Sheria ndani ya dini ya Kikristo (Mahakama)

mwiba,

ni kweli kuna matatizo ya uvaaji kwa wanawake na wanaume pia; nguo za kubana au vimini kwa wanawake, suruali za milegezo kwa wanaume na mambo kama hayo. Lakini haya ni mambo ya kimaadili zaidi kuliko mambo ya kushughulikiwa na sheria. Makanisa mbali mbali huwa wanazo taratibu zao za kushughulika na mambo haya na hizo taratibu hutofautiana kutoka kanisa moja hadi jingine. Haya mambo ya uvaaji hayahusiani moja kwa moja na imani bali ni mambo ambayo yanaonekana kuathiriwa na mila na desturi mbali mbali.

Ni kweli kabisa kuna maeneo kuingia kanisani na mini-skirt si issue kubwa na kutokana na mila na desturi za maeneo yale kama hakuna mtu anayekuwa "offended" wanawake huwa huru kujimwaga vile wapendavyo! Hata wanaume vile vile. Kwa ninavyojua, mafundisho mengi ya ukristo huangalia mambo ya ndani zaidi kuliko mambo ya nje kama mavazi anayovaa mtu au chakula anachokula; ambayo mara nyingi hubadirika kutokana na mila, desturi na mazingira ya mahali husika. Haya si mambo ya kushughulikiwa kisheria sana. Hata jamii zinazokaa uchi kabisa wanaweza kuwa wakristo na wakaendelea kusali bila matatizo ikiwa kukaa uchi kwenye jamii husika si tatizo!! Ukristo husisitiza zaidi mambo ya upendo na ukiangalia katika amri kumi za mungu ambazo wakristo huzifuata hadi leo, uvaaji halimo katika amri hizo kumi! Hata wakatoliki ambao wanazo amri sita za kanisa bado katika zile amri sita uvaaji si mojawapo ya amri hizo!

Mambo ya kuhukumu mwizi katika ukristo si masuala ya kiimani hivyo hukumu juu ya wizi (au mambo yote ya kijinai) huchukuliwa kuwa ni mambo ya kushughulikiwa na serikali; wezi hata wakiiba sadaka au mali ya kanisa hushitakiwa katika vyombo vya sheria vya kiserikali.

imesisitizwa tuvae kwa kujistiri. Sasa kujistiri kwa masai, siyo sawa na kujistiri kwa mchaga, mpare na kadhalika. Nakubaliana na wewe kuwa huathiriwa na tamaduni zetu, kama yalivyo majina, kristo alituachia jina moja tu, yaani wakristo. Sasa kuitwa iman, ramadhan, juma, adamu, ntamaholo nk, havina uhisiano wowote na ukristo. Jina ni jina tu
 
Galatia 6:1, inasema
"ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. 2 mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya kristo. 3 maana mtu akijiona ni kitu, si kitu, ajidanganya nafsi yake. 4 lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa wenzake. 5 maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe".

12. Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurtisha kutahiriwa; kusudi wasiudhiwe kwa kusudi la msalaba wa kristo, hilo tu. 13 kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari kuona fahari katika miili yenu. Ff

ukisoma galatia 3:23 inasema.
" lakini kabla ya kuja ile iman tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile iman itakayofunuliwa. 24 hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25 lakini iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi. 26 kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa mungu kwa njia ya iman katika kristo yesu. 27 maana ninyi nyote mliobatizwa katika kristo, mmemvaa kristo".
 
Basi nasema enendeni kwa Roho..... Lakini Roho akiongoza HAMKO CHINI YA SHERIA. Amen.
 
aj.before.after.jpg
Most of us know the Ten Commandments (or at least the important ones), but how well do any of us know all the rules of the Bible and adhere to them?

For one year, A.J. Jacobs carefully studied the Old and New Testaments and did his best to follow every law to the letter. He grew a beard; stopped cursing; stoned adulterers (well, he did what he could) and wrote about the experience in the witty, insightful memoir, "The Year of Living Biblically."
For those of you who can't wait for the Cliffs Notes version of the book to arrive, we asked Jacobs to give us a top 10 list of the weirdest and toughest laws in the

Source: The Weirdest and Toughest Laws in the Bible - Asylum.com
 
God wanted Israelite to maintain the best breed of animals they had.
My be because from the breed they were get more milk an meat.
crossing with the breed they dont know might have degenerated the best breeds of their animals.
Hapa si mahali pake thought.

Kumbe Mungu sheria za ke ni kwa Waisraeli tu?

quote_icon.png
By zomba

Mambo ya Walawi 19:19
Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.

Wewe umejibu ya mifugo tu, na hiyo ya shamba? inakuingia akilini? Na hiyo niliyokuwekea nyekundu? Kuna Mkristo anayeifata?
 
Kwahiyo kaka kwa mtizamo huo, haitupasi sisi watanzania kuwahukumu mafisadi, wauza madawa la kulevya, wauaji wa aribino,etc? kama siyo hivyo basi mtoa mada anataka kujua mfano nini hukumu iliyoelezwa kwa mujibu wa mafundisho ya kikristo kuwa mtu akiiba nini afanywe?

Ndiyo kazi inayobaki kwa serikali lakini haitahusika na kanisa. Kanisa ni la Mungu na Utawala ni wa dunia. Na kwa vile Biblia inatambua uwepo wa serikali za kidunia dunia itabaki ikiwahukumu kulingana na sheria za dunia. Sheria kuu ya Mungu inasubiri mwisho na atatoa hukumu sawa na matendo yako.

Hivyo sisi tunatakiwa kuheshimu hao viongozi na mamlaka zote zinazotuongoza kwa maana zinasemimia kwa mjibu wa Biblia hata kama wanaoongoza si wacha Mungu.

HivyoMkuu, hakunahaja ya kuanzisha mahakama yetu wakati Biblia inajitosheleza na kila mtu anatakiwa kuijua na kuifuata kama ilivyo.

Shukurani
.
 
Back
Top Bottom