Shibuda ageuza bunge sehemu ya mipasho!

Chadema watulie, watu kama Shibuda watakuwa wengi katika kuelekea demokrasia ya kweli. Kuhangaika nao ni kupoteza mwelekeo kwani Chama kinaweza kukumbwa na yaliyotokea kwa NCCR ya Mrema na Marando. Badala yake Chama kitende kana kwamba kinachukua ushauri wa hawa wazee "walioshindwa kuleta mabadiliko kwa miaka 50", kisha wakati mwafaka wataondoka wenyewe.

Wito ni kwa uongozi wa kweli wa Chadema kuhacha malumbano kwani wabaya ni wengi kuliko inavyoweza kudhaniwa!
 
Hawa dawa yao ni kuwa-Mubarak .........

Vinginevyo, tutahangaika sana hadi kuwabadili akili zao zilizozeeka .....

Pipo Pawaa soon itaingia. Kwa sasa hivi Tanzania, Mafuta, nyasi na kuni tayari zipo, badi CHECHE.
 
Ukweli ni kwamba huyu Bwana uwezo wake ni Mdogo sana na kwake kuongea pumba c swala lakuuliza mie since akiwa ccm alikuwa akipewa nafasi yakuchangia tu mie natune channel tofauti kwahiyo 2sitegemee point ya maana hapo simply b'coz kajiunga CDM uwezo wake ndo upo mwisho hapo cha msingi CDM waandae Mtu makini wakutake hiyo position kwa miaka ijayo.
 
ccm walimtosa akaingia chadema,keshapata ulaji wa kibunge ,je inawezekana kwa chama kumvua mtu ubunge?


Ndio inawezekana kwa kumvua uanachama wa hicho chama husika. Hivyo huyo mbunge anakosa sifa za mbunge,kwani kwa katiba yetu mbunge lazima awe mwanachama wa chama fulani cha siasa.
 
Huyu ndiye aliyesema anataka kugombea urais. Mtu ambaye anaongea kwa ngonjera za watoto wa shule atawezaje kuainisha masuala ya kiutawala ambayo yanafuata mkondo wa kisheria.
Atatuaibisha huyu
 
Cheyo na Shibuda ni vipofu waliopofushwa na sifa za wana CCM. Wasichokijua ni kwa nini tumemchagua Lema. Inabidi wajue nchi hii iko kwenye transition kutoka mikononi mwa wazee kama wao kwenda mikononi mwa vijana. wao hawawezi kuona kwa sababu era yao imekwisha ni kama mtu akifa huzikwa na kumbukumbu zake huishia pale alipokata roho. Hivi ndivyo akina Cheyo na Shibuda wanavyoona. Kwa sisi tuliowachagua akina Lema tunahitaji watu jasiri wasio na nidhamu ya woga bali kizazi kama kile kilicholeta mageuzi Tunisia na Misri. Sisi tuliomchagua Lema tunaelewa tunachotaka, tunataka era yetu itakayokuwa na mabadiliko ya kweli na waelewe tutasonga mbele kwani tunaona kuna fursa ya kuleta mabadiliko kwa kuwa tuna mawazo mbadala na siyo ya mgando kama Cheyo na shibuda na wengine. tutakapofika hatua ya kufanikiwa naomba Mungu awaweke hai wakati huo wazinduke waone na wajiunge kama walivyojiunga wazee kule Misri. Vijana ndo chachu ya maendeleo,tunasonga mbele kwa spidi, hatutishwi na wala hatutatikisika na vibweka vyao vya kutafuta upendeleo wa kugawiwa chumvi chakavu na CCM.

G.Lema songa mbele , we know you can lead and take us to the destiny that most of us are highly expecting.
we Trust you, we believe in your confidence, wisdom, unswayed leadership and we pray that God will fight for you all the way.

Tuko nyuma yako kamanda na Mbunge wetu.
 
Unajua huyu jamaa alikua anaimba mashairi kiukweli si utani, sasa kukoti the whole content ni vigumu. Shibuda ameponda sana CDM, anadai hawana hili wala lile na kwamba yeye anauasili wa sisiem naamegundua kuwa upinzani hamna kitu baada ya kuingia CDM, na kwamba kutoka CCM alianguka kwa bahati mbaya.

tatizo lako una ashumu kuwa wote tumesikiliza bunge. unatakiwa utoe mada na ufafanuzi.
 
ccm walimtosa akaingia chadema,keshapata ulaji wa kibunge ,je inawezekana kwa chama kumvua mtu ubunge?

ni rahisi tu. Akifukuzwa uanachama wa chadema automatically amevuliwa ubunge, coz huwezi kuwa mbunge kama si mwanachama wa chama chochote. Ndio maana mrema alipoondoka nccr alipoteza ubunge wake wa temeke.
 
Unajua huyu jamaa alikua anaimba mashairi kiukweli si utani, sasa kukoti the whole content ni vigumu. Shibuda ameponda sana CDM, anadai hawana hili wala lile na kwamba yeye anauasili wa sisiem naamegundua kuwa upinzani hamna kitu baada ya kuingia CDM, na kwamba kutoka CCM alianguka kwa bahati mbaya.

Hivi ni kweli alisema hayo? Kama ndivyo nasubiria kusikia kesho kafukuzwa CDM.
 
tuache longolongo,tuanzishe moment,serikali ing'oke madarakani.Maisha yamekuwa magumu huku bunge likiendelea kupiga soga mjengoni

acha uchochezi usiokuwa na maana. kwanza nahisi wewe wala haushi ndani ya TZ. Tanzania tunaenda kwa term kwa unataka madaraka subiri 2015.
Hivi zambia baada ya UNIP ya Kaunda madarakani, au Banda wa malawi, au Moi wa Kenya kuna nini cha maana walichofanya walioshinda uchaguzi hadi leo zaidi ya rushwa na kudidimiza uchumi.

Sasa sisi watanzania utamaduni umejengeka kwa uchaguzi kila baada ya miaka mitano na sasa awamu nne zimefika wewe bado una mawazo ya mapinduzi badala ya kufikiria uchaguzi ujao tufanye labda chama tofauti kiingie madarakani au magufuri-lowassa-agombee kupitia ccm.
 
Baada ya kuongea shibuda alifutiwa na cheyo, na bunge likamaliza session yake ya jioni, tafakari walichoongea wote kina msg gani, angalia mpangilio huo, tia akili.
 
huyu mama ni spika mzuri tu ila wakati mwingine anauma na kuweka uccm kiasi, ndiyo siasa zenyewe
 
Umri wa m2 ktk maisha c jambo la mcngi angalia akili yake hawajui hao shibuku na cheni coz 2shachoka habari za wazee tatizo la umeme litabaki history ndio sentesi wanayotaka waige vijana labda
 
Vijana wajifuze na kufata ya wazee hata kama wanasema "wanafunzi wanapata mimba kwa ajili ya kiherehere chao"

Vijana wajifuze na kufata ya wazee hata kama wanasema "mimi sio waziri wa mvua"


Vijana wajifuze na kufata ya wazee hata kama wanasema " sitapenda kupeleka kesi za rushwa mahakamani zinazowahusu vigogo wa serikali kwa sababu rais JK amenikataza na anawakingia kifua.


Vijana wajifuze na kufata ya wazee hata kama wanasema "CCM inaongoza na itaongoza milele"


Vijana wajifuze na kufata ya wazee hata kama wanasema "siitaji kura za wafanyakazi"


Vijana wajifuze na kufata ya wazee hata kama wanasema "CCM haina haja ya kukaa katika meza ya mazungumzo na CHADEMA kuhusiana na uchaguzi wa umeya Arusha mjini"
 
Alianza kwa kushukuru kama kawaida lakini baadae ni kama alikuwa mshahiri hivi kwa jinsi alivyokuwa akiongea mpaka kengele inagonga akaomba aendelee kama wabunge wataridhia.
Kiujumla siwezi kumquote accurate lakini alikuwa kama mahoka kwa jinsi alivyokuwa akichangia hoja bila mwelekeo. Haaaaah Shibuda ukiendelea hivi sijui kama utafika mbali?

Shibuda elimu yake ni ndogo sana-form four failure, alikuwa anaongea kwa kuimba ngonjera ambayo hata huwezi elewa anaongea na kumanisha nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom