Shibuda ageuza bunge sehemu ya mipasho!

Wadai ujana wao utawapeleka pabaya. Wakae watulie, na wajifunze kwa wazee.

Mkuu KakaJambazi mbona unatoa Hoja as if kila mtu ameshasikia ama anafahamu unachotaka kuongea plz hebu leta habari kwa urefu wake asa if unawaabarisha watu wasiosikia, wewe ni mkongwe humu
 
Shibuda ameanza kwa kusema anampongeza swahiba wake mkubwa Dkt.JK baadaye akasema anawapongeza wana CCM kwa kumpa kura.Aliunga na kushuka mashairi kwamba,vijana hawana adabu, wanajifanya wanajua na wanadharau wazee.Ameongeza kwamba, aliyoyaona ndani ya upinzani ni kwamba, hawna dira, ni wavurugu tupu, wanaopinga kila kitu.Kwa ujumla ameonekana kutokuwa muumini wa yale wayafanyayo CDM.Muda wote alikuwa akishangiliwa na wabunge wa CCM na baadaye Mzee Mapesa alimpongeza Shibuda huku akiiponda Chadema vibaya
 
Wakuu wanachotaka CCM wanaelekea kufanikiwa, tunaimba nyimbo wanazotaka, eti itakadi zisiwepo utaifa mbele,wakuu itikadi si mbaya kama inavyoanza kutafisiriwa ila itakadi inayojali maslahi binafsi, itikadi zitakuwepo tu na chama kikipendwa maana yake itikadi yao imependwa pia. Wote walio bungeni ni wanasiasa, siasa iachwe vp?

Siasa ni nini kama haina maana? Nahisi wabunge wa cdm kuwa wanyonge na kuanza kuimba nyimbo zile zile na ccm. Misimamo ya cdm ni tishio kubwa na hata rais juz amekiri,naomba cdm wasilee cancer kama shibuda yale maneno leo ni machafu mno, nipo mbali na natumia simu, nikitulia nitaandika zaidi mwelekeo wa malengo mema ya cdm na jinsi mambo yalivyo na inavyoelekea kuwa.

Tuendelee kusimamia tunachoamini,tusipotezwe na kuhisi cdm wanakosea.
 
CCM leo watalala usingizi mnono,Shibuda ameonesha wazi ama kapewa fedha chafu acahfue CDM na kwa kweli kafanya.Kilichojitokeza leo bungeni ni sawa na kusema Shibuda hayuko CDM. Amewaponda sana vijana huku akisema kwamba, si lolote watulie wawe na heshima kwani wanaendeshwa na hisia tu. Pia amesema kwamba, CDM inaburuzwa na mtu mmoja na yey hayuko tayari.

For sure we need more reaction, hali si nzuri. Mamluki wamevamia kambi
 
Baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa Katibu wa wabunge wa CDM John Mnyika aliomba wabunge wote wakutane.Nadhani suala la Shibuda litakuwa linajadiliwa.To me Shibuda ni wa kusimamishwa ubunge na kama ikiwezekana Kamati Kuu ya CDM imtimue mara moja.Kwa kilichojitokeza leo bungeni ni fedheha kubwa.Shibuda ni makapi na hafai kuwa ndani ya CDM
Ni kweli huku akijua kuwa nguzo kubwa ya CDM ni vijana amewaponda wabunge vijana kuwa wawe na busara na kuwa wazee ni hazina, yaani hata nimeshindwa kuwa specific ya yale aliongea lakini kwa tuliomuona amefuka Moshi sana.
 
Ole wao CHADEMA wakiyapokea makapi haya...Rev Kishoka amewahi kusikika akiwaasa kupitia jamvi hili.
 
maneno ya shibuda ni machafu mno,imenishtua mno kuwa mtu kama huyu imekuwaje cdm hawakumjua mapema,wasipomfukuza mara moja ni hatari sana,shibuda jina la cdm limembeba sana,inashangaza maneno yale bungeni.jamani hiyo nidhamu anayosema shibuda kuwa vijana hatuna ndio hiyo anayotufundisha kubwabwaja kimipasho bungeni ukikiponda chama chako! Cdm wasipomfukuza haraka sana itashangaza sana,hakuna cha kutaka radhi wala maelezo wacha cdm wapoteze jimbo lakini walinde heshima yao na misimamo yao.
 
Baada ya kusikiliza michango ya Vullu, Shibuda na John Cheyo, leo jioni nimekata tamaa na Bunge la 10, hakuna kitu pale ni usanii mtupu. Ni Bunge lenye kutia aibu, hakuna zaidi ya vijembe kwa CDM.

Inasikitisha saana, wabunge wa Bara wanacheza ngoma inayopigwa ng'ambo ya pili, wanatelkeza jukumu lao la msingi kupigania maslahi ya wapigakura wao, kule kuna Baraza la Wawakilishi, linajadili maslahi ya watu wao, huku kina Shibuda na Cheyo wanageuza Bunge sehemu ya mizaha badala ya kujikita kwenye masuala yenye tija kwa waliowatuma pale.

Kwa michango ya leo nimepoteza imani na hilo Bunge.

Wakati umefika kwa Watanganyika kuingia barabarani. Tunisia na Misri wameweza, nasi tunaweza.
 
Kwa iyo vijana wajifunze kwa wazee hata kama wazee haohao wanafanya upuuzi na upumbavu??
Hakuna mzee karne hii, wazee haohao ndo wanalipeleka taifa pabaya. Hakika nasisitiza hapo Bungeni kila mmoja kaingia kwa vigezo halali na hukuna relation ya baba kwa mtoto, wabunge wote ni sawa na atakayekosea anapaswa kuambiwa ukweli bila kuzingatia ni bibi, baba, shangazi wala mzee.
Busara haitambuliwi kwa uzee bali ni kwa matendo mema na yenye nia njema ya kujenga taifa.
 
maneno ya shibuda ni machafu mno,imenishtua mno kuwa mtu kama huyu imekuwaje cdm hawakumjua mapema,wasipomfukuza mara moja ni hatari sana,shibuda jina la cdm limembeba sana,inashangaza maneno yale bungeni.jamani hiyo nidhamu anayosema shibuda kuwa vijana hatuna ndio hiyo anayotufundisha kubwabwaja kimipasho bungeni ukikiponda chama chako! Cdm wasipomfukuza haraka sana itashangaza sana,hakuna cha kutaka radhi wala maelezo wacha cdm wapoteze jimbo lakini walinde heshima yao na misimamo yao.
Wamfukuze tu, wasingekuwa vijana wala asingepata ushindi,na angegombea kupitia chama tofauti na CHADEMA leo hii hasingekuwa bungeni. Wamuondoe haraka la sivyo atakiua chama.
 
Huyu mh anafanya anachokijua na kama alienda shule ya anachokifanya alifaulu kwa alama za juu sana, take it from me. CDM wanatakiwa wajue wanafanya nini wakiwa na wabunge wa aina hiyo ya shibuda, tena watulie kwelikweli.

Kuna ujinga waotaka kuuingiza hapo bungeni ambao unatakiwa ukemewe tena mapema. Wabunge wa upinzani (hasa vijana), kuchangia kwa kuonyesha failure za serikali ati ni kukosa heshima kwa wakubwa wazee, ambao kwa bahati mbaya wengi ni viongozi serikalini (mawaziri). Kama mtu ni mtumishi wa wananchi amefail kudeliver kwenye kazi yake halafu anataka sympath kwa kutumia umri wake, ukubwa-uzee (huu ni utamaduni mpya) nina hakika mpaka miaka 100 tutakuwa hivi tulivyo.

Pendekezo langu yule ambaye anadhani kashindwa na anahitaji kuheshimiwa akae pembeni, aachane na utumishi wa umma. Akishindwa kazi na akang'ang'ania kubaika ambiwe alivyo shindwa kazi hata kama ataona kuwa kavunjiwa heshima. Nawaomba waotuwakilisha wasijeingia kwenye mtego huo kwani kufanya hivyo, in this generation, kutakua ni kifo chao kisiasa.
 
shibuda is a waste of time, amepewa nafasi ya kuchangia hajachangia chcochote mpaka wakina chilagati wakawa wanamshangaaa
sorry shibuda sio chadema

hata cheyo ametumia kadi ya uzee
mimi nawashauri vijana wabunge kazeni buti
maswali mazuri yameulizwa na vijana kama umeme nk lakini wazee ilikuwa nashukuru nashukuru nashukuru
 
Ametoa angalizo kwa Wabunge Vijana kujifunza kwa Wabunge waliodumu kwenye siasa muda mrefu, amewaonya kuwa kama hawatafanya na kuendelea na wayafanyayo sasa wataishia kuwa Wabunge wa miaka 5 tu na kisha kupotea kwenye ulingo wa siasa.
 
Baada ya kusikiliza kilichotokea jana bungeni baada ya mh.Lema kutaka mwongozo toka kwa spika nimekuwa nikijiuliza, mbona hakumjibu kwa kumpa muongozo na badala yake kuanza kuanza kusema bunge limeanza kukosa adabu?Hili wadu mnalionaje.
Kwakweli kwa staili hii ya u-spika tutamkumbuka sana S.S
 
CCM na viongozi wazee wamezoea kuuenzi ule usemi usemao
Funika kombe mwanaharabu atie.
Maana yake udhaifu walio nao tuuvumilie tu mradi tunalinda heshima yake.

Viongozi wazee waelewe kuwa wanachofanya wabunge vijana ndio kizazi cha leo na tunachotaka utandawazi si kufunika kombe mwana haramu apite.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom