yao waliwateua? Iweje walitoa maelekezo katika majukumu yao wa kazi na katika semina elekezi halafu leo tuwabebeshe lawama mawaziri na viongozi wengine huku tuwakwepa hao wa juu?

sijui nini kifanyike kwa hawa watu " ila mgao unakera " miaka 50 baada ya uhuru sasa chini ya mipango lukuki mmmh !!!!
 
Mbona hutuambii umenukuu toka gazeti gani? au wewe ndiye chanzo cha habari hiyo? Haujui kuwa hiyo ni plegiarism?
 
Hapa Shibuda amekonga nyoyo za wengi na mimi nafikiri kwamba ministers ought to do alot more. Wengi ni watu ambao unajiuliza wamekuwaje mawaziri. Hao wakuu wa wilaya na mikoa ndiyo usiseme.

Mkuu lakini kumbuka Pinda alishiriki katika kuteua mawaziri, vinginevyo labda katiba haikufuatwa. Hivi waziri anakuwa na mkataba kwamba ukimfuta kazi kabla mkataba wake haujaisha atakupeleka mahakamani? Kama watu hawaperform si wafutwe?
 
Kuhusu Pinda, Shibuda anaturidisha enzi zile za siasa za REDET na baadhi ya media kwamba "Kikwete ni mzuri ila anaangushwa na wasaidizi wake". Kwa Nape yupo sawa, Anatumika kuwapumbaza wananchi, nakuwaongezea maisha magumu.Nchi sasa iko gizani kwa sera mbaya za CCM.Wao wanapita huko na huko bila haya kuwadanganya wananchi. Ni wakati sasa wananchi wawakatalie na kuwambia warudi huko huko walikotoka wakatekeleze Ilani ya vyama vyao.
 
I like the Kenyan style of performance agreements and performance appraisal for all ministers, judicial officers parastatal, government agencies and members of the executive. Ni lazima viongozi hawa wawe na score cards on which to gauge their performances. Ilivyo sasa waziri hana cha kumpima nacho kwa kipindi husika. Ndo maana akina Ngeleja can afford kupiga porojo halafu benchmarks wanazoweka hawatekelezi.
 
Back
Top Bottom