Sheria zetu tunatungiwa na wasio wanasheria

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,821
Bunge letu ndio chombo mama cha kutunga sheria.
Lakini wengi wa wabunge hao sio wanasheria,
je hili ndilo linalotupelekea kuwa na sheria zenye wingi wa mapungufu?
 
mara nyingi Serikali inapeleka Muswada wa sheria Bungeni ukiwa tayari umeandaliwa kisomi na mabingwa wa sheria pale wizara ya katiba na sheria kwa ushirikiano na ofisi ya mwanasheria mkuu na kwa kupewa mwongozo wakitaaluma kutoka katika taaluma husika inayotungiwa sheria, mfano sheria ya wanyamapori,ni lazima kuwe na kamati ya wanataaluma hiyo ambao wao wataclear all doubts za kisomi ndani ya fani husika, na kamati hiyo ya kitaaluma/technical staff inakutanaga na wadau wa sekta husika kupata maoni yao, kisha muswada huo ukiishakupitiwa na mkundi yote ndio hupelekwa kwenda kupitishwa na wabunge, kwa ujumla ofisi ya mwanasheria mkuu ndo inapaswa kuwajibika kama sheria husika hakukidhi haja, na hapo wabunge watasema walipotoshwa na ofisi hiyo, kama ambavyo Chenge anavyolaumiwa leo.
 
Bunge letu ndio chombo mama cha kutunga sheria.
Lakini wengi wa wabunge hao sio wanasheria,
je hili ndilo linalotupelekea kuwa na sheria zenye wingi wa mapungufu?
hivi ni lazima WABUNGE WOTE WAWE LAWYERS?
 
Bunge letu ndio chombo mama cha kutunga sheria.
Lakini wengi wa wabunge hao sio wanasheria,
je hili ndilo linalotupelekea kuwa na sheria zenye wingi wa mapungufu?

Kwa hiyo ni mabunge mangapi unayo yajua wewe yamejaa wanasheria? Na je una shauri sifa moja wapo ya kuwa mbunge ni kuwa mwanasheria? Kazi ya mwanasheria siyo kutunga sheria bali kutumia sheria ambazo tayari zipo.
 
Back
Top Bottom