Sheria ya kuhasi wanaume wanaorudia kubaka yaja

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itashauri iundwe sheria ya kuhasi wanaume wanaobainika kurudia matendo ya ubakaji na ulawiti mara baada ya kupewa adhabu ya kifungo cha miaka thelathini.

Ummy%20Mwalimu.JPG

Ummy Mwalimu - Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma na waziri wa wizara hiyo Mh.Ummy Mwalimu wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika itakayofikia kilele chake kesho juni 16.

Mh. Mwalimu amewataka wazazi wasiruhusu watoto wao kulala na watu wasiokuwa wazazi wao na hawafahamiki vyema hasa ndugu kwani wameendelea kuwa chanzo cha kuwaharibu watoto kwa kuwabaka na kuwalawiti.

Aidha Mh. Ummy amesema kuwa wizara yake pamoja na ile ya katiba na sheria imekwishampelekea mwanasheria mkuu wa serikali barua ya kutaka sheria ya ndoa ya mwaka 1971 irekebishwe kwani inashawishi watoto kuolewa wakiwa wangali watoto.

Chanzo: EATV
 
watoaji mimba nao wafanyejwe, lazima tukae chini na kuangalia vyanzo vya tatizo kuweka sheria kali haisaidii sasa hivi mnaruhusu vituo vya television,redio magazeti kupromoti hayo mambo matokeo yake ndio hayo jingine ni tatizo la ajira ambalo linawafanya watu kuwa na msongo wa mawazo kiasi wanajikuta wanafanya vitendo vya aibu ukiondoa na matukio machache yanayohusisha ushirikina na ukosefu wa maadili
 
walau nawe umewakumbuka watoto wasiozaliwa bado, maana wanaongoza kuuwawa. hawawezi kujitetea au kupiga kelele. humu jukwaani wengi hawawatetei watoto hawa. kila la kher ndugu
 
Sasa hivi kila mtu anajoropokea ili aonekane ana chapa kazi. Mmemjua mtu tabia yake, kuna utaratibu gani wa kumfuatilia nyendo zake, ushauri nasaha n.k?
 
Sheria ikipitishwa kuhasi wanaume baradhuri mabazazi itapendeza sana.
Tena ingefanywa kwa kosa la kwanza pindi apatikanapo na hatia, ili mradi ibainike pasina shaka kuwa muhusika katenda kosa hilo.
Huyo shetani zikinyofolewa anakuwa amepata dawa ya umpole,uadilifu na uaminifu.
Kama enzi za watemi, mtu huyo akishafanywa towashi alipangiwa kazi ya kusinga wake za mtemi. Kazi hiyo waliifanya kwa uaminifu bila kutiliwa mashaka.
 
Back
Top Bottom