Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Msimamo wake
Lakini Shibuda alilimbia gazeti hili jana atashangaa kama atatuhumiwa kwa maoni yake binafsi aliyoyatoa bungeni juzi juu ya kutaka wabunge waendelee kulipwa posho za vikao vya Bunge.

"Nitashangaa kama nitaitwa na kiongozi yoyote wa kambi yetu ya upinzani au Chadema kwa tuhuma za kutoa maoni yangu huru niliyoyatoa bungeni jana (juzi), hata nilipokuwa CCM nilipenda kusahihisha palipokuwa na makosa".

"Sitarajii Chadema kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama mimi sitakiwi kutoa maoni huru basi hakuna maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".

"Tusitafute hila na visa kwa maslahi binafsi, tutambue kwamba mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".

Alisema kwamba hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho ya vikao vya Bunge.

Shibuda akifafanua zaidi suala hilo la posho japo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chake ilitaka kupunguza posho hizo za vikao pamoja na mshahara wa mbunge, alisema, "Ilani ya Uchaguzi ni mpango kazi wa kuendeleza programu ya chama kilichopo madarakani, kwa hiyo hivi sasa hapa bungeni bila kujali itikadi zetu wabunge tunaunganishwa na programu ya kuendeleza nchi, utawala bora na uongozi wa kuongoza fikra za Watanzania".

Sijui!! Lakini kuna ka ukweli hapa na ndio maana wakubwa wa humu (Jamii Forum) hamleti mjadala!
 
yaonyesha kuwa Shibuda si mmojawapo wa CDM. Hana taarifa na yanayofanywa na WanaCDM kama wabunge. Yupo yupo tu kama mtu aliyekosea njia. Kama hayo ni maoni binafsi je na posho anachukua!!??
 
Kuna mtu mmoja, ambaye ana uzoefu na vichaa kwa muda mrefu, baada ya kuusikia mchango wote wa Mh Shibuda alinishtua aliponiambia kuwa Mh huyu ni kichaa. Eti mtu unaweza muona (seemingly) kuwa safi na mzima kumbe ka asili mia ka ukichaa kako juu.
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.
 
Huyu wamtose tuu kwani hana pakwenda ss vi amekuwa anatoa msimamo tofauti na chama chake
 
sHIBUDA BI mSALITI,
SHIBUDA NI CHIZI
SHIBUDA SI MTU WA KUWA CHADEMA
SHIBUDA HAJUI SIASA ZA CHADEMA
SHIBUDA HAIWEZI CHADEMA
SASA SHIBUDA AFUKUZWE CHADEMA AENDE KWA MAFISADI NA WEZI WENZAKE CCM
 
Ushauri:
CDM wanatakiwa kumuacha shibuda huko huko CDM lakini wamdhibiti kama alivyodhitiwa Samuel Malechela huko CCM.Asipewe na nafasi ya exercise anything for CDM kwisha hadi afike 2015 then mnatafuta teenager wa kisukuma MSOMI wa kileo pale Maswa anachukua jimbo kwisha!!!! Hakuna haja ya kuumiza vichwa huo ni mfupa uliomshinda fisi(CCM).Watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa Maswa kwa sasa ni halali ya CDM hata CCM wanalijua hilo.Wale ni wasukuma bana wakisema Dasamaga they mean it.
 
shibuda,shibuda ni mzigo kwa wananchi wa jimbo lake,tunasikitika sana sisi wana mapinduzi kuwa na kiongozi mwenye fikra potofu! angalia shibuda tutakumwaga!We are here for serious development! not jokes!
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.

sHIBUDA amekuwa CCM muda sana na tena alikuwa mjumbe wa NEC na alikuwa akishinda kwa kura nyingi tu.Lakini ilifikia CCM wakagundua tatizo la shibuda na wakajitahidi kumkanya lakini hakujirudi.Ikafikia hali ya kutokuelewana na KAMATI KUU YA MKOA hadi RC.Hapo CCM wakasema basi na aende japo ni potential kwa chama mkoa.Hata CDM wakimtema hakuna atakayeshangaa mkoani SHY.kwa taarifa yako siasa za SHY kwa sasa zinahitaji mtu aliyekwenda shule, umma wa shinyanga unahitaji maendeleo na sisi ubabaishaji ndiyo maana CCM wamemwagwa.Shibuda must go, his service potential has started declining.
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.
huu ni uchizi. CCM walimnyanyasa kwa sababu gani? Unatufanya sisi wote humu ndani kichwa cha mwendawazimu?
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.
Mabata hujulikana kwa uharo!
 
Wewe ni mgonjwa wa akili kama Shibuda!!
 
Ndugu RITZ, wewe ndiye Mkabila na Mdini.
Utavuna unachopanda.
 
Kutohudhuria vikao vya wabunge wenzake (km hoja ni kwamba hakuwemo kikaoni) wa chama ni kosa pia.na angeweza kuwasilisha mchango kwa njia ya maandishi..! na kama anafuata demokrasia kweli basi pia angefuata hata collective responsibility ambayo wabunge wengi walitoa msimamo wa pamoja katika kikao rasmi..! ameshindwa kutimiza wajibu wake katika Vikao rasmi anabwabwaja nje! hafai..afukuzwe!..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom