Shibuda aachiwa na Polisi na kusema "CCM wamenipa Umaarufu"

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Mgombea Ubunge wa Chadema jimbo la Maswa Magharibi John Shibuda ameachiwa huru na kusema kuwa kukamatwa huko na kuwekwa ndani kumempatia umaarufu hivyo atashinda.
 
Mkuu weka source hapa, maana wiki la mwisho hili kuna kila aina ya propaganda. Kama ameachiwa basi tusherehekee ushindi.
 
ama kweli mwisho wao umefika, Mungu Mkubwa, harakati hizi hazitakoma mpaka kieleweke, Tanzania Bila CCM inawezekana.
 
Karibu mtani Shibuda aka MANDELA, hawa mabwege safari hii wanakwena chini tuuuuuuuuuuuu.
 
Shibuda Magalle ccm mnaye Kamanda huyu

shibuda%20jela.jpg
 
Wooow...at last!
Wote tunafurahia kuachiwa huru kwako, na kweli sasa hivi umeongezeka umaarufu sana kutokana na kosa la ccM na polisi wao kukuweka ndani wakati hukuwepo eneo la tukio!
Naamini kuwautashinda, maana jina lako limetajwa zaidi kipindi hiki, na wengine wamekujua kupitia kosa hilo la ccM!
TUNAKUTAKIA MAFANIKIO, TUNAKUHITAJI!
 
Mongoiwe,

Fanyia kazi ushauri wa dictator, tupe source mapema tugonge glasi za furaha
 
hahaaaa mi nataka haya matukio yote uchaguzi ukiisha nitengeneza documentary flani hivi nije niuze nikiwa mzee nimestaafu
 
Mongoiwe,

Fanyia kazi ushauri wa dictator, tupe source mapema tugonge glasi za furaha

Msiwe na wasi nimeongea na Katulanda yule mpiganaji mwandishi wa Mwananchi ambaye anafuatilia suala hili, anasema amezungumza naye kwa simu na amethibitisha kuachia. nami mliponitaka kuweka Source nilijaribu kumpigia na kuzungumza naye akanieleza kuwa yuko nje na sasa anajipanga kuangalia Kampeni zake ili aweze kupita kila eneo katika jimbo.
 
Mkuu weka source hapa, maana wiki la mwisho hili kuna kila aina ya propaganda. Kama ameachiwa basi tusherehekee ushindi.
Mkuu DICTATOR, ni kweli Kamanda Shibuda ameachiwa kutoka mikononi mwa polisi kwa vile hakuhusika na tukio lililomfanya akamatwe. Lilikuwa ni shinikizo la viongozi wa CCM katika kutapatapa kwao. Nimeongea naye na amethibitisha hilo. Mapambano yanaendelea. Tujiandae kukabiliana na changamoto za ngwe hii ya mwisho kwani mafisadi wanakuja na hila nyingi, hawataki kung'oka kirahisi.
 
Mongoiwe,

Fanyia kazi ushauri wa dictator, tupe source mapema tugonge glasi za furaha

Nimeongea naye kwa njia ya simu ni kweli kaachiwa na sasa hivi na anaingia kwenye kikao cha ndani cha Chadema-Maswa
 
Kazi na maombi ndio msingi wa maisha ya binadamu. Ingia tena kazini mpambanaji baada ya kuruka kihunzi cha shinikizo la makamba na Riz1 wake. jk kila mti anaokamata unateleza!!
 
SHIBUDA, hawamwezi kwenye uwanja wa siasa, kwenye mdahalo, kwenye jukwaa la kitaaluma ama hata kiunjanja.
huyu mzee amatulia, anaongea kama anatania lakini ni mutu ya akili nyingi.
 
Tulisikia Ridhiwani alikuwa huko Maswa sasa imekuwaje au ameshindwa kushinikiza abaki humo lupango hadi baada ya uchaguzi....
 
Hongera Shibuda enedeleza nguvu za kumkomboa kutoka kwenye utumwa wa kifikra,kiuchumi,kijamii,waache mafisadi wajikanyage
 
Shibuda songa mbele hawa majitu wanajisumbua. Wafanyakazi tupo na chadema kwani nilienda udom kila ofisi inasifiwa chadema hakuna wa sisiem mwenye jeuri ya kusema. Furaha niliyonayo ni kubwa kwa shibuda kuachiwa. Sisiem mmelaaniwa
 
Tulisikia Ridhiwani alikuwa huko Maswa sasa imekuwaje au ameshindwa kushinikiza abaki humo lupango hadi baada ya uchaguzi....
Nasikia huyu kijana aligaragara na kulia sana kwenye msiba kuliko wafiwa, hii yote ikiwa ni janja yakutafuta huruma ya waombolezaji, waipe kura chama yake na baba yake!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom