Sheria ya kudhibiti maandamano yaja

CCM wapo kwa ajili ya matumbo yao na ndugu zao tu. Msiumize vichwa kuna mwisho wao, watatajana wote siku ikifika.
 
Sheria yoyote inapotungwa kitu cha kwanza lazima iheshimu katiba ya nchi! Haya tukiangalia katiba ya nchi inasema nini kuhusu maandamano? au katiba itatenguliwa ili hiyo sheria itungwe? au wanaongelea kwenye katiba ijayo imbayo inaimbwa kila siku? au ndo kutishia nyau watu wazima? Huu uoga wawatishie hao mafala wao waoga wanaotamani amani ya uvumilivu na si amani uhuru na haki.





A friend of my enemy is my enemy too
 
Kwenye mchezo wa kandanda utajua kuwa timu imezidiwa kete pale inapoanza kucheza rafu, inapoanza kukaba mtu badala ya kukaba mpira! Kifo cha ccm na serikali yake ni pale inapoanza kutumia vitisho na /au sheria kandamizi kuwabana wapinzani; kutungwa kwa sheria ya kudhibiti maandamano kutawapa credit CDM na kuichimbia kaburi ccm na watu wake. Enyi washauri wa ccm kama mnataka chama chenu kidumu acheni kuwakaba akina Lissu kabeni mpira/hoja zao!
 
ndugu watanzania nimekuwa nafuatilia kwa karibu mambo ya chama pendwa cha Chadema. kuna mambo machache naweza kuyasemea ambayo yanaweza kuja kuwa neema kwa watanzania huko mbeleni. ukipita kila mahala ukisema chadema unaonekana unaelekea kuongea point kw kuwa imejengeka sifa miongoni mwa watanzania kuwa ndo chama ambacho kinaweza kuleta neema kwa watanzania. mimi mwenyewe nimewafananisha wanaharakati wa chadema na the late Martin luther king JR. huyu jamaa aliongea speech ya I have dream ambayo iligusa maisha ya wenzetu .wiki hii nimefuatilia kwa karibu speech ziizotolewa bungeni kwa maoni yangu kama watawala hawatajenga mazoea ya kuchukua maoni ya upinzani kuna jambo ambalo laweza kuja tokea huko mbeleni ambalo litakuwa kwa manufaa ya wapenda haki. chondechonde mambo yanayosemwa yapo usiyapuuze kwani ni ya msingi na ndio yanayowagusa watanzania wengi. mwisho nasema nina matumaini kuwa iko siku CHADEMA watatawa hii Tanzania yetu na ndio itakuwa mwisho wa dhuluma na rushwa its my hope justice will preveil.that is what we Expect long live Chadema Long Live Tanzania
 
Mwanzoni alikuwa akijitambulisha kama Judge na kuwa hana chama lakini siku zimepita sasa amekuwa kada wa magamba AG hoovyoooooo!!!!!!!!
 
Tanzania nchi yetu kwa sasa inapitia kipindi kigumu sana kisiasa na kiuchumi. Serikali liyoko madarakani chini ya uongozi wa Chama Cha Magamba-CCM imepoteza mwelekeo wa kuongoza nchi.

Mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kuonekana kwamba CCM wamepoteza mvuto kwa Watanzania kutoka 80% mwaka 2005 mpaka 60%! Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kilionekana kutoa upinzani mkali na kuchukua karibu majimbo yote muhimu katika Majiji na Miji mikuu ya Mikoa. Matokeo haya yamewatia kiwewe CCM na serikali yake.

Tunachoshuhudia sasa ni juhudu na bidii ya Serikali ya CCM kutaka KUBADILISHA SHERIA,KANUNI,TARATIBU NA MIFUMO mingi mingine ya kiutendaji ILI KUWAKABILI au kwa lugha nyepesi KUWADHIBITI CHADEMA ili wasifurukute maana wanaonekana kutishia MASLAHI YA CHAMA TAWALA NA SERIKALI YAKE.
  • Tumeshuhudia mapema kabisa mara tu ya Bunge kuanza KANUNI NA TARATIBU ZA BUNGE ZIKIBADILISHWA ili kuwadhibiti CDM. Tuliona jinsi serikali ilivyokuja na hoja ya KUBADILISHA KANUNI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI.
  • Tumeshuhudia HOJA YA CHADEMA YA KUTAKA KATIBA MPYA ikitekwa na CCM kwa HILA ili waweze kuichakachua na hatimaye waje na KATIBA MPYA FEKI ambayo itaendelea kulinda maslahi ya watawala na serikali yao ya MAFISADI.
  • Tumeshuhudia KANUNI FULANI FULANI naTARATIBU ZA BUNGE zikikiukwa MAKUSUDI ili kuwadhibiti CDM. Hoja nyingi za CDM kutoka kwa WABUNGE MAKINI wa CDM zimezimwa au kukaliwa makusudi bila ya kutolewa maelezo ya kina HATA BAADA YA SPIKA kuomba ushahidi wa maandishi toka kwa wabunge husika. Mifano hai ni HOJA YA MHE. GODBLESS LEMA YA KUMWAMBIA WAZIRI MKUU PINDA KUSEMA UONGO BUNGENI kuhusu mauaji ya Arusha.
  • Tumeshuhudia Wabunge wa CDM na kambi yote ya upinzani wakizuiwa na SPIKA MAKINDA KUULIZA MASWALI YA PAPO KWA PAPO KWA WAZIRI MKUU.
  • Tumeshuhudia POLISI WAKIKIUKA SHERIA YA KUKAMATA NA KUWATIA WATU MAHABUSU BILA KUJALI HAKI ZA WAHUSIKA hasa WABUNGE WA CDM. Mifano kama Mhe. Mbilinyi a.k.a Mr.Sugu-MB wa Jiji la Mbeya,Mhe.Tundu Lissu-MB na MNADHIMU wa KUB akitiwa ndani huko Tarime,Waheshimiwa Mbowe-MB wa HAI na Kiongozi wa KUB na Mhe. G.Lema MB wa A Town wakiwekwa ndani huko Arusha kufuatia vurugu za Polisi na mauaji ya watu wasio na hatia.
Kama haya hayatoshi juzi Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Magamba amesema Bungeni kuwa kuna MPANGO WA KUBADILISHA SHERIA YA MAANDAMANO ili kuwazuia CDM wasiendelee KUANDAMANA!!!! Huu ni ukiukwaji wa HAKI ZA BINADAMU kwa sababu maandamano ni haki ya kila Mtanzania.

Hapa ndipo unapogundua kuwa Serikali ya CCM haiko makini katika kufanya mambo yake.Kwa maana nyingine haina washauri wazuri wa kuishauri serikali hususan katika nyaja ya siasa. Kwa mtu makini anaweza kugundua kuwa hawa CCM wanafikiri wataitawala TZ milele na hata siku moja hawataondoka madarakani. Maana kama mtu una mtazamo wa mbele kuwa kuna leo na kesho, huwezi kutunga sheria ambayo kuna siku na wewe sheria hiyo hiyo itakurudi. Mfano tuseme kuwa siku CDM wakishika uongozi wa nchi ina maana CCM nao hawataruhusiwa kuandamana wakiwa kama wapinzani. Huu ni ujinga na uvivu mkubwa sana wa kufikiri.

Haiwezekani kila siku viongozi wa CCM wanakaa kufikiria ni sheria gani itawadhibiti CDM badala ya kukaa na kufikiria NAMNA WATAKAVYO WEZA KUTATUA MATATIZO YA WA-TZ ukiwemo UMASKINI wa kutupwa na UKOSEFU WA NISHATI MUHIMU YA UMEME! Huu ni upuuzi wa karne kwamba Mawaziri wetu wanafikiria namna ya KUPATA PESA YA KUWAHINGA WABUNGE ILI WAPITISHE BAJETI FEKI YA WIZARA FULANI KWASABABU WANAJUA NI YA UONGO NA ISIYOTEKELEZEKA.

Mimi namaliza kwa kuuliza hivi: TUMESHUHUDIA WABUNGE WENGI WA CCM WAKIONEKANA KULALA FOFOFO BUNGENI na kila wakiguswa wanadai ni UCHOCHEZI WA magazeti! Sasa Je, KWANINI SPIKA MAKINDA NA WABUNGE WAKE WA CCM HAWATAKI KUTUNGA SHERIA YA KUWATOA NJE WABUINGE WANAOLALA BUNGENI MAANA WANAKUWA WAMESHINDWA KUWAWAKILISHA WAPIGA KURA WAO. Haiwezekani hata kidogo mbunge aliyelala aseme anatafakari. Maana anakuwa hajasikia kilichosemwa na mchangiaji anayetoa mchango wake au hoja!

Napendekeza Wabunge wa Upinzani watoe hoja ya kutaka MBUNGE ANAYELALA ANATAKIWA ATOLEWE NJE YA UKUMBI WA MKUTANO AKISINDIKIZWA NA ASKARI na ARUDISHE POSHO YA SIKU HIYO MAANA NI SAWA YULE AMBAYE HAKUHUDHURIA KIKAO CHA BUNGE.
Naomba WABUNGE wote wa upinzani wapinge kwa nguvu zote mpango wowote wa AG WEREMA wa KUTAKA KUFUTA SHERIA YA MAANDAMANO.

Nawasilisha.


 
Hiyo sheria na ije tu, lakini waambieni kabisa kwamba hiyo mitaa ya masaki na o'bey hakuna mtu atalala usingizi . wote tutakesha na milio ya bunduki, waagize risasi nyingi sana badala ya pembejeo za kilimo.
 
Mfa maji aachi kutapatapa. Kama ulivyosema kwa usahihi kabisa nchi yetu imepoteza dira; chama tawala kimemeguka katika vipande vipande vivyoumana kama panzi. Huko serikalini hali siyo tofauti, kila mtu anasema lake; juzi alisikika mkurugenzi wa Takukuru akisema jarada la kesi ya Chenge tayari liko kwa DPP, naye DPP akakana habari hizo hadharani. Usanii huo ni ushahidi tosha unaodhihirisha ni kwa kiwango gani viongozi wa idara hizo nyeti wasivyokuwa makini katika kazi zao bali wamegeuka kuwa wanasiasa. Kama hiyo haitoshi hata baraza la mawazirihalifanyi kazi zake kama kitu kimoja; juzi Membe aliliambia bunge wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya kuwa serikali iko kwenye mchakato wa kuruhusu uraia wa nchi mbili, siku chache baadaye waziri mwenye dhamana ya uraia akakana kuwepo kwa mpango huo. Aidha hivi majuzi mwanasheria wa serikalui akitoa taarifa rasimi ya serikali alisema mahakimu wa wilaya wameteuliwa kuwa "makrona" ili kuwa wanachunguza mauaji yanavyotokea katika mazingira yenye utata, siku hiyo hiyo waziri wa mambo ya ndani yeye alisema uchunguzi wa mauaji ya aina hiyo unafanywa na polisi na taarifa inapelekwa kwa DPP kwa hatua zaidi. Ukizingatia vurungu machi iliyopo katika uendeshaji wa nchi ambayo haya matukio niliyoyataja ni kiashirio inaonekana wazi ya kuwa kuna haja kubwa ya kushinikiza kuwepo kwa mageuzi. Hali hiyo haiwezi kuzuiwa eti kwa kudhibiti maandamano, kinyume chake udhibiti wa aina hiyo unaweza kuharakisha uwepo wa mageuzi
 
Kutokana na fack za hapo juu kwanini magamba msituachie nchi yetu kwa amani?au mwataka damu imwagike ndo mwamini tumewachoka
 
Back
Top Bottom