Elections 2010 Shibuda ahamia CHADEMA

Wewe hujaelewa somo, tatizo si kwamba wasihame vyama. Mimi sitaki huu umalaya wa kisiasa na uroho wa madaraka wa kusubiri mpaka ushindwe primaries za ubunge ndio uhame chama. Kama unahama chama on principles bila tamaa ya madaraka poa tu, kaa miezi mitatu na kamisaa mnajadili mambo, soma literature za chama, unapigwa msasa watu wanakukubali.

Sio leo umelala CCM, kesho unaamka unakuwa CHADEMA, keshokutwa mbunge wa CHADEMA. Hata itikadi ya chama na sera zake hujui.

Mambo ya aibu hayo.
Wewe unajua malengo ya chama cha siasa au unaropoka tu, ni pamoja na kuingiza wanachama kwa mbinu zozote zile.
 
Hao ndio wana si hasa na si hasa zao, mambo yakibana haraka haraka wanakuwa vinyonga na yakiwa safi ni kauli moja. ''tuna msimamo''
sina hakika iwapo bwana John alikuwa na mpango au aliwaza siku moja atahama C C M (tetesi)
maisha ya si hasa ni popote, chama si Baba wala Mama. Nenda Ngoshaa...!
 
Wewe unajua malengo ya chama cha siasa au unaropoka tu, ni pamoja na kuingiza wanachama kwa mbinu zozote zile.

Hata kwa chinja chinja? Wewe unaelewa tofauti kati ya uanachama wa kawaida na mwanachama kupewa nafasi ya kugombea ubunge katika chama?

Marx Groucho alisema "I refuse to join any club that would have me as a member." Hizi types za Shibuda naona zina msimamo ulio reverse hilo kuwa "I will join any party that would have me as a member" and get them to parliament of course.
 
Hata kwa chinja chinja? Wewe unaelewa tofauti kati ya uanachama wa kawaida na mwanachama kupewa nafasi ya kugombea ubunge katika chama?

Marx Groucho alisema "I refuse to join any club that would have me as a member." Huyu Shibuda naona ana msimamo ulio reverse hilo kuwa "I will join any party that would have me as a member" and get him to parliament of course.
Hayo ni mawazo yako, siku hizi sikutofautishi wewe na Malaria Sugu=Tumain yeye ni udini wewe ni u much know wote mko kwenye group moja la kukera ila mnapishana kwa viwango. Nilishamwambia MS kama anaona namkera na yeye ananikera vivyo hivyo, na wewe kama utaniona sina point na wewe nakuona huna point vile vile.
 
Point well taken, you don't like me and you think I don't have a valid contribution.

Kama nilivyosema mwanzo, siko hapa kupendwa, sitafuti sifa wala siogopi lawama.

Huk kwenye kusema sina point, the central idea ya forum hii ni kujuzana kwa mazungumzo ya back and forth, sasa wewe huna majibu kwa maswali yangu, unakimbilia kusema mimi much know, unalia lia tu.

Unaoneka huna nyimbo, na kama hupendi kusoma maneno yangu kuna feature ya kuniscreen uione posts zangu kabisa, jifunze kutumia JF labda itakusaidia usikereke zaidi. Your loss.

Ninaowakera hawana muda hata wa kusoma posts zangu, sembuse kunijibu.

Wewe unanisoma, unanijibu, nakujibu, unanijibu, wewe huwezi kusema nakukera, nikikukera utaruka ninachoandika.
 
Kwani jamani mtu akihama nyumba ni vibayaa!
Ni maamuzi yake na yeye anajua kipi anafata nyumba nyingine, hapo hakuna sheria inomfunga lakini ujue afikapo tu kule kupya, basi kuna sheria zake,
Basi Bw. Shibuda hajavunja aendako hali kadhalika atokako, mwache aende na huko ndo apimwe kwa utendaji wake.
Siasa ni biashara kama biashara nyingine za faida na hasara.

''WHO JAH BLESS NO MAN CURSE''
 
Hata kuhama nyumba kuna contracts na documents za kusaini na kukubali, sio unakurupuka tu unaingia nyumba ya watu, halafu si unaingia tu, unaingia halafu hapo hapo unataka ukiranja.

Hata hao watoto wa nyumba uliyohamia watakuona hili jibaba vipi, mbona linataka kupata ubwete ubwete kirahisi tu.

Respect you have to earn, na huko CHADEMA sioni kama mtu anaweza kujiprove na ku earn respect katika muda mfupi.

Tatizo wote CHADEMA na Shibuda chancs are wako desperate kupata ubunge, kuna mkuu kashaleta mahesabu ya ruzuku hapa.

Hivi hiki ndicho motivation kubwa kabisa ya vyama vyetu ? Ruzuku ? What happenned to the peoples business ?
 
Huyu kinyonga naye sishangai...kinachonishangaza anachelewa tu kuwafata akina Lwaks na Akwilombe wenzake huko...!
 
Hivi unapohama chama kwa ghfla hivi(kama amehama ) ni kwa kuwa anaamini in both sera za ccm na chadema au?

Au anaamini kuwa yeye tu ndie anaeweza kuwatumikia wananchi wa jimbo Hilo?
 
Kuna baadhi ya wana CCM wakihama chama nak uingia upinzani %ge ya shaka inakuwa ndogo. Mfano mdogo tu nikilinganisha Shibuda na Mpendazoe binafsi kwangu naona Shibuda anahitaji kutathminiwa zadi hata ya mpendazoe kwa chama chochote atakachokwenda kabla ya kukubaliwa au kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama.

Lest assume Shibuda inakuwa kweli kahamia chama XYZ and let assume kuwa JK kashinda Urais anamchagua Shibuda kuwa Mkuu wa Mkoa, au wilaya GGGG.Je wataka mabadiliko tunatakiwa tufurahi?????. Binafsi kwa mtazamo wangu itakuwa ni mazingaombe.

Shibuda huyu mtani wa JK tena utani na mzaha wao wanauonyesha wazi wazi angehamia CHADEMA au CUF 2015 wakati JK kaondoka nisingekuwa na shaka sana lakini kwa mwaka huu 2010 mhhhhh.

Bora ahame Malechela lakini kwa shibunda mhhhhhnnn . Nimekuwa nikimfatilia sana huyu jamaa trough vyombo vya habari.

Na probability ya shibuda kuondoka CCM ni ndogo mno.
 
Mi nafikiri hapo anakuwa haamini CCM wala CHADEMA bali tatizo lake ni kutamani na haamini kwamba ameshindwa...
Kishapu wana kazi ya kuthibitisha kuwa wao ni wapiga kura wa aina gani,
wapigia CHAMA... Au Wapigia MAJINA... Nafkiri iwapo hicho CHAMA Kipya kitamsimamisha yeye basi ndipo hapo majibu yatapatikana.

Na iwapo atashinda nitaamini kuwa wabongo wengi ni bendera fwata upepo(bado sijaamini hivyo)
Unajua kwanini nimesema hivyo?
Kwasababu ebu fikiria we ni mwanachama CCM NA KADI UNAYO. Siku ya uchaguzi unaenda kuchagua JINA.. Tena ktk chama kingine tofauti na kadi iliyopo kibindoni... Kisa? Una mapenzi na JINA? Mbona hukuhama naye? We utakuwa msaliti (hiden/secrecy betrayal).
Japo Chama si Baba wala Mama zetu je? Huo ni ushabiki au?
Hapa kazi ipo kwa wanachama mamluki/ wanachui ndani ya ngozi kondoo.

Politricks mmh! Acha tu!
 
Huyo jamaa akitoka CCM saana saana UDP kwa Cheyo ndio wanaweza kuelewana, na kama ni ile ya kikweli kweli sio mwaka huu labda 2012/13 kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015
 
Hivi kuna mtu yeyote anayemchukulia serious huyu Shibudu?

Mazee kuna watu wanakwambia akija CHADEMA anaweza kuchukua jimbo halafu waende kuongeza viti vya bunge, na ruzuku.

Tamaa ya viti vya bunge na ubunge hata haiwezi kuona kwamba huu mkangafu hauchaguliki kwa wananchi.
 
Bongo wamejaa mazuzu kila kona, sishangazwi na huo upupu.

Zuzu + Zuzu = Mazuzu.
 
Hivi unapohama chama kwa ghfla hivi(kama amehama ) ni kwa kuwa anaamini in both sera za ccm na chadema au?

Au anaamini kuwa yeye tu ndie anaeweza kuwatumikia wananchi wa jimbo Hilo?

Wanaohama vyama ghafla wamegawanyika kwenye makundi tofauti, kulingana na mtazamo wangu.

Kundi la kwanza ni opportunists, ambao wako kwenye vyama kwa ajili ya kutaka ulaji, sasa ulaji ukiingia mchanga inabidi ahame kwenda kutafuta sehemu nyingine.

Kundi jingine, wako wanachama wa CCM ambao wanaendelea kuwa wanachama lakini kiundani wamechoshwa na madudu ya humo ndani, so ikitokea opportunity ya ku-trigger kuhama kwake, anaitumia kuondoka. Tatizo la kundi hili ni ngumu kuwatofautisha na opportunists na hasa wanapohama baada ya ulaji kuingia mchanga.

Kundi jingine, wako wana CCM ambao wakionewa na mfumo mbaya wa chama chao, huamua kuondoka na kwenda kujiunga na chama ambacho wanahisi labda mfumo wake ni mzuri. Mfano, assuming mtu ameshinda kihalali kwenye kura za maoni, halafu jina linaenda CC na NEC, jamaa wanalikata bila kutoa maelezo ya kueleweka, hakuna mtu anaweza kuvumilia hayo mambo.

Kwenye hili kundi la mwisho ndipo sasa watu hupozwa na nafasi za kuteuliwa. Hivi majuzi JK amesema kwamba wale waliokosa wawe na subira, kuna nafasi nyingi za kuteuana maana mvumilivu hula mbivu. Mfano, Dr. Tizeba alishinda mwaka jana kwenye kura za maoni, jina halikurudi. Zikaanza chokochoko za wana CCM wao wenyewe kushitakiana mahakamani, baada ya hizo chokochoko Dr Tizeba akapewa ukuu wa Wilaya Sikonge. Bwana Kangoye baada ya kugaragazana kwenye kura za maoni na uchaguzi mdogo wa Tarime, alipigiwa pande la ukuu wa Wilaya. Kuna watu wengi wanapewa post za kuwapoza ili wasiondoke, lakini inaonekana wazi kwamba wako frustrated.

Swali ambalo ninajiuliza kila siku, mtu ni Mkuu wa Mkoa/Wilaya kazi ambazo ni za kuwatumikia wananchi lakini bado anakwenda kusaka Ubunge, kwenye Ubunge kuna nini? Nina orodha ndefu sana ya hao wakuu wa wilaya na mikoa ambao wanakimbilia kwenye Ubunge na wengine huwa wana kofia mbili kabisa, yaani Mkuu wa Mkoa na Mbunge. Mfano Bwana Lukuvi, Monica Mbega, Mohamed Abdulaziz na Dr. James Msekela (hawa wote ni wakuu wa miko) na mwaka huu walienda kuomba ridhaa ya kugombea. Orodha ya wakuu wa wilaya ni ndefu zaidi. Hivi jamani kwani mtu akiwa mkuu wa wilaya/mkoa siyo kwamba anatumia umma huo huo? Au mishahara na marupurupu ya Ubunge ni makubwa sana?
 
Point well taken, you don't like me and you think I don't have a valid contribution.

Kama nilivyosema mwanzo, siko hapa kupendwa, sitafuti sifa wala siogopi lawama.

Huk kwenye kusema sina point, the central idea ya forum hii ni kujuzana kwa mazungumzo ya back and forth, sasa wewe huna majibu kwa maswali yangu, unakimbilia kusema mimi much know, unalia lia tu.

Unaoneka huna nyimbo, na kama hupendi kusoma maneno yangu kuna feature ya kuniscreen uione posts zangu kabisa, jifunze kutumia JF labda itakusaidia usikereke zaidi. Your loss.

Ninaowakera hawana muda hata wa kusoma posts zangu, sembuse kunijibu.

Wewe unanisoma, unanijibu, nakujibu, unanijibu, wewe huwezi kusema nakukera, nikikukera utaruka ninachoandika.

Yaani ww ni man at work uko hapa kwa kazi maalum kuhakikishaunaitetea CCM kwa njia yeyote ,kwa mtu mwnye shaka na hili afuatilie post za huyu joka kuu.
Anyway ndio demokrasia hukatazwi kufanya kazi yako ila nawaonya watu humu.
Kama watakufuatilia you suck big time na kazi yako agent one.Inawezekana watu wanalala mika ufisadi wakati ukoo wako unanufaika you got to do you got do.
 
Tukifuatilia mambo ya itikadi za vyama tutakenda mbali sana kwa sababu Tanzania haiwezekani! Tukumbuke mpaka leo hii mtu aliyekubali kushindwa na kuamua kungangania itikadi za chama chake ni baba wa taifa peke yake JK Nyerere! Wote waliokuwa wakimuunga mkono walimwacha na ujamaa wake wakahamia kwenye ubepari!!
Hapa dhana ya mtu uhama chama nafikiri kutokuridhishwa na mazingira yaliyomfanya akashindwa, ambayo yatadhihirika kuwa ni kweli ikiwa atashinda kama alivyo fanya Dr Slaa wakati akigombea ubunge Karatu!
 
nn umesema kweli yaani anauliza baada ya muda anajijibu mwenyewe anasahau kama aliuliza swala hilo. Tatizo la kiranga huwa ana muhe muhe wa kujibu haraka haraka bila kuelewa hoja inataka nini ni kama vile amesetiwa na jibu moja tu kichwani. Mfano kama kichwani ameseti jibu la 'hakuna kugombea kama umehama chama', hata akielezwa mbona katiba haisemi hivyo lazima jibu lake liwe hilo hilo moja tu.

huyu kiumbe ni wa ajabu simuulewe kama yuko hapa kwa kazi maalum,kama ulivyo ainisha hapo juu anakuwa kama kasetiwa ktk kuongea msimamo fulani tu kwake hakuna majadiliano
 
chadema hawana mpya yoyote kazi yao itabaki kutamani tamaufu ya fisi mkono wa mwanaadamu utaanguka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom