Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Sio kweli amour,,nilishaona kipindi kimoja kwenye tv yao watoto wakiwa darasani wamekaa kwenye matofali...
 
Hii sheria ni nzuri, lakini itaweza kusimamiwa ipasavyo?
Maana kuna vitengo vingi sana katiks nchi yetu vinavyohitaji usimamizi mzuri.
Ikiwa watafanikiwa katika hili basi nitawatilia shaka, kwanini hili kwanini liwezekane na mengine yenye umuhimu mkubwa yashindikane?
 
Kinachoshangaza tanzania ni woga wa kufungua kesi za kikatiba kupinga sheria za kidhalimu. Wenzetu kenya tayari wamezipinga sheria za aina hii mahakamani mara tatu na kuifanya serikali ya kenya kukaa kimya.
 
Wangeongeza sheria iwe kali zaidi, kwani watz wanavichwa vigumu sana, na ukizingatia kwamba watz ni washamba wa hii mitandao, kwa hali hiyo wanaingia kwa nguvu kubwa sana hadi wanataka wao wawe juu ya wale ambao wana miaka zaidi ya 50, na wakati huo ni mbumbumbu hata hawajui sheria zinasemaje.
 
Sheria kandamizi ni maalum kwa kuwabeba wakoloni weusi na si kwa kupunguza matumiI mabaya ya mtandao.
 
Sheri zipo ila hazifuatwi na viongozi wetu hawana ujasiri wa kufuatilia hizi kwsi za madawa ya kulevya maana nakumbuk a baba Rizz aliwahi kusema orodha UA wafanyabiasha wa madawa ya kulevya anayo lakini tunashangaa mpaka anaondoka hajawataja
 
Sheria hii imeundwa ili kudidimiza upinzani watu wasiwe na Uhuru wa maoni wa kuikosoa saeikali pale inapofanya maovu
 
Usimamizi wa serikali yetu ni mbovu ata tukiongea mambo mengi utekelezajiii mbovu lakini cha msingii tufikishe ujumbe ukweli ni kwamba mitandao iko mingi alafu inasumbua network system zao ovyo asubuhii njema wanajamii wenzangu
 
Ambae anaona hizi sheria ziko sawa kichwani ana matope (kusema hivi tayari nishavunja kipengele kimoja na naweza kwenda jela mwaka au kulipa fine isiyopungua three million).Unaona ilivyo rahisi kumfunga mtu. Siamini walikaa wabunge na wao kwa akili zao kabisa wakapitisha haya madudu. Hii ni dictatorship kabisa, sijaona HATA KIMOJA ambacho ni right kuhusu hiyo sheria, em aliyeona kipengele ambacho kinasaidia bila kukandamiza aniambie isije kua nimeruka mambo ya msingi.

Naona ni muda sasa inabidi watu tuungane kuipinga hii ifutwe kabisa au ifanyiwe marekebisho.

Ukisoma vizuri hiki kimeseji tu tayari mtu anaweza jipanga akanifunga maana hata identity tu nayotumia sio jina langu halisi.
 
MSIJALI HII SHERIA ILIPANGA KULINDA UHUNI NA UHALIFU WA WATU FULANI FULANI WA CCM NA INAPIGWA VITA NA DUNIA NZIMA, IKO KINYUME NA UHURU WA KUNENA, NA ITAFUTWA
 
Back
Top Bottom