Shibuda ageuza bunge sehemu ya mipasho!

nimekua nikifuatilia bunge la kumi tangu lilipoanza, hakuna jipya zaidi ya kupigana vijembe na majungu, yaani kila mbunge anaye pata nafasi ya kuchangia huanza na kuilaumu chadema, hatakama tuhuma ni za uzushi, jamani fanyeni tuliyo watuma!!!!!!
 
Nianze kwa kusema kuwa misingi ya demokrasia imejengwa tangu enzi na enzi katika principle ya demokrasia na uwajibikaji. KWa maana nyingine, demokrasia kamwe haiondoi uwajibikaji wa watu husika. Hii ndio maana pamoja na kushinda kwa kishindo, Hitler aliondolewa madarakani kwanguvu ya majeshi ya kimataifa katika vita kuu na sasa tunaona hata baada ya kushinda uchaguzi Mubarak ameondolewa kwa sababu ya kushindwa kuwajibika baada ya demokrasia kumpa ukuu wa nchi.

Tukirudi nyumbani CCM iliwahi kuwa chama nguli kisicho na mpinzani. Naam, ni unguli wa CCM uliofanya hata kura ya maoni kuona kwamba Tanzania ipo tayari na vyama vingi ilileta matokeo kuwa watanzania zaidi ya asilimia 90% waliona CCM inafaa kuongoza pekee. KWanini CCM ilikuwa bora? Ni kwasababu Nyerere alihakikisha misingi ya demokrasia na uwajibikaji inatunzwa wakati wote akiwa hai. Nitakupa mfano hai wa marehemu Horace Kolimba Katibu Mkuu wa Zamani wa CCM. Huyu kwa kutumia "demokrasia" aliongea waziwazi kuwa CCM imepoteza dira. Tukumbuke kuwa Kolimba hakuwa fisadi na wala hakuwa na kashfa yoyote ile wakati huo. LAkini Nyerere alimkanya na baadae kiumtungia kitabu (na Kolimba alitimuliwa CCM badae) kwa sababu ya msimamo wake huo. Sio kwamba alionewa ila aliadabishwa kwa kutumia uhuru wa kuongea (DEMOKRASIA) vibaya. Kolimba kama kada mwandamizi alitakiwa ajue kuwa ALIWAJIBIKA kuionya CCM lakini katika platform (eneo) maalum kwa kufanya ivyo. Kolimba angeweza kuionya CCM katika vikao vya chama na huko angesikika vyema. Lakini kwa yeye kutumia platforms zisizo sahihi, aliitumia Demokrasia vibaya.

Miaka imepita na Nyerere hayupo tena. KWanini nasema CCM ni mfu. CCM imekufa kwasababu uwezo wa chama kuruhusu demokrasia huku ikihakikisha uwajibikaji haupo tena. Leo hii Lowassa anaweza kujiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa ya ufisadi lakini bado anapewa uhuru wa kuwa mjumbe wa kamati mkuu na sasa mwenyekiti wa kamati ya bunge. Ni ufu huu huu unaomwezesha Rostam kuonyoya Tanzania kwa Richmond, DOWANS lakini bado ni muheshimiwa CCM. Uhuru wanaopewa akina Makamba na Tambwe Hiza kutukana hata marehemu wa Arusha bila kuwajibishwa kutokana na matamshi yake ndio ulioiua na unaondelea kuiua CCM paka sasa hakuna mtu mwenye haki na akili sawasawa anataka kuwasikia.

Nirudi kwa Cancer ya CHADEMA niliyoiita SHIBUDA. Ikumbukwe kuwa cancer hii iliingia CHADEMA pale tu iliposhindwa kura za maoni CCM. KWaiyo CANCER SHIBUDA hakuwa na nia ya ndani ya ila tamaa ya kuukwaa ubunge ndio uliompeleka CHADEMA. Angesamehewa na kukubalika ikiwa tu ana adabu na kufuata principle ya uwajibikaji. Kinyume chake, CAncer SHIBUDA amekuwa mstari wa mbele kusambaza sumu CHADEMA. KWa mfano:

1. Aligoma kuingia na kutoka wakati wa hotuba ya mkwere kinyume na uamuzi wa CHADEMA uliotokana na kura halali za wanaCHADEMA walioko bungeni.

2. Alihudhuria sherehe iliyoandaliwa na CCM ya kufungua bunnge kinyume na matarajio ya wana CHADEMA

3. Katika tukio la mauaji ya ARUSHA ameonyesha wazi kuwa upande wa CCM

4. Amewahi kukunjiana ngumi na mbunge mwenzie toka MWanza amabe ni mwana CHADEMA halisi bwana Ezekiel Wenje

Haya yote na mengine yanaonyesha kuwa CANCER SHIBUDA haifai kuwepo CHADEMA na ikiachwa kama CCM ilipotoka kupendwa na zaidi ya asilia 90 ya watanzania na sasa kuchukiwa, CHADEMA itafika huko si muda mrefu.

NAWASHAURI VIONGOZI WA CHADEMA KUFANYA KIUME NA KUMVUA UANACHAMA CANCER SHIBUDA. Nafahamu mbunge mmoja atapungua ila nina uhakika hiko kiti kinaweza kurudi CHADEMA maana watu wameichoka CCM.

Pili chaguzi ni nzuri kwa upinzani maana zinaviweka vyama vya upinzani kwenye macho na masikio ya wapiga kura. LEteni by election na watu wataendelea kuwasikiliza maana kama mnavyoona, PUNGUANI MAKINDA hatawawezesha kuongea bungeni.

Nafahamu kuwa Zitto nae amekuwa ndumilakuwili kama CANCER SHIBUDA ila kwa mawazo yangu, kabla ya mkwere kumpa nafasi katika kamati ya madini, Zitto alikuwa anajitambua. In fact, wakati huo Zitto alikuwa moto kuliko hata Dr. Slaa. Na kwasababu CHADEMA imetoka mbali na Zitto, naamini amekwisha earn respect tofauti na hii CANCER iitwayo SHIBUDA. TAFADHALI CHADEMA msichelewekumuondoa CANCER SHIBUDA manake msipom-discredit mapema, ataendelea kutumiwa na CCM kuisambaza sumu yake CHADEMA na kukiuwa chama. Kolimba alitimuliwa kwa kuwa mkweli bila kuwajibika sembuse hii CANCER ambayo haina faida na CHADEMA? CHADEMA ni wakati wa kuonyesha kuwa hakuna aliye juu ya chama. NAOMBA KUWASILISHA!!
 
Kambi ya CDM imeanza kwa kususua, wakati wenzao wamepania kuwaonyesha kuwa si lolote si chochote, wenyewe wameamua kuwa "apologetic". Hilo litawamaliza. Jambo lingine litakalo imaliza CDM ni kutowachukua hatua dhabiti watu kama Shibuda ambaye dhahiri kwake yeye CDM ameitumia kama ngazi ya kupata ubunge, vinginevyo yeye ni CCM damu damu.

Kwa nijuavyo wanasiasa wa kitanzania hawwana hiyo ya kuwa 'damu damu' kwenye chama fulani simply becauase we dont appreciate the value of having ideology. Kwa wanasiasa wa aina ya shibuda yuko tayari kwenda chama chochote kile ili apate ubunge! kuwa yeye ni CCM damu damu si kweli huu ni uongo!! CCM damu damu wamweke rumande siku tatu still awapende?

CDM inapaswa ikuze demokrasia ya ndani ya chama kwa bahati mbaya demokrasia ya CDM within ni F! haimo CDM ni kama CCM mwenyekiti hasemwi waziwazi, maamuzi lazima yawe ya pamoja na aliye kinyume si mwenzetu this manifested by CDM from her members to fans!! demokrasia ya ndani ya chama inapaswa kuwa MTAJI...leo hii Mbowe akisemwa vibaya ndiyo demokrasia yenyewe , uhuru wa kujieleza!! bahati mbaya ili linakuwa ndiyo ajenda kiasi cha kuathiri uwezo wa kawaida wa kufikiri, uki-recall incident za Zito za kuporwa uongozi , mara kurudishiwa unaweza kusema haraka kuwa they have problema somewhere.

Kuna Incident mbili tatu ambazo CDM they dont want to recall kuhusu shibuda, aliwekwa kikao hivi alifanya nini? maana tatizo limeanzia huko, Shibuda si mfuata mkumbo!! ana misimamo yake na hii imekinzana na CDM since then!! ndiyo leo analeta maneno ya aina hii kama kuiponda CDM! mkisitisha uanachama wake hivyo afutwa ubunge, ataenda CUF na ubunge atashinda tena!!

All in all Shibuda ana simama vizuri sana kama mgombea binafsi!!
 
Hivi are these people worth hizo pesa wanazopata ?, mi naona wanafanya usanii kwa mtaji wa kodi zetu.., mjengoni ni full kupongezana na kupigana vijembe.... Now more than ever nadhani itabidi tuangalia mishahara na marupurupu yao..
 
Hivi are these people worth hizo pesa wanazopata ?, mi naona wanafanya usanii kwa mtaji wa kodi zetu.., mjengoni ni full kupongezana na kupigana vijembe.... Now more than ever nadhani itabidi tuangalia mishahara na marupurupu yao..


Ndiyo watanzania walivyozoea! na vyama vinaringia kuwa na wabunge wengi!!! bunge halina faida na wabunge nona wasanii tu, HAMNA KITU PALE
 
nimekua nikifuatilia bunge la kumi tangu lilipoanza, hakuna jipya zaidi ya kupigana vijembe na majungu, yaani kila mbunge anaye pata nafasi ya kuchangia huanza na kuilaumu chadema, hatakama tuhuma ni za uzushi, jamani fanyeni tuliyo watuma!!!!!!
VIJEMBE, MIZENGWE NA MAJUNGU BUNGENI NI LESENI YA
UHAKIKA KUWAREJESHA WABUNGE UCHWARA
USWAHILINI WAKALEE WATOTO


Kwa mtaji wa hizi kura za kuchakachua huenda wapiga kura tulipitiwa hata tukawaachia watu wa darasa la saba, la kumi na mbili na wale wa darasa la kumi na nne nao pia wakawa wamejazana kwenye viti vyetu vya uwakilishi huko bungeni.

Kwa karne hii ya 21, watu kama hawa licha ya kuwa na haki kikatiba nao kutia timu, wabunge wa aina hii ni mzigo mkubwa sana kwa wapiga kura. Kazi yao kubwa ni kuvuta posho, kuchelewesha mijadala kwa kutokuelewa kinachoendelea kwa urahisi, na wakati mwingi HULAZIMIKA KUFUATA MKUMBO ILI PICHA ISIJE IKAUNGUA kwamba ni aina mojawapo wa wabunge si riziki.

Itachukua muda kuondoa bangi vichwani mwao baadhi ya wabunge wetu ambao tafsiri ya uwakilishi mzuri ni vijembe, zomeazomea, kiongozi wa fitna na mizengwe na mambo kama hayo.

Hkika inasikitisha kwamba wabunge wa aina hii BADALA YA KUFIKIRI OBJECTIVELY KWA MASLAHI YA TAIFA, WAO HUHAMISHIA UDHAIFU WAO WA UFINYU WA kupokea changamoto za mawazo pinzani na kuanza vita dhidi ya watoa hoja alimradi tu ionekane nao wako bize na kujishughulisha huko hata kama hakuna tija wanayoletea taifa kwa michango yao.

Naamini kwa Tume huru ya Uchaguzi, hakuna chuya za aina hiyo itakayopita nje ya makubaliano ya kura zetu na kufanya wabunge wabovu kujaa mjengoni tena.
 
Nafahamu kuwa Zitto nae amekuwa ndumilakuwili kama CANCER SHIBUDA ila kwa mawazo yangu, kabla ya mkwere kumpa nafasi katika kamati ya madini, Zitto alikuwa anajitambua. In fact, wakati huo Zitto alikuwa moto kuliko hata Dr. Slaa. Na kwasababu CHADEMA imetoka mbali na Zitto, naamini amekwisha earn respect tofauti na hii CANCER iitwayo SHIBUDA. TAFADHALI CHADEMA msichelewekumuondoa CANCER SHIBUDA manake msipom-discredit mapema, ataendelea kutumiwa na CCM kuisambaza sumu yake CHADEMA na kukiuwa chama. Kolimba alitimuliwa kwa kuwa mkweli bila kuwajibika sembuse hii CANCER ambayo haina faida na CHADEMA? CHADEMA ni wakati wa kuonyesha kuwa hakuna aliye juu ya chama. NAOMBA KUWASILISHA!!


Hata wale wapenzi wa CCM wanataka akina Sita, Mwakyembe, Kilango wavuliwe uanachama!! nieleze tofauti ya CDM na CCM katika ku-deal na wanachama wake!!

unaweza ukawa umeandika wee kumbe unajieleza vizuri ni jinsi gani unavyotaka CDM kiwe kama CCM, huu ni ugonjwa mbaya sana!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom