Sheria ya kudhibiti maandamano yaja

Kama hiyo sheria itapita,basi hakuna sababu ya kuwa na BUNGE,HAKUNA SABABU YA KUWA NA VYAMA VYA SIASA,HAKUNA SABABU YA KUWA NA VYAMA VYA KIRAIA,NA ITAMKWE WAZ KUWA NCHI HII HAINA UTAWALA WA SHERIA,DEMOKRASIA ITABAKWA KAMA KATIKA UTAWALA WA KIIMLA HUKO ULAYA MIAKA YA 1600

Wanajaribu kila njia kuhakikisha wananchi wanakosa haki yao ya kisheria ya kuandamana. kimsingi sioni maandamano yakitumika vibaya ila sasa ni kutokana na kwamba mambo yamewazidia serikali na wanaona wakati umefika wa kuzima kasi ya wapinzani.

Basi tuwekee link,,,,,tusome habar yote,,,,,maana yeye chanzo chake cha habar ni mwananch,nami chanzo changu ni JAMIIFORUMS
Chanzo chako cha Habari Gani tena wakati hata Heading ni Ya Gazeti la Mwananchi la Leo!Sema Source Mwananchi

Ukiona taifa linazidi kuongeza sheria na kuminya haki za watu wake,basi ni dalili na ishara ya anguko la taifa husika,anachosema Werema ni mwendawazimu pekee anayeweza kutoa mawazo kama hayo.Kwa kadri watakavyominya uhuru wwetu ndivyo chuki dhidi yao itakavyoongezeka,na watawala hawataki kuambiwa ukweli eti lugha kali,hakika ukweli na haki vitashinda

Nanyaro thats critical thinking.Serikali yetu inaumwa ugonjwa wa kutokufikiria!anguko laja soon tu!

Sheria ya kudhibiti maandamano yaja Send to a friend
Friday, 29 July 2011 22:38
0diggsdigg

MAHAKAMA ZA KORONA KUTUMIKA KUCHUNGUZA MAUAJI TATA YA RAIA
Neville Meena na Habel Chidawali,Dodoma
KAULI za kuendelea na maandamamo mpaka kieleweke ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa Chadema zinaonekana kuikera Serikali na sasa inakusudia kuifanyia marekebisho sheria husika ili kuyadhibiti.Maandamano ni miongoni mwa mambo ambayo yalitawala mjadala wa siku mbili bungeni wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, iliyowasilishwa juzi na Waziri Shamsi Vuai Nahodha.

Akichangia hotuba hiyo jana kabla ya kuahirishwa kwa Bunge kwa ajili ya mapumziko, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema mabadiliko hayo ya sheria yatalenga kuzuia bughudha katika maeneo ambayo watu hawashiriki maandamano husika.

"Tunadhani kuna haja ya kurekebisha sheria ili kuregulate (kudhibiti) maandamano katika maeneo ambayo watu si washiriki wa maandamano hayo, hili linawezekana maana nchi kama Ujerumani wamefanya hili," alisema Werema na kuongeza:

"Nimesikia hapa kauli mbalimbali zinazohamasisha maandamano na wengine wanasema tutaandamana mpaka kieleweke na wengine wanasema kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam, tunasema ndiyo ni haki ya kisheria, lakini lazima tuzingatie kwamba wapo wasiopenda maandamano haya."

Kadhalika, Werema alitumia nafasi hiyo kutoa somo kwa wabunge kuhusu mivutano iliyotokea bungeni siku chache zilizopita: “Peaneni nafasi kwa kila mtu na mwenzake na muwe na ushirikiano kama ambavyo mikono ya kushoto na kulia inakuwa na ushirikiano mzuri.”

Jaji Werema aliwaambia wabunge kuwa kazi ya kuwakilisha wananchi inahitaji uvumilivu kuliko kazi nyingine na akawataka wabunge wa pande zote kutumia lugha za kistaarabu wanapo kuwa ndani ya ukumbi wa bunge.

Hata hivyo, alikemea tabia za baadhi ya wabunge kutumia lugha za maneno makali akitolea mfano wa hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi... “Ni kweli Mheshimiwa Lema (Godbless) alitumia lugha kali kidogo.
Hapa naomba ifahamike hivyo, lakini yote mimi ambaye ni Mwanasheria wa Serikali nasema muendelee kuvumiliana na kuangalia lugha za kutumia. Namshukuru sana Mheshimiwa Lukuvi (William), katika hotuba ile alitaka kusimama amzuie Lema, lakini nikamwabia muache aendelee kwani kuna njia nyingi za kuzungumzia hivyo akimaliza utaomba mwongozo.’’

Alisema kuwa katika suala lile yeye (Werema) akiwa Mwanasheria Mkuu, ndiye mwenye dhamana ya kulisemea jambo hilo.

Kauli za Wabunge wa Chadema
Wabunge wengi wa Chadema katika kuchangia hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi walisisitiza kwamba maandamano lazima yafanyike ili kudai haki ambazo zimekuwa zikiminywa na Serikali kwa kutumia vyombo vyake vya dola.

Mbunge wa Nyamagana, Highness Kiwia alisema kwake maandamano ni sawa na "mama na baba wa ubunge" wake akidai kwamba kama si maandamano asingetangazwa kuwa mshindi wa nafasi yake hiyo.

"Nataka mtambue kuwa bila ya maandamano, mimi Kiwia nisingetangazwa na kuwa mbunge maana hali ilikuwa ni mbaya kuliko mnavyofikiri na ndiyo maana mkitaja maandamano napata tabu sana kwa kuwa nayaona maandamano sawa na baba na mama," alisema Kiwia.

Mbunge huyo alisema kuwa maandamano ya Chadema yanawaamsha Watanzania kutoka katika usingizi mzito wa kuibiwa kwa rasilimali ya nchi ambayo kila siku wanadangwa na amani.

“Hata hayati Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) aliwahi kusema, ufisadi na rushwa wakati wa amani ni adui mkubwa kuliko wakati wa vita na hiyo ilikuwa ni hotuba ya Nyerere ya mwaka 1965 katika Bunge la Bajeti, sasa nasema haki ya mama lazima kupiga kelele hadi kieleweke."

"Wakati naingia katika chumba cha kujumlishia kura saa 1:00 jioni mwaka 2010, niliingia nikiwa mbunge tayari maana utaratibu wa kuweka matokeo vituoni ulikuwa ukinihakikishia hilo, lakini siku ya kwanza ilishindikana na siku ya pili wananchi wa Ilemela, (Mwanza) waliamua kuandamana kushinikiza mbunge wao atangazwe."

Kwa upande wake, Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje alisema kuwa yuko tayari kukamatwa na kuwekwa ndani wakati wowote, lakini maandamano ni lazima kwa Tanzania hadi kitakapoeleweka.

Mbunge mwingine aliyezungumzia maandamano ni Philipa Mturano Viti Maalumu (Chadema) ambaye alisema ukiukwaji wa haki za binadamu ni miongoni mwa mambo yanayochochea uwepo wa maandamano hayo.

Mturano alitoa mfano wa mtoto Juma Hamza (12), ambaye alipigwa risasi na polisi wa doria wa Kituo cha Chang'ombe, Dar es Salaam kwamba licha ya kuhusika kwao na tukio hilo wamemtelekeza.

Mbunge huyo alilinukuu Gazeti hili la Mwananchi toleo la Julai 2, mwaka huu akisema taarifa hizo ni za kusikitisha hivyo kumtaka Waziri Nahodha na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema kuchukua hatua kumsaidia mtoto huyo.

"Haya ndiyo mambo ambayo yanasababisha watu waandamane, leo hii nasema ikiwa mtoto huyu hatapata huduma lazima nitahamasisha wananchi wa Temeke tuandamane hadi kwa waziri na yeye tumchukue twende naye Ikulu ili tukapate hela ya kumtibu mtoto huyu."

"Mtoto huyu picha yake inaonekana hapa kwenye gazeti ni kama amepoteza matumaini kwa sababu ana kidonda kikubwa kinachotoa usaha mwingi, jamani kama ni bahati mbaya kwa nini wanashindwa hata kumhudumia?"

Hata hivyo, kwa upande wake Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde aliponda kufanyika kwa maandamano akisema CCM hakiwezi kutishwa na maandamano kwani ni chama kilichokomaa kisiasa.

Alisema vyombo vya dola vinavyomilikiwa na umma lazima vifanye kazi yake na kwamba lazima wale wote wanaokaidi sheria wachukuliwe hatua.

"Sheria zipo kwa ajili hiyo, kama wewe unaambiwa twende kituoni halafu unakataaa ni dhahiri kwamba polisi watakulazimisha hivyo lazima usukumwe kidogo," alisema Lusinde.

Uchunguzi wa Mauaji
Katika hatua nyingine, Werema amekiri bungeni kwamba Serikali imekuwa dhaifu kwa kutochunguza vifo vya raia ambavyo vimekuwa vikitokea katika mazingira yenye utata na kuahidi kwamba taratibu zinafanywa ili uchunguzi ufanyike.

"Nakiri kwamba tulilegalega kidogo kwa kutofanya uchunguzi wa mauaji yaliyotokea bila kujua sababu zake, lakini tumejiandaa shughuli hiyo itaanza karibuni".

Alisema uchunguzi wa vifo hivyo utafanywa na Mahakama za Korona (Coroner’s Court) ambazo zilikwishaundwa tangu mwaka 2004 kwa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali namba 252 la Julai 16, 2004.

"Jaji Kiongozi kwa kushirikiana na Jaji Mkuu waliwateua mahakimu wote wakazi kuwa makorona (viongozi wa Mahakama za Korona), hivyo watu wa kufanya kazi hii (ya uchunguzi) wapo. Tutatumia taarifa hizi zilizotolewa, ipo ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora na yingine ili kujua nini hasa kilichotokea," alisema Jaji Werema.

Kwa muda mrefu Chadema kimekuwa kikishinikiza kufanywa uchunguzi wa mauaji kadhaa ambayo kinadai kuwa yalifanywa na polisi katika sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Arusha, Tabora na eneo la Mgodi wa Nyamongo mkoani Mara.

Lema, akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani juzi, alihoji sababu za kutoundwa kwa mahakama za uchunguzi wa mauaji hayo.

Alisema uundwaji wa mahakama hizo ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (The Inquest Act) Sura ya 24 na kwamba Waziri Mkuu wakati anahitimisha mjadala kuhusu Bajeti ya ofisi yake, alikubaliana na ushauri wa kambi ya upinzani kwamba Serikali itaanzisha mahakama ya kuchunguza mauaji hayo.

"Kambi rasmi ya Upinzani inachotaka sasa ni kuona utekelezaji. Je, ni lini waziri mwenye dhamana atatangaza uteuzi wa kuundwa kwa mahakama hiyo katika Gazeti la Serikali ili wauaji wahukumiwe? Tunataka uchunguzi ufanyike haraka ili haki itendeke mapema," alisema Lema.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi wa Vifo, Sura ya 24 ya Sheria za Tanzania, kifo chochote ambacho kimetokea katika mazingira ya shaka kinatakiwa kuchunguzwa. Uchunguzi huo ni pamoja ule wa kidaktari ili kubainisha sababu halisi ya kifo husika na hatua ya pili ni uchunguzi wa kimahakama kwa kutumia mahakama ya korona ili kujiridhisha kwamba kifo hicho hakijatokana na vitendo au sababu za kijinai.

Source: Mwananchi.

My Take: Naona CCM (Magamba) Imeshikwa pabaya!!

Hilo haliwezekani kwani siku zote chanzo cha maandamano ni kukosekana kwa haki na wanaoandamana ni wananchi si hy sheria!! Je tanzania kuna haki?

Sijawahi kuona huyu Mheshimiwa G Lema akikosea jambo namuona kama mtu mwenye upeo uliopitiliza kila akisema jambo linakua na mantiki mwanzoni wengi walikua hawajamuelewa vizuri wakadhani nimkurupukaji na mtu wa fujofujo kama alivyo sema waziri mkuu lakini kadri siku zinavyo enda nadhani hata yeye pinda atakua anamheshimu na kumkubari sana na atakua amekoma kumkurupukia nimtu mwenye hoja makini na zenye mashiko heko G Lema endeleza mapambano.

KAULI za kuendelea na maandamamo mpaka kieleweke ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa Chadema zinaonekana kuikera Serikali na sasa inakusudia kuifanyia marekebisho sheria husika ili kuyadhibiti.Maandamano ni miongoni mwa mambo ambayo yalitawala mjadala wa siku mbili bungeni wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, iliyowasilishwa juzi na Waziri Shamsi Vuai Nahodha.

Akichangia hotuba hiyo jana kabla ya kuahirishwa kwa Bunge kwa ajili ya mapumziko, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema mabadiliko hayo ya sheria yatalenga kuzuia bughudha katika maeneo ambayo watu hawashiriki maandamano husika.

"Tunadhani kuna haja ya kurekebisha sheria ili kuregulate (kudhibiti) maandamano katika maeneo ambayo watu si washiriki wa maandamano hayo, hili linawezekana maana nchi kama Ujerumani wamefanya hili," alisema Werema na kuongeza:

"Nimesikia hapa kauli mbalimbali zinazohamasisha maandamano na wengine wanasema tutaandamana mpaka kieleweke na wengine wanasema kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam, tunasema ndiyo ni haki ya kisheria, lakini lazima tuzingatie kwamba wapo wasiopenda maandamano haya."

Kadhalika, Werema alitumia nafasi hiyo kutoa somo kwa wabunge kuhusu mivutano iliyotokea bungeni siku chache zilizopita: “Peaneni nafasi kwa kila mtu na mwenzake na muwe na ushirikiano kama ambavyo mikono ya kushoto na kulia inakuwa na ushirikiano mzuri.”

Jaji Werema aliwaambia wabunge kuwa kazi ya kuwakilisha wananchi inahitaji uvumilivu kuliko kazi nyingine na akawataka wabunge wa pande zote kutumia lugha za kistaarabu wanapo kuwa ndani ya ukumbi wa bunge.

Hata hivyo, alikemea tabia za baadhi ya wabunge kutumia lugha za maneno makali akitolea mfano wa hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi... “Ni kweli Mheshimiwa Lema (Godbless) alitumia lugha kali kidogo.

Hapa naomba ifahamike hivyo, lakini yote mimi ambaye ni Mwanasheria wa Serikali nasema muendelee kuvumiliana na kuangalia lugha za kutumia. Namshukuru sana Mheshimiwa Lukuvi (William), katika hotuba ile alitaka kusimama amzuie Lema, lakini nikamwabia muache aendelee kwani kuna njia nyingi za kuzungumzia hivyo akimaliza utaomba mwongozo.’’

Alisema kuwa katika suala lile yeye (Werema) akiwa Mwanasheria Mkuu, ndiye mwenye dhamana ya kulisemea jambo hilo.

Chanzo: mwananchi

Sheria hiyo itakuwa ni batili na itakuwa inakiuka na kuingilia uhuru wa mwananchi kudai haki zake kwanjia ambayo anaiona ni sahihi. Na ikiwapo sheria hiyo basi itakuwa ndiyo kifo cha ccm, maana tutakuwa tunaivunja ilikuzidai haki zetu. Na ikumbukwe kuwa sheria yeyote ile duniani inayokandamiza haki na usawa inapaswa kuvunjwa mara moja na kufuata ama kutii utu wa mwanadamu.

Sasa Unabii unatimia kwamba JMK ni chaguo la Mungu ili watu waone bila magamba inawezekana!

Hawa wanasahau kuwa sheria zinatungwa na wananchi wenyewe kwa uwakilishi wa wabunge wao na kupata maoni ya wadu ambao ni wananchi.

Halafu magamba wanajisahau sana wanadhani wataendelea kuwa pale ikulu hata uchaguzi ujao. Kama sheria hii itatpitishwa kwa ubabbe kazi yetu ni moja tu ni kuwaweka pemebeni 2015 halafu sheria hiyo iwadhibiti wenyewe waliyoitunga wakati wakiwa wapinzani. Na watakao kuwa madarakani lazima wazitumie shereia zote za ukandamizaji kuhakikisha hawafurukuti. ukweli ni kwamba sheria hii inakuja kutumika kwao wenyewe maana 2015 lazima wang'oke. Chadema haitawapa shida maana wanakubalika hata kama maandamano yatakuwa regulated.

Hivi hakuna mmoja wetu humu anaweza kuipata hiyo sheria inavyotumika huko German na kuibwaga hapa tukasaidiana kuchambua?

Ccm hawajui kwamba kuna siku na wao watakuwa chama cha upinzani,hizi sheria wanazoweka wasije kulalamika

mhh... hiyo sheria ya german sio ndio ile aliyosema hamad rashid ya kuwa maandamano kwa wenzetu huwa yanafanyika usiku..!? oooh.. i remember it.. hahaaha ndoa ya kafu na magamba bana naona baba anakaa na mama kujadili mikakati ya kuiongoza familia yao, baba amepokea ushauri wa mama ana utekeleza, mapenzi mema wanandoa

Today we are engaged in a deadly global struggle for those who would intimidate, torture, and murder people for exercising the most basic freedoms. If we are to win this struggle and spread those freedoms, we must keep our own moral compass pointed in a true direction.
Barack Obama

Change does not roll in on the wheels of inevitability, but comes through continuous struggle. And so we must straighten our backs and work for our freedom. A man can't ride you unless your back is bent.
Martin Luther King, Jr.

We struggle with the complexities and avoid the simplicities.
Norman Vincent Peale

If there is no struggle, there is no progress.
Frederick Douglass

I know where I'm going and I know the truth, and I don't have to be what you want me to be. I'm free to be what I want.
Muhammad Ali
If you can, help others; if you cannot do that, at least do not harm them.
Dalai Lama

An error does not become truth by reason of multiplied propagation, nor does truth become error because nobody sees it.
Mohandas Gandhi

Any people anywhere, being inclined and having the power, have the right to rise up, and shake off the existing government, and form a new one that suits them better. This is a most valuable - a most sacred right - a right, which we hope and believe, is to liberate the world.
Abraham Lincoln

I have a simple philosophy: Fill what's empty. Empty what's full. Scratch where it itches.
Alice Roosevelt Longworth

Have a nice week end.

Hii ndio matokeo ya uchaguzi wa kupindisham matokeo, ila 2015 si mbali kwa maandalizi yanayoendelea. Na tutaandamana kwa ukandamizaji wowote hadi kieleweke.

Similar Discussions

Back
Top Bottom