Shibuda aitangaza West Afrika akiwa Dominica

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
IMG_1323.JPG

IMG_1069.JPG

IMG_1259.JPG

Ujumbe kutoka Bunge la Tanzania ukiwa nchini Dominica wakiwamo Zungu na Shibuda
 
Sijaona tatizo hapo as far as tz hatuna vazi la taifa.

Mbona sijawahi kumwona akivaa vazi hilo hapa Tanzania, hapa yupo na kaunda suti tu, iweje anunue vazi la Afrika Magharibi anapoenda central Amerika, maana yake hana msimamo siyo? Mgona Slaa, Lisu na Mbowe mahakamani wanavaa shuka za kimasai? Ningempongeza angevaa lile vazi la wamang'ati wa Singida angetuwakilisha vizuri kiutamaduni.
 
Hakuna tatizo ni vazi la kiafrika. Tatizo lako ni la kiafrika magharibi? Hapo shida ipo wapi? Shida unaileta mwenyewe: ni kama mimi ninavyoweza kuileta shida kwa kukuuliza kwa nini avae kimang'ati wakati yeye ni msukuma (unamaanisha kimang'ati ndio kitanzania? Anawakilisha wamang'ati (subset) ama tanzania (set)? Unaona sasa shida zingine tunavyozitengeneza bila sababu ya msingi?
 
Hii ilikuwa ziara ya kiserikali au binafsi,kupiga picha za miaka ya sabini kwa 2011 du!!!!
 
Hakuna tatizo ni vazi la kiafrika. Tatizo lako ni la kiafrika magharibi? Hapo shida ipo wapi? Shida unaileta mwenyewe: ni kama mimi ninavyoweza kuileta shida kwa kukuuliza kwa nini avae kimang'ati wakati yeye ni msukuma (unamaanisha kimang'ati ndio kitanzania? Anawakilisha wamang'ati (subset) ama tanzania (set)? Unaona sasa shida zingine tunavyozitengeneza bila sababu ya msingi?

IMG_1259.JPG

Wamang'ati au wasukuma, au wamasai ni watanzania si wa west Africa. Wakongo wanautangaza ukongo, na wakenya wanaitangaza Kenya hali kadhalika watanzania tuitangaze Tanzania. Wengi wetu waoga tunaelekea kuiga tamaduni za wengine wakati tamaduni zetu tunazo tu za kujivunia. Mfano yule mbunge wa kike aliyekwenda kwnye mikutano hivi karibuni huko nje na kuvaa kimasai huku kichwani kaweka mic ya kusikiliza utafsiri amenikuna kichwa, lakini wengi wetu tu waigaji wa ya kigeni na kubeza tamaduni zetu.
 
Mbona hao wanawake waliovaa suruari huwasemi? sema unamchukia Shibuda.

Hatumjadili Shibuda hapa, tunajadili vazi alilovaa. Pamoja na wanawake kuvaa suruali pale, lakini vazi linalojitokeza zaidi ni ule mvao wa Shibuda ambao unawakilisha uvaaji wa wa west Africa.
 
Hakuna hoja hapa, na sitaki kuamini kuwa walikwenda kuiwakilisha nchi kwa kuonyesha mavazi, ni hoja zake na alichojifunza huko ndio zingetuonyesha kama ameiwakilisha nchi vizuri au la na wala sio mavazi.

Na kama swala ni kuwakilisha kwa mavazi basi ulipaswa kumpongeza Shibuda kwa kuvaa vazi la Ki-Afrika tofauti na wabunge wenzake waliovaa mavazi ya Kimagharibi.
 
Hakuna hoja hapa, na sitaki kuamini kuwa walikwenda kuiwakilisha nchi kwa kuonyesha mavazi, ni hoja zake na alichojifunza huko ndio zingetuonyesha kama ameiwakilisha nchi vizuri au la na wala sio mavazi.

By the way kama unapenda sana mavazi ya kiasili basi ulipaswa kumpongeza Shibuda kwa kuvaa vazi la Ki-Afrika tofauti na wabunge wenzake wote waliovaa Kimagharibi.

Mfano yule mbunge wa kike aliyekwenda kwnye mikutano hivi karibuni huko nje na kuvaa kimasai huku kichwani kaweka mic ya kusikiliza utafsiri amenikuna kichwa, lakini wengi wetu tu waigaji wa ya kigeni na kubeza tamaduni zetu.

Unapowakilisha nchi si ushiriki wa vikao tu, mwonekano wako pekee unaweza kuitangaza nchi yako vizuri. Inaingia akiini mwako kwenda kutangaza matumizi ya ngamia huko mazingira ambayo si ya watanganyika ila ya north africa? Utavaa vali la King Mswati utakuwa unaitangaza Swaziland na si Tanzania. Tujivunie mambo yetu na wakiyaona watakuja kutalii, lakini vazi la shibuda linaeleweka kupeleka watalii west africa.
 
..Kama ingelikuwa walikwenda kuonyesha mavazi basi Warembo na Wanamitindo wangefaa zaidi kwa hilo kuliko hao Wabunge, na kwa kuwa hawakutumwa wanamitindo basi fahamu kuwa hoja na walichojifunza ndio muhimu na wala sio mavazi.

Last time i checked hakuna vazi la Tanzania.
 
lakini FF hayo mengine ya kikatolika aka Roma italia na mengine ni ya ........ wastaarabu aka Mecca
 
ya huku kwetu ni mgolole, au ya wagogo, wamasai, wamangati, wahehe nk nk
 
lakini FF hayo mengine ya kikatolika aka Roma italia na mengine ni ya ........ wastaarabu aka Mecca

Hizo ni fashen tu tofauti lakini zote kanzu, hata ukitembea mitaani leo utakuta wanavaa kanzu tofauti kwa mikato, mishono, lakini zote kanzu tu.

Na hilo ndiyo vazi letu la Taifa kwa wanaume kwani linakubalika na dini zote, tabaka zote, hazijalishi maskini wala tajiri.
 
Back
Top Bottom