Shibuda awashangaa wanaoogopa urais

Je, ungependa JMK agombee kipindi cha pili
NDIYO________ HAPANA
Mimi naanza na HAPANA hivyo hadi sasa NDIYO (0) na HAPANA (1)
Duh mnachekesha sana yaani mnaanza hapa kupiga kampeni kama vile ni wanachama wa CCM.. Kwa nini sijaze majina yenu mahala mkayatuma makao makuu ya CCM ktk kikao chao cha Kamati kuu itasaidia sana..
Nje ya hapo hainusumbi kitu kwa sababu sintampigia kura wala mgombea yoyote wa CCM..Kifupi CCM has to go!..ndio imani yangu.
Hadi sasa hivi kwa michango niliyoiona humu inaonyesha wazi vyama vya upinzani wana kazi ngumu sana...Kumbe maneno ya Nyerere kweli tupu!.. mzee marehemu Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi..Amin!
 
Shibuda naye asing'ang'anie tu kuwa ni haki yake kugombea kikatiba, pamoja na hilo atueleze mambo ya msingi ambayo yanamfanya agombee. Maana wale wanaodai J.K aendelee wanajenga hoja kuwa J.K kaongoza vizuri basi naye Shibuda atamke kuwa J.K wao Kazi imemshinda. Na kama ni mapungufu ya J.K basi atueleze na namna yeye atakavyofanya tofauti na J.K. ili tumpime kama ana dira ya kuinyosha nchi au la. Tunataka kumsikia akitamka kuwa 'J.K kazi ya kuwapatia maisha bora watanzania imekushinda, kazi ya kumbambana na maswaiba wako imekushinda. Mimi kama Shibuda nitafanya so and so.............. Vinginevyo tutamuona kuwa ni wale wale wanaonyemelea ikulu ili wakale na makundi yao ya kifisadi.
 
Hayati nyerere alishasema kuwa upinzani wa kweli utatokea CCM. hayo tumeyaona ya S Africa kugawanyika kwa ANC. Hao wanaoona wana uchungu na katiba na ilani na dira na itikadi na nchi, wajiengue kuanzisha chama mbadala, au wateue chama kimoja kama CHADEMA na kuanza kampeni
 
No one knows kama walikuwa nao au lah!! Those past days watu waliogopa kutoa maduku duku yao kwa sababu walibanwa. sasa hivi kuna uhuru wa kujieleza, ndio maana unaona watu wana sikika. Labda hata wakati huo unao uzungumzia walijitokeza watu na mawazo kama ya Mh, Shibuda ila nguvu za dola zilicheza nao.

Nionavyo mimi, Mh, Shibuda anatumia haki yake ya msingi, hakuna mahali popote panapo mzuia kusema anayo yasema. Hatu paswi kumhukumu kwa lolote.

Keep up Bw SHIBUDA.
 
Wakati wa Mwinyi na Mkapa sio sawa na wakati huu; Utamaduni wa kuogopana ndani ya CCm hata pale ambapo mtu hafai ndio umeifikisha nchi yetu kuwa maskini kiasi hiki!! Kama Kikwete anapendwa muachieni ashindanishwe na wengine watakaojitokeza kwani anachotekeleza muungwana ni hiyo hiyo ilani ya CCm kwahiyo hoja kuwa tumuache amalize kazi aliyoamza haipo; huyo mwingine ataendeleza kutekeleza ilani ile ile ya chama ambayo muungwana imemshinda; hakuna tene maisha bora kwa kila Mtanzania!!
 
wananchi walitoa mawazo yao/mitizamo yao KWA KADRI YA UPEO WAO.na shibuda nae aliwashangaa kwa mtizamo wake binafsi/mawazo na hisia zake.So,i dn't see any problem jamani.

UNAJUA NIN?si kweli kwamba wananchi hawamtaki j.k,illa WANANCHI WANAMTAKA RAISI MWENYE SIFA NA VIGEZO.raisi atakaesimama kidete kwa maslahi ya nchi

HAPPY EASTER!
 
Shibuda naye asing'ang'anie tu kuwa ni haki yake kugombea kikatiba, pamoja na hilo atueleze mambo ya msingi ambayo yanamfanya agombee. Maana wale wanaodai J.K aendelee wanajenga hoja kuwa J.K kaongoza vizuri basi naye Shibuda atamke kuwa J.K wao Kazi imemshinda. Na kama ni mapungufu ya J.K basi atueleze na namna yeye atakavyofanya tofauti na J.K. ili tumpime kama ana dira ya kuinyosha nchi au la. Tunataka kumsikia akitamka kuwa 'J.K kazi ya kuwapatia maisha bora watanzania imekushinda, kazi ya kumbambana na maswaiba wako imekushinda. Mimi kama Shibuda nitafanya so and so.............. Vinginevyo tutamuona kuwa ni wale wale wanaonyemelea ikulu ili wakale na makundi yao ya kifisadi.


Mie nafikiri anachokisema Shibuda ni sawa, Muda wa kujieleza kuwa huyu hajafanya hiki mie ntafanya hiki baado. Mbona jambo liko waazi kwamba kugobea uraisi 2010 ni haki ya kila mwana CCM. JK asiogope wala nyie mnaomuunga mkono msiogope, haki itendeke, ukifika muda wagombea wajitokeze wajieleze bila faulo wala kufanyiana usanii. Tuwe kama nchi za wenzetu jamani, kushindana ndani ya chama iwe kawaida na sio uhaini.
 
-
- By the way, Pasaka njema kwa wana-JF wote, na familia zenu popote mlipo, Mungu awajaze baraka na busara zaidi za kulisaidia taifa letu. Sasa ni wakati wa kumpa nafasi Mungu, safari kidogo, tutaonana tena next week Mungu akipenda, salam kwa familia na wote huko majumbani wakuu!

Pasaka Njema!

Respect.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!

Asante nawe pia.
 
Hoja ya msingi hapa ni kuwa, CCM ni lazima ionyeshe mfano (wa kidemokrasia) kwa kuruhusu wanachama wake wenye nia ya kuomba kuchaguliwa kupewa nafasi ya kufanya hivyo. Naamini kuwa kila atakaejitokeza atakuwa anajiona kuwa anafaa kuongoza. Kanuni, sheria na Katiba zinaruhusu wanachama hai kushiriki walau kwa kiasi hicho. Si vyema kuanza kampeni za kuzuia wanachama wa CCM kutumia haki yao kushiriki/kuomba kuchaguliwa (tena hadharani). Suala la uwezo wa wagombea kufanya lolote zaidi ya kiongozi aliepo madarakani litafuata wakati muafaka utakapofika (wakati wa kampeni). In fact, sio lazima wawe na uwezo wa kupata kura za kutosha ili wawe na sababu za kuomba ridhaa ya wananchama wenzao kuchaguliwa. Lingekuwa jambo jema kama watu wengi wenye sifa zinazohitajika kimsingi kujitokeza kugombea.

Kuna baadhi ya watu wanaodhani kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM kutaka JK aachiwe kuendelea bila kupingwa (kwa kipindi cha pili) ni kauli za kudharauliwa. Hilo ni kosa kubwa. Kauli zao zina nguvu sana. Na wanaozitoa pia wanajua hivyo. Ni kauli zinazolazimisha viongozi wengine wote kuweka msimamo katika jambo ambalo muda wake haujafika, linahusu haki binafsi za kila mwanachama kuchaguliwa (kwa siri) na ni kampeni zinazofanyika kabla ya muda wake kufika.

Ningeelewa kama harakati/kauli hizi za baadhi ya viongozi wa CCM zingefanywa wakati wa kipindi cha uchaguzi (mwakani).
 
Isnt this an act of individual publicising?
I hope he wont get threats from his decision.However I can see he isnt that strong to shake baba ridhiwani!!!!
 
Labda ulimi uliteleza alitaka kutamka kwamba CCM ni chama cha matajiri.

BAK sidhani kama ni ulimi uliteleza,bali ni hulka ya viongozi kuwadanganya wadanganyika na ni hulka ya wadanganyika kudanganyika....Juzi waliambiwa bilioni moja ni vijisenti na bado mtu huyo huyo atawateuliwa mgombea raisi masikini hao.

OK, lets say ulimi uliteleza na badala ya chama cha matajiri ama masikini, sasa ni chama cha mafisadi,je wadanganyika wataona hilo?Ama watafuata utamaduni?

Hadi hivi sasa najaribu kuangalia ni wapi masikini wa Tanzania watapata pa kutokea, tusubiri tuone kama kuna wazalendo watakaofanya kweli ndani ya ccm ili tuweze kuondokana na utamaduni ulitufukarisha na kuendelea kuwa omba omba huku tukiwa na kila rasilimali na nguvu kazi....Inanishangaza sana kuona kuwa JK aliwaahidi wananchi maisha bora kwa mategemeo ya kutembeza bakuli....How on earth? Wadanganyika hawajiulizi maswali hayo?

Kunapokuwa na Rais anayeingizwa madarakani na iterest groups,hapo tunaona shida inakuwa kwenye utekelezaji wa issues zenye interest kwa wananchi kwasababu katiba ni ya kijamaa na mfumo wa uchumi ni wa kibepari,sasa tizama loophole hapo,watu binafsi(viongozi)na magroup yao wanadai ni usalama wa Taifa kujilimbikizia mali za Taifa na nyingine kuuza kwa wageni bila kuzingatia maslahi ya Taifa...Inashangaza sana kuona jinsi mambo yalivyo halafu kuna viongozi wanaoitwa wenye busara wame relax kabisa na kusema tuendeleze utamaduni wa umasikini,kukumbatia ufisadi na uomba omba,kabla hata hawajakubali kuwa tuko kwenye serious trouble na if we've made any progress to get out of the mess,wao wanadai tuendeleze utamaduni wa upofu na ukiziwi,tuendelee kutosikia na kutokuona kuwa tunadanganywa kuwa ccm ni chama cha masikini na kwamba mafisadi wanachota vijisenti tuu.....

Watanzania watakuwa wanajianganya kama wanadhani kuwa umasikini unaondolewa na woga na ukondoo,hilo wasahau...Haki ni haki, lakini haipatikani bure,na freedom always has a cost...Utamaduni wa ccm ni kama ule wa BAATH party ya Saddam,ni utamaduni ambao ni grupu flani ndio linachagua kiongozi, na wananch kupiga kura ni kama rubber stamping tu.....Kunatokea wababe flani tu ndani ya chama na wanasema nchi itatikisika....Viongozi hao waboronge wasiboronge,wananchi watapewa tu maelezo na mambo yataendelea,ni kama some sort of monarchy lakini ni within the circle of a certain class or group of people with the same interest etc kama ilivyo kwa ccm na baath party,badala ya family kama ilivyo kawaida ya monarchy.

Nina uhakika kama tungekuwa na viongozi makini basi tungekuwa mbali,hivyo basi naona mfumo ama utamaduni wetu ni wa kutizamwa upya,binafsi nimekataa kuendelea kudanganywa,lets wait and see kama wananchi ni kweli wamebadilika kama tunavyosikia kutoka kwa kina Mwandosya,Mwakyembe na wengineo kuwa wananchi sasa wameamka na si kama zamani.
 
jmushi1,
Unajua toka mwanzo nimekuwa nikisema hakuna mtu zaidi ya JK ni kutokana na mfumo mzima wa CCM.. hadi sasa hivi chama kizima kinawakilisha makundi ya watu ndani na nje ya chama. Ndio maana nikasema kama Kikwete hafai na kweli hafai NANI anayefaa?.. watu wamekuja na majina ya watu wakifikiria kwamba hawa watu hawana makundi na kuwa wapo tayari kutuletea kile tunachokitaka ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha mafisadi, utunzi wa KATIBA mpya inayokubalika leo kulingana na mazingira yetu.. HAKUNA mtu huyo CCM!...na kibaya zaidi ni kwamba Kamati Kuu inatakayo kaa hivi karibuni nafikiri itapendekeza Kikwete kuwa mgombea pekee toka chama CCM awamu ya pili... kwa nini bado watu wanafikiria kutoka ndani ya kabati ambalo halina nguo ya kutokea..

Malecela kazungumza kuwa CCM ni chama cha maskini akimaanisha nini malengo ya chama kile toka kizaliwe, na kumtetea kwake Kikwete ni kutokana na kufahamu kuwa chama chake kimevamiwa na Mafisadi hivyo kupoteza malengo yake...Siisi wote humu ndani JF tunapingana na yote yaliyotokea na pengine kujiunga na vyama pinzani sio kwa sababu hatukipendi chama CCM, au hatupendi mrengo, sera na nguvu ambazo ziliwekwa na viongozi waliotangulia ktk kulihudumia taifa letu isipokuwa ni kutokana na viongozi wa chama hicho kupoteza miiko na maadili ya Uongozi..

Chama huongozwa na watu na ikiwa watu wenye madaraka makubwa ndani ya chama ni katika kundi la mafisadi iwe toka Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete inashangaza sana kusikia bado kuna watu humu wana matumaini kuwa yupo mtu ndani ya CCM ambaye anaweza kuleta mabadiliko mtu ambaye anaytegemea kuchaguliwa na Kamati Kuu inayowashirikisha viongozi ambao wamepooteza tayari heshima yao kitaifa...
Nachohofia mimi sana ni matokeo ya awamu ya pili, kutokana na Historia ya nchi yetu toka Mwinyi hadi Mkapa ni kwamba viongozi hawa wote waliharibu uchumi wa nchi yetu ktk awamu hizo..Na sitegem,ei zuri kutoka kwa Kikwete isipokuwa nategemea wananchi hawatakichagua chama CCM kuendelea na uongozi mwaka 2010 bali watatazama nje ya chama hicho kumtafuta kiongozi bora..
 
There is no need to wait for another five years in order to make our judgement about Kikwete's ledership role. The writing is on the wall. We should be able to tell the truth to our leaders when they failed to deliver their promises. Thanks for your services, but we are not satisfied with your leadership approach therefore we need a new direction as well as new leader. BYE BYE!
 
Bubu Ataka Kusema,
Mkuu hakuna anayekataa maelezo yako isipokuwa tunapogomba sisi ni kutokana na maneno yako mwenyewe.. Unaposema:- Thanks for your services, but we are not satisfied with your leadership approach therefore we need a new direction as well as new leader. BYE BYE!

Then WHAT?..
 
You don't know what should be the next step? :confused:
 
Kuna baadhi ya watu wanaodhani kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM kutaka JK aachiwe kuendelea bila kupingwa (kwa kipindi cha pili) ni kauli za kudharauliwa. Hilo ni kosa kubwa. Kauli zao zina nguvu sana. Na wanaozitoa pia wanajua hivyo. Ni kauli zinazolazimisha viongozi wengine wote kuweka msimamo katika jambo ambalo muda wake haujafika, linahusu haki binafsi za kila mwanachama kuchaguliwa (kwa siri) na ni kampeni zinazofanyika kabla ya muda wake kufika.

Hapa nipo pamoja na wewe. Ningpenda kuongezea kuwa sauti hizoinaonyesha dalili fulani, kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa Kikwete amebanwa ndani ya CCM kiasi kwamba nafasi yake mwakani ipo hatarini kutokea ndani ya CCM kwenyewe, otherwise, kusingekuwa na sababu ya kuanzani kumpigia debe wakati huu huku ikiwa inafahamika kuwa 'utamaduni' wa chama ni kumwachia vipindi viwili
 
Back
Top Bottom