Sheria ya madai

Feb 25, 2011
5
0
Naombeni jamani msaada, kwani nimekua nikikopa kwenye tasisi flani za fedha. Nilipofikia kukopa milioni 7 waliniambia nilete kwanza milioni 5 ili kufidia sh. 1500000 iliyobakia katika mkopo uliotangulia wa milioni 3. na milioni tatu na nusu itakayobaki wataifadhi kama dhamana ya mkopo. Baada ya makubaliano nikawapelekea milioni tano. Baada ya hapo wakaenda kuangalia biashara yangu kama inaridhisha. Baadaye wakaniambia nije siku inayofuata. Nilipoenda wakaniambia biashara yangu hairidhishi kuchukua mkopo wa milioni saba, wakaniambia unastahili kuchukua milioni tano tu.. Nikawaambia wanirudishie miliono zangu tano tuanze upya mkataba wa milioni tano kwa kuwa mkataba niliosaini ni wa milioni7. Wakakataa mwishoni wanipa milioni tano kama mkopo wa kurudisha na riba. nikawaambia mi si nimewapa milioni tano sasa hizi si hela zangu? Baadaye wananifuata niwalipe tena milioni tano. Sheria inasemaje!
 
Back
Top Bottom