Sheria ya mirathi yasemaje

NGUGO

Member
Apr 8, 2012
36
6
Wana sheria wa JF Salama?
Ufumbuzi wa hili ukoje?
Mwaka 1975 nilioa kwa ndoa ya kimila, bahati mbaya ndoa hiyo ilivunjika mwaka 1980 tukiwa tayari tumezaa watoto watatu. Mwaka 1986 nilipata mwenzi mwingine tukafunga ndoa kanisani, tumejaliwa kupata watoto wawili.
Tatizo linakuja kuwa mama watoto huyu mpya anadai hawatambui hao wanangu wa awali na anasema hata ikitokea ikafika maswala ya urithi, wale watatu hawahusiki na mirathi.
1. Je! Sheria za mirathi zasemaje hapo wanasheria? 2. Je! Nikiamua kugawa urithi ningali hai nitakuwa nimekiuka sheria za mirathi?
 
Ndugu,

Nimesoma tatizo lako, naweza kusema yafuatayo;
1. Wewe ndiye nwenye KUWATAMBUA watoto wako kwanza (watoto wote 5 ni wako?)
2. Mkeo huyo wa pili MTAMBULISHE watoto wako, kwamba "huyu, huyu na huyu ni watoto wangu halali.
3. Watoto wote watano kwa kuwa ni halali watambulishe kwa ndugu zako wote, hili ni jukumu lako (sio la mwingine)
4. Waunganishe watoto wako wote ili wafahamiane vizuri
5. Mkeo, mtalaka wako, nduguyo au mtu yeyote hawana mamlaka ya kutomtambua / kutowatambua watoto wako.
6. Suala la kuridhi ni suala linaloamuliwa na mwenye kuridhisha mali zake (si vinginevyo)
7. Andika HOSIA leo hii (leo hii) na ugawe mali zako zote kwa unayemtaka (tenda wema kwa wote)
8. Wekesha hosia yako sehemu inayoaminika kama vile mahakamani au kwa ndugu unayemuamini.
9.
10.

TAMBUA
a) Ukifa sasa (sikuombei kifo - japo inawezekana), watoto wako hao watatu hawatapata kitu chochote kama hawana wakuwashughulikia au watapata baada ya muda mrefu.
b) Usiwe na mawazo mgando kwamba ukiandika hosia UTAKUFA. Ni watu makini/wanaojali wanao kuandika hosia.
c) Fuatilia suala hili - maana wanasheria wanaweza kukushauri vinginevyo au kukupa sheria ya miradhi kama ulivyoomba
 
@ngungo, msikilize na tekeleza aliyokwambia wilson mwaijage.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom