Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Kuna haja ya kufikiri juu ya fikra tunazofikiri na kuwaza juu ya mawazo tunayowaza kabla ya kutaka mabadiliko yoyoteyale
 
ila nawaambia ukweli kuwa baba rizi hatasaini huu upuuzi , namfahamu yule raisi wetu ni mwenye akili na ni msikivu sana , sio kama hayo ma ccm fata upepo ya huko bungeni , kila kitu ushabiki tu
 
Pamoja na kuwa Kanali Muamar Gaddafi aliwapa wananchi kila kitu zikiwemo huduma za kijamii kama maji,shule,afya,umeme nk lakini alipoamua kuwanyima UHURU WA KUTOA MAONI lilikuwa ni KOSA KUBWA mpaka imefikia kulipia kwa gharama ya damu yake.
Nirejee kwenye mada yangu. Hii sheria ya makosa ya mtandao ni hatari kwa amani na utulivu wa nchi. Kuwanyima watz uhuru wa kutoa maoni yao,uhuru wa kupokea taarifa nk ni janga na ni volkano inayosubiri kulipuka,iliyomgharimu Gaddafi kwa gharama ya damu yake.
Hitimisho: wape watu kila kitu ila sio kuwanyima UHURU wa kutoa maoni na kupata taarifa,unatengeneza volkano itakayolipuka.
 
Iwapo mh.Raisi atasaini muswaada wa makosa ya mtandao na kuwa sheria,moja ya matakwa ya utekelezaji wa sheria hiyo itakuwa ni kuwataka watoa hudumu(wamiliki wa mitandao na blogs) kutoa taarifa mbalimbali za watumiaji zikiwemo taarifa za majina halisi ya watumiaji wa mitandao na blogs mbalimbali na itakuwa ni kosa,kwa mujibu wa sheria,mtoa huduma kutotoa taarifa hizo pindi zinapotakiwa.

Sasa wadau,kwa sheria hii,haya majina ya bandia(fake ID) tunayotumia yatakuwa na maana na umuhimu wake wa awali?

Sipati majibu kabisa!
 
  • Thanks
Reactions: jme
Tunakoelekea hata haya matumizi ya majina ya bandia yanaweza kabisa kufutwa na sheria hii ikafanyiwa marekebisho kwa lengo la kulazimisha matumizi ya majina halisi iwapo tutakaa kimya bila kuchukua hatu sasa.

yote yatafutwa na sasa tutakuwa kama ilivyo facebook, instagram na twitter
 
Iwapo mh.Raisi atasaini muswaada wa makosa ya mtandao na kuwa sheria,moja ya matakwa ya utekelezaji wa sheria hiyo itakuwa ni kuwataka watoa hudumu(wamiliki wa mitandao na blogs) kutoa taarifa mbalimbali za watumiaji zikiwemo taarifa za majina halisi ya watumiaji wa mitandao na blogs mbalimbali na itakuwa ni kosa,kwa mujibu wa sheria,mtoa huduma kutotoa taarifa hizo pindi zinapotakiwa.

Sasa wadau,kwa sheria hii,haya majina ya bandia(fake ID) tunayotumia yatakuwa na maana na umuhimu wake wa awali?

Sipati majibu kabisa!

Kimsingi lengo la sheria hii ni kumzuia tumbili asipate nyaraka zinazofichua ufisadi wa mlinzi wa mali ya mwenye shamba. Kwa bahati mbaya inatukumba wote. Hivi wao itawabagua kwa jinsi ilivyo general? Hata hivyo ninachojua ni kwamba Rais ataitia sahihi tu kama alivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya katiba baadaye kwa kuiridhisha chama chake akaagiza irudishwe bungeni eti ikafanyiwe marekebisho ya kupigiwa kura ya ndiyoo! Walosema ndiyo wameshinda.
 
Iwapo mh.Raisi atasaini muswaada wa makosa ya mtandao na kuwa sheria,moja ya matakwa ya utekelezaji wa sheria hiyo itakuwa ni kuwataka watoa hudumu(wamiliki wa mitandao na blogs) kutoa taarifa mbalimbali za watumiaji zikiwemo taarifa za majina halisi ya watumiaji wa mitandao na blogs mbalimbali na itakuwa ni kosa,kwa mujibu wa sheria,mtoa huduma kutotoa taarifa hizo pindi zinapotakiwa.

Sasa wadau,kwa sheria hii,haya majina ya bandia(fake ID) tunayotumia yatakuwa na maana na umuhimu wake wa awali?

Sipati majibu kabisa!

Tulijiunga na JF kabla ya majina bandia kuwa Criminalized, kwa hiyo tuko kwenye safe side as far as majina bandia yanahusika! Tatizo litakuwa kwenye content za Post zetu, tuwe makini maana adhabu za hiyo Sheria zinatisha!
 
Iwapo mh.Raisi atasaini muswaada wa makosa ya mtandao na kuwa sheria,moja ya matakwa ya utekelezaji wa sheria hiyo itakuwa ni kuwataka watoa hudumu(wamiliki wa mitandao na blogs) kutoa taarifa mbalimbali za watumiaji zikiwemo taarifa za majina halisi ya watumiaji wa mitandao na blogs mbalimbali na itakuwa ni kosa,kwa mujibu wa sheria,mtoa huduma kutotoa taarifa hizo pindi zinapotakiwa.

Sasa wadau,kwa sheria hii,haya majina ya bandia(fake ID) tunayotumia yatakuwa na maana na umuhimu wake wa awali?

Sipati majibu kabisa!

Mimi Tu Pekee Ndiyo Nadhani Nitapona Kwakuwa Natumia ID Yenye Jina Langu Halisi La GENTAMYCINE Bin MNYARWANDA. Kazi Ipo!
 
Fikra huru na mijadala yenye tija rais akisaini itakuwa imezikwa rasmi
Na hii mitandao kama JF itakosa tija na maana katika matumizi
 
Ikisainiwa hii sheria ndo kifo cha jamiii forums. Na wao wameliona hilo kwa hiyo wanapigana kufa na kupona.kuhakikisha muswada hausainiwi. Sababu ya Fake ID watu wapo huru kuongea mpaka unajiuliza hawa watu wanatokea wapi maana kwenye Facebook na Twitter hawaonekani ha ha ha
 
Back
Top Bottom