Ninayo shida kidogo ndugu zangu kulingana na Sheria kuhusu Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu. Nahitaji kufahamu kwamba; Je mwanafunzi anayo haki ya kuishitaki Bodi pale inapokuwa imechelewesha kumpatia mkopo (fedha) kwawakati kama inavyotakiwa wakati mi mnufaika wa mkopo.?Na kama anaweza kushitaki anaweza kuomba fidia za gharama ambazo amezipata kutokana na kucheleweshwa kwa mkopo (fedha) hizo kutoka Bodi?