Shibuda awa mwenyekiti mpya CHADEMA mkoa wa Shinyanga

Jana Baraza kuu la CHADEMA Mkoa wa Shinyanga limemtangaza John Magale Shibuda kuwa Kaimu Mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga (Soma majira la leo).Habari hizi zilinishtua kidogo nikawa na maswali machache:
Kweli Shibuda ametubu na kuutii uongozi wa Taifa chini ya Mh Mbowe.??
Je,Shibuda ataacha kutofautiana na viongozi wenzake hasa wabunge??
Si ni Shibuda huyuhuyu aliyekashifu wabunge wa Chadema bungeni??
Si ni Shibuda huyuhuyu aliyesema Mh Wenje hana adabu??
Si ni Shibuda huyu huyu aliyesema Chadema ni mkusanyiko wa wanaharakati wasio wanasiasa??
Je,Shibuda si alileta vurugu kwenye vikao vya wabunge wa Chadema huko Bagamoyo??
Ikumbukwe Shibuda ni mbunge pekee wa jimbo ambaye hakupewa wizara kivuli bungeni.

Nimeeleza yote haya si kwa chuki na Shibuda bali changamoto kwake kwamba alikuwa amepoteza imani na wanachama wengi kwa matendo yake yasiyotabirika na anapaswa kurejesha heshima yake kwa kutii viongozi wa chama na wabunge wa chama chake...
Chadema wawe makini kwani kwa sasa ni mbadala wa CCM, uwezekano wa kuongoza TZ unajionyesha kwa CCM sasa kutekeleza sera zake kwa kuziigiza. Hivyo wawe makini na viongozi mapandikizi au wenye tamaa ya madaraka. Tunawaombea Chadema mje mshinde uchaguzi ili muikomboe TZ.
 
Hili linanipa mashaka.Huyu shibuda ni wa kumuondoa mapema kabla hajakomaa na kuweka gamba.
Binafsi siungi mkono huyu mtu kupewa nafasi yoyote ndani ya CHADEMA.
 
Akiharibu shauri lake kimsingi tumemweka hapo strategically ili tupate kumuasses moja kwa moja kutoka kwenye site and from there we can conclude...nani kakwambia CDM is good for nothing
 
Let him be! Tunaimani na kamati iliyokaa na kuona Shibuda ndiye anayefaa kusogeza jahazi kufika pwani!
 
My only concern is his mental stability...He has a number of personalities which makes him unpredictable.HE IS A TIME BOMB.
 
Hofu za kijinga zinawasumbua akina yakhe.....yaani hamna aibu kabisaaa kusema kuwa shibuda hajahama kiroho ccm,hamjui lolote kabisaaa,bora aseme mtu asiye mtumishi wa makao makuu au asiye mwanachama wa karibu kuliko ninyi vibaraka wa ujima....mnajua kabisa madiwani wa shinyanga na wabunge wengi wa huko walipata ushindi chini ya usaidizi wake,pia ndiye aliyesimama kuwasaidia madiwani wa cdm kufungua kesi zao...je makao makuu wanasaidia nn...yaani ipo siku nitaanza kuwataja hewani nyie watu hatari sana kwa chama chetu...na huyo ndiye kiongozi aliyetayari kukaa na watu anytime na kujadili,pia msiote kumleta tumbo huku....hapati kitu.
 
ndo mambo ya siasa hayo ndugu yangu usishangae utaona :A S-confused1: mawengemwenge bure
Jana Baraza kuu la CHADEMA Mkoa wa Shinyanga limemtangaza John Magale Shibuda kuwa Kaimu Mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga (Soma majira la leo).Habari hizi zilinishtua kidogo nikawa na maswali machache:
Kweli Shibuda ametubu na kuutii uongozi wa Taifa chini ya Mh Mbowe.??
Je,Shibuda ataacha kutofautiana na viongozi wenzake hasa wabunge??
Si ni Shibuda huyuhuyu aliyekashifu wabunge wa Chadema bungeni??
Si ni Shibuda huyuhuyu aliyesema Mh Wenje hana adabu??
Si ni Shibuda huyu huyu aliyesema Chadema ni mkusanyiko wa wanaharakati wasio wanasiasa??
Je,Shibuda si alileta vurugu kwenye vikao vya wabunge wa Chadema huko Bagamoyo??
Ikumbukwe Shibuda ni mbunge pekee wa jimbo ambaye hakupewa wizara kivuli bungeni.

Nimeeleza yote haya si kwa chuki na Shibuda bali changamoto kwake kwamba alikuwa amepoteza imani na wanachama wengi kwa matendo yake yasiyotabirika na anapaswa kurejesha heshima yake kwa kutii viongozi wa chama na wabunge wa chama chake...
 
kumbe ni tetesi ! Ningeshangaa sana , nani atahutubia kwenye mikutano ya kinana ?
 
shibuda huyu pandikizi au mwingine? kama ndiye huyu ninayemfahamu labda umekosea badala ya kuandika ccm ukaandika cdm
 
Jana Baraza kuu la CHADEMA Mkoa wa Shinyanga limemtangaza John Magale Shibuda kuwa Kaimu Mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga (Soma majira la leo).Habari hizi zilinishtua kidogo nikawa na maswali machache:
Kweli Shibuda ametubu na kuutii uongozi wa Taifa chini ya Mh Mbowe.??
Je,Shibuda ataacha kutofautiana na viongozi wenzake hasa wabunge??
Si ni Shibuda huyuhuyu aliyekashifu wabunge wa Chadema bungeni??
Si ni Shibuda huyuhuyu aliyesema Mh Wenje hana adabu??
Si ni Shibuda huyu huyu aliyesema Chadema ni mkusanyiko wa wanaharakati wasio wanasiasa??
Je,Shibuda si alileta vurugu kwenye vikao vya wabunge wa Chadema huko Bagamoyo??
Ikumbukwe Shibuda ni mbunge pekee wa jimbo ambaye hakupewa wizara kivuli bungeni.

Nimeeleza yote haya si kwa chuki na Shibuda bali changamoto kwake kwamba alikuwa amepoteza imani na wanachama wengi kwa matendo yake yasiyotabirika na anapaswa kurejesha heshima yake kwa kutii viongozi wa chama na wabunge wa chama chake...
Waache wafu wazike wafu wenzao!
 
Siku zote Shibuda huwa haaminiki kwani mara nyingi anachoongea huwa tofauti na kilicho moyoni mwake au matendo yake, huyu bwana alikuwa/au bado ni UWT sasa vipi kupewa nafasi nyeti ndani ya CDM? ni sawa na leo umchukue Mbowe awe mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro kweli hiyo itakuwa imetulia? kwa mtindo huu wasiwasi yangu ni kupoteza majimbo yote ya Shinyanga, WHY NOT MPENDAZOE OR OTHERS THAN SHIBUDA?...Dr Slaa alikuwepo, Mbowe alikuwepo sasa tunaomba ufafanuzi wenu!
Huku sio kaskazini, wanamaamuzi yao na hakuna VIFARANGA HUKU
 
Jamani mimi pamoja na kuwa mwenyeji wa Mkoa wa Shinyanga lakini binafsi simkubali kabisa Shibuda kupewa nafasi kubwa kama hiyo hata kama ana kaimu atakihujumu tu chama katika muda huo...

Naomba TUMAINI MAKENE, BEN SAANANE NA wengine wa Makao makuu watueleze ukweli wa habari hii...
 
mambo ya 2011 haya
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom