Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,583
Kwa sababu watu waliopendana ni ngumu kuchukiana. Sheria inawapa nafasi ya kujifikiria. Unless ndoa hiyo iwe ilikuwa ya mkeka. But if there was love, sheria imeona possibility of reconcilling ipo. Na tuna ushaidi wa watu ambao wameweza kuyashinda majaribu ya ndoa na sasa ndoa zao ni mifano ya kuigwa.
Hiyo nafasi ya kufikiria maamuzi inaitwa "cooling-off period". Kwa Tanzania sijui kama ipo kwenye sheria za talaka. Lakini kwa nchi kama Marekani majimbo mengi yana hicho kipengele cha "cooling-off period" kwa sababu hiyo hiyo uliyoitaja wewe. Kawaida huo muda wa kufikiria huwa ni wa siku tisini (90) ila inategemea na jimbo lenyewe.
Kwa hiyo si kwa vile tu wana no-fault divorce law(s) basi inamaanisha ukienda kuomba talaka leo basi ni kesho yake tu unapata decree. Halafu pia mkitalikiana haimaanishi kuwa hamuwezi tena kuja kuoana. Kuna watu kibao waliotalikiana na baadaye kuja kugundua kuwa walikosea na wakaoana tena.