Sheria Mpya ya Mafao Haiwagusi Wabunge na Viongozi Wengine Wakubwa?

ymani hilo limeshapitishwa sasa tunaomba solution tufanye nn ili tulizuie?

Katika nchi hii kuna mambo ya ajabu sana, na hili ni mojawapo. Wafanyakazi katika sheria hii mpya wana mambo muhimu ya kujiuliza:

Upitishwaji wa Sheria Hii Mpya
Sheria zote zinazopelekwa bungeni ikiwa pamoja na marekebisho yake, wadau hupewa na nafasi ya kuzijadili na kutoa maoni yao kabla ya kujadiliwa bungeni. Kwa nini mabadiliko ya sheria hayakujadiliwa, yakapitishwa kinyemela bila ya kupata maoni ya wenye mifuko yao? Wamiliki wa mifuko hii ni wafanyakazi, wala si serikali maana serikali haichangii chochote katika mifuko hii.

Uzuri ya Mabadiliko Haya
Wafanyakazi ni watu wenye akili timamu, si punguani wala si watoto kiasi cha kuonekana kuwa kuna watu wengine wanaojua uzuri na faida ya mabadiliko haya zaidi ya wafanyakazi wenyewe. Wafanyakazi wana haki ya kuamua kwa utashi wao juu ya nini kilicho na manufaa kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye, haki hiyo haipo kwa serikali wala bunge au chombo kingine chochote. Kama mabadiliko haya yanafanywa kwa manufaa ya wafanyakazi kwa nini manufaa hayo yasipelekwe kwa wafanyakazi ambao ndiyo wadau wakubwa, wakayadili na kuona faida badala ya kuyapitisha kwa siri?

Wafanyakazi Kunyang'anywa Pesa Yao
Mifuko hii inatunza fedha za Wafanyakazi, si fedha ya serikali. Lakini mifuko inavyoendeshwa hapa Tanzania, imefanywa kuwa ni pesa za serikali na hivyo serikali kuamua kuzitumia pesa hizo kadiri inavyotaka au hata kuiwekea sheria na kanuni bila ya ushiriki kamilifu wa Wafanyakazi ambao ndiyo wachangiaji wa mifuko hii. Serikali imeifanya mifuko hii ndiyo hela ya serikali ya kuendeshea miradi mikubwa ya maendeleo bila kuangalia faida watakayopata wachangiaji wa mifuko hii kwenye hiyo miradi ya maendeleo. Mifuko hii haipo kwaajili ya kuendesha serikali au kugharamia miradi ya serikali, jukumu lake la kwanza ni kuangalia manufaa ya wanachama wake ambao ni Wafanyakazi lakini haki hii ya msingi ya wanachama wa mifuko hii imeporwa na serikali.

Njama za Kuwaibia Wafanyakazi
Faida zinazotajwa na wanaotetea mabadiliko haya ni za kinadharia sana. Katika nchi ambayo ni 6% tu ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi ndiyo walioajiriwa kwenye sekta rasmi, uhakika wa mfanyakazi kuwa katika ajira wakati wote mpaka kufikia umri wa miaka 55 au 65 ni mdogo sana. Wafanyakazi wengi kwenye sekta binafsi wanafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, na baada ya kumaliza mikataba yao hakuna uhakika wa kupata ajira tena. Mathalani mfanyakazi ameajiriwa mara moja kwa kipindi cha miaka 2, ni vipi atanufaika na mabadiliko haya? Na wakati huo atakapofikisha miaka 55 (kama atafika) atapata nini wakati thamani ya shilingi inaporomoko kila siku na huku mfumko wa bei ukikua kwa kasi ya ajabu? Ndiyo maana mabadiliko haya hayana manufaa kwa wanachama wa mfuko bali ni njia nyingine ya kupokonya hela ya mfanyakazi kwa kutumia lugha ya udanganyifu. Kilio cha wafanyakazi wa Tanzania ni kodi kubwa ya PAYEE, badala ya serikali kusikiliza kilio hiki cha wafanyakazi, imezidi kuwapokonya hata kile kidogo walichokuwa nwakipata wamalizapo mikataba yao ya kazi. Baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakitumia mafao haya kuanzishia miradi midogo midogo, wengine huyatumia kwa kujisomesha na wengine hata kuwasomesha watoto wao ambao kwa vipato vyao vya mwezi wanashindwa kufanya hivyo.

Serikali kwa sasa inachukua karibu 20-30% ya mshahara wa mfanyakazi kama PAYE, sasa imeamua kuchukua tena 20% ya mshahara wa mfanyakazi. Hii ina maana sasa serikali itakuwa ikichukua karibu 40-50% ya pesa yote ya mfanyakazi.

Hoja ya Kuiga Mfumo wa Mataifa Mengine
Kati ya sababu zinazotolewa ni kuwa mfumo huu mpya unafuata maelekezo ya ILO na jinsi nchi nyingine zinavyofanya. Undumilakuwili wa serikali ni kama ifuatavyo. Tumekuwa tukiongelea matumizi mabaya ya fedha za umma yanayofanywa na serikali na watendaji wake. Kwa mfano katika serikali kukifanyika kikao wanalipana posho ya malazi na chakula, na posho ya kukaa. Posho hii ya kukaa hailipwi na nchi yoyote iliyoendelea, ukiwauliza kwa nini wasifuate taratibu zinazofuatwa na mataifa mengine, jibu ni kuwa 'sisi ni taifa jingine na hivyo hatulazimiki kufuata taratibu za mataifa mengine'. Mataifa ya wenzetu kiongozi yeyote ambaye taasisi yake inakumbwa na kashfa, lazima mkuu wa kitengo hicho huwajibika, lakini hapa kwetu ukiwauliza kwa nini tusifuate mfumo huo wa wenzetu, tunaambiwa hutulazimiki kufuata mifumo hiyo maana sisi ni Taifa huru ambalo halilazimiki kufuata taratibu za mataifa mengine, na yapo mengi ya namna hiyo. Inapokuja kwenye suala la kumkamua mfanyakazi, ukiuliza juu ya kodi kubwa anayokatwa kwenye PAYE, utapewa takwimu za kodi za mataifa mengine (hapo haielezwi tena kuwa sisi ni Taifa huru lisilohitaji kufuata juu ya nini mataifa mengine yanafanya). Kwenye hili la mifuko ya jamii nalo wafanyakazi wanaambiwa kuwa ndivyo mataifa mengine yanavyofanya. Wakati katika uhalisia mataifa hayo yana uhakika mkubwa wa ajira kwa watu wake, yana umri mkubwa zaidi wa tegemeo la kuishi, sarafu zao ni imara, na mfumko wa bei upo chini sana ukilinganisha na Tanzania. Serikali iache kuendekeza mambo yanayowadhulumu wafanyakazi wakati huo huo ikiyatetea yale yenye kuwanufaisha viongozi wa serikali.

Wafanyakazi Wanatakiwa Kufanya Nini?

Wafanyakazi Wamiliki Mifuko Yao
Wafanyakazi, katika katiba mpya wahakikishe inaingizwa kwenye katiba mpya kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ni mali ya wafanyakazi na itasimamiwa na wafanyakazi wenyewe kwa kupitia vyama vyao vya wafanyakazi. Mifuko hii itakapokuwa chini ya wafanyakazi wenyewe itaweza kufanya kazi kwa manufaa ya wanachama wake, itaweza kuanzisha vitega uchumi ambavyo vitamwezesha mwanachama kuwa na gawio la faida maisha yake yote kwa kutegemeana na kadiri alivyochangia. Kwa kiasi cha pesa kinachopatikana kwenye mifuko hii kuna uwezekano mkubwa wa wafanyakazi wanapoondoka kazini kupewa pesa yao yote waliyochangia, na bado wakaendelea kushikilia hisa katika vitega uchumi kutokana na faida zilizopatikana. Hili litaondoa wajumbe wa bodi na wakurugenzi wanaoweza kuteuliwa kwa manufaa ya kisiasa na kisha wakaamua kuwatumikia waliowateua kuliko wanachama wa mifuko.

Kudai Ripoti ya Mchakato wa Mabadiliko ya Sheria
Wafanyakazi kwa kupitia vyama vyao vya wafanyakazi wadai taarifa juu ya mchakato wa namna mabadiliko yalivyofikiwa. Kama ikigundulika kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi walishirikishwa lakini wao hawakuwashirikisha wafanyakazi, viongozi wote wa wafanyakazi wafukuzwe kwenye nafasi zao. Kama hilo halitawezekana, basi wafanyakazi wote wajitoe kwenye uanachama wa vyama vyote vya wafanyakazi na kuunda vyama vingine vyenye kufanya kazi kwa manufaa ya wanachama wake na siyo kwa manufaa ya serikali.

Njia za Kisiasa
Wenzetu katika mataifa yaliyoendelea, ikifika wakati wa uchanguzi makundi mbalimali huweka bayana matakwa ya kundi lao, na hutoa tamko kuwa, 'sisi kama kundi mojawapo la kijamii, tutamchagua kiongozi au chama kitakachosimamia au kufanya mambo 1) -----, 2) ----n.k.'. Wafanyakazi wa Tanzania, sasa ni wakati wa kuungana na kuachana na ushabiki wa kisiasa na badala yake kama kundi mojawapo la kijamii kuangalia maslahi ya kundi letu. Ifike mahali, kama wafanyakazi wa Tanzania tutamke kuwa, 'wafanyakazi wote tutakiunga mkono chama au mgombea ambaye atashusha PAYE kwa 25% kutoka ilipo sasa na kwa namna yeyote ile mtu asilipe PAYE inayozidi 20% ya mshahara wake. Pili tuseme kuwa tutamchagua kiongozi au chama kitakachokuwa tayari kuiachia mifuko ya kijamii irudi kwa wanachama wake na iendeshwe na wanachama wenyewe.

Wafanyakazi wa Tanzania tukiendekeza siasa na ushabiki wa vyama, wanasiasa wataendelea kuwachezea wafanyakazi miaka yote huku wao wasiozalisha wakijipangia maslahi mazuri na mazingira ya malipo starehe huku mchangiaji mwenyewe akibakia hoi bin taabani.
 
Kama nilivyowahi kueleza katika moja ya mada za JF, wamiliki wa mifuko hii, ambao ni sisi wafanyakazi, hatuhusishwi katika maamuzi ya jinsi ya kutumia fedha iliyopo katika mifuko yenyewe.

Serikali hujitwalia pesa kadri inavyoona kwa vile inayachukulia kama mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Fedha. Kwa ukweli ni kwamba fedha hiyo ni yetu sisi , si ya serikali. Pengine tuulize na swali ambalo tulipaswa kuuliza hapo kale. Je mnafahamu mishahara walipwayo wakurugenzi na uongozi wa juu wa mifuko hiyo?

Mkipata jibu mtatambua kwa nini jambo hili wala haliwanyimi usingizi. Walitoa mikopo ya kujenga UDOM na inavyoelekea mikopo hii hailipiki. Njia pekee waliyoiona ni kusitisha malipo yeyote hadi mhusika afikishe umri huo na hivyo kuutunisha mfuko ili uweze kulipa madai ya hao watakaostaafu.

Hii ni dhuluma kama wengi wanavyoeleza.
 
Sasa huu ni us....nge aisee. Wabunge walikuwa wapi wakati huu upuuzi unapita? au haikusomwa bungeni?

Ndugu yangu idadi kubwa ya wabunge ni wa CCM na wapo pale kwa ajili ya kulinda maslahi ya CCM na sio wananchi. Hapo ndipo umuhimu wa kuwapiga chini wabunge wa CCM 2015 ndipo unaonekana.
kwa swala hili wafanyakazi woote tulikuwa na sababu ya kutoirudisha tena CCM madarakani, lakini utashangaa itakapofika 2015 mimi na wewe tunaolalamika humu tutabadili mawazo kwa kupewa tshirt na kanga tuu.
 
Mimi nadhani ushauri anaopewa mheshimiwa nadhani wanaotoa ushauri wana agenda ya siri mioyoni mwao. Huwezi kuboresha maisha ya mtumishi kwa kuzuia mafao yake. Je hii migodi inayochipua na kwisha utakuja kumdai nani? na haya mashirika yanayoanzishwa kila kukicha ili kupeana ulaji na je yakifa utamdai nani?

Ukiwa huna mshauri mzuri omba ushauri toka jamiiforum utapata ushauri na utaelewa nini kinaendela kuendelea kuwamini washauri wako ndo hii ya kuja kila siku UCHUMI WA DUNIA na midororo wa uchumi wakati wewe si raisi wa dunia! Naomba kama usemavyo wewe shauriwa changanya na zako huku ukiangalia ukweli mfano mzuri katiba vijana wako walikushauri haina shida (mwanasheria mkuu na waziri wa sheria wakati ule na wakasimama kusema haina tatizo) lakini ulipochungulia nje ya pazia ukaona umati wa watu na ukauliza wanataka nini?

Katiba ukajua kuwa ulikuwa unadanganywa kuwa haina shida kumbe kwa nje kuna kelele. Fanya utakayokumbukwa na wananchi si marafiki zako kwani watakutosa mbele ya safari
 
Hivi kwa nini sisi wachangiaji wa mifuko hii hatuna sauti ndani ya hivi vyombo?...Sisi kama shareholders ilipaswa tuwemo katika mabaraza ya maamuzi ya hivi vyombo na hakika hii sheria kandamizi isingefika hapa ilipo,jamani bado hatujachelewa hili swala ni la msingi sana kwetu wachangiaji,

Kama wametuibia kwenye misitu tumenyamaza, kwenye madini tumenyamaza,sasa wameona bora watutie vidole vya macho ili waone machozi yetu.....

Tufanye maamuzi na yatakuwa na nguvu kama yatasimamiwa na vyama vyetu sisi wafanyakazi (wachangiaji)
.....Tunaweza kufanya mass strike kupitia vyama vya wafanyakazi pamoja na vyama vya haki za binadamu ili hiyo sheria iwe reviewed.
 
Mimi siku zote nasema hawa wanasiasa ni wajinga sana na hawajui wapi wanakwenda. Kwanza hawa jamaa wanaotamba na siasa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana ndo maana hata mashuleni tulikuwa tunawakimbiza sana. Utaona wengi ht matokeo yao ya shule si mazuri na waliishia kusoma vitu vya ajabuajabu tu leo hii ndo wanataka kutuongoza na kutuamlia nini cha kufanya.

Wengi wao ni wavivu wa kusoma ila wapiga kelele sana, waganga wa kienyeji na wasomi wachache walioogopa kutumikia taaluma zao na kuamua kuungana na kundi la watu wasiopenda kujishughulisha ktk kufikiri (ndo maana Prof, Doctor, Lawyer, Engineer, etc. hana tofauti na Mganga wa Korogwe kwani wote wanafikiria ktk kipimo kimoja cha kuunga mkono hoja).

Wameshindwa kukusanya mapato migodini, bandarini na kodi nyingine, matokeo yake wanafikiria pombe, sigara, PAYE zitaongoza nchi, wameona ahadi hazitekelezeki na chama kinapoteza dira wakaibuka na pesa zetu za mifuko ya jamii ili warudi madarakani na kuendeleza wizi wao.

Ukisoma ule mswada utaona kuna kiswahili na kiingereza, sasa kwenye kiingereza wanaandika mtu atachukua michango yake upon retirement na juu mwanzoni mwa paragraph wamedifine retirement to be 55 or 60yrs. Hakuna sehemu wamesema mtu haruhusiwi kuchukua pesa yake akiacha kazi kabla ya umri wa kustaafu ila hiyo definition hapo juu ndo inayoonekana, waandaaji wa mswada walificha hilo neno na baada ya wabunge wetu kutoliona na kuelewa wao wamelichukua na kulitolea ufafanuzi sasa mswada ukiwa umepitishwa na Bunge tayari, hata hao wabunge ukiwauliza watakwambia hicho kitu hawakijui ila walipitisha bila kujua.

Na sehemu ya kiswahili wameandika utachukua pesa yako baada ya kustaafu ila hawajaandika maana ya kustaafu. Sasa km mimi naacha kazi na kukurudishia kadi yako nikiwa na miaka 35 inamaana mimi sio mwanachama wako na sina uhusiano wowote na wewe, niache niondoke zangu ya nini unataka kukaa na pesa zangu wakati mimi nazihitaji na sijakuomba unitunzie? Kwani wao ni bank mpk wang'ang'anie pesa zetu? Mbaya zaidi huyu rais na timu yake muda wao ndo umekwisha hivyo sasa inakuwaje wao waamue kuliingiza taifa ktk mgogoro mkubwa hivi na wao wanaondoka?

Wanadanganya eti ni kwa manufaa ya wanachama, Mkapa alikuwa hana akiri aliyeanzisha mifuko yote hii ila Kikwete ndo clever wakati kila mtu anajua uwezo wa Ben Mkapa? Unaacha kazi na 40yrs au less na bado ni kijana una nguvu ya kutosha ila kupata pesa yako unasota sana kwenye hizo ofisi mpk na rushwa itembee sasa ukiwa na 55 or 60 na unaishi mikoani au hata hapa Dar kila siku uende ofisini kudai pesa zako si bora uwaachie tu.

Tumeona wazee wa East Africa mpk mabomu yametembea sasa sisi si risasi watapiga kabisa? Mpk mimi nafikisha 55yrs Kikwete na hawa wazee wenzake watakua wamekufa wote sasa hata mkiamua kushtaki nani atawalipa? Hapa mmechemka na hiyo sheria haitofanya kazi kwani Bisimba na TUCTA wanaenda mahakamani so mpk kesi iishe ndo sheria itaanza km kisingizio chenu cha siku hizi cha "KESI IPO MAHAKAMANI" kinavyosema.
 
hata me nashangaa hawa wawakilishi wetu walikuwa wap? na mpaka leo siku ya nne hakuna hata mmoja aliyelitplea ufafanuzi hapa...Hakika wametusaliti na wanastahili adhabu...
Kaka mi ndio mana sipigi kura us.....nge mtupu, wote wapo kwa maslahi yao ukiona wanapiga kelele ujie kina kitu kinawabana na wao lakini vinavyotugusa sisi direct ambavyo havi influence maisha yao wanapiga kimya, jiulishe mbunge gani asiejua hili linatuumiza?
 
Yaani inasikitisha sana. Suala hili likiachwa bila kupigiwa kelele na ikiwezekana maandamano makubwa watanzania watazidi kuwa masikini na kunyonywa kutokana na jasho kubwa walilovuja wakati wakifanya kazi.

Leo anataka stahiki na haki yake ya pesa aliyokuwa akikatwa anaambiwa asubiri hadi miaka 55 au 60! Upuuzi mkubwa! Unyonyaji mkubwa!

Ninavyojua ni kwamba pesa hizo wanazokata hazipo, wamepeleka kwenye majengo wanayoporomosha au walipeleka katika kampeni za uchaguzi ndo maana wanatumia ujanja ujanja. Watanzania tusikubali.
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Wakuu serekali yetu sasaivi imeshazoea migomo ili ipige watu ikiona hakuna mgomo haijisikii raha sasa hapa wameona madaktari wametulia, wakachokoza walimu wameona kimya sasa wamegusa wote kwa ujumla, mi naona wanatupima nguvu au wanataka vyombo vya usalama vifanye mazoezi mana wamechoka na amani na silaha wanazo nunua hazifanyi kazi, Naomba serekali ituache ictuchafue mana imegusa pabaya, binafsi sijui lengo lao ni nini.
 
Mkuu pesa ni ile ile hata kama utafikisha miaka 55 baada ya miaka 40. Tena unapewa pesa yako bila riba ikiwezekana utaipata baada ya kufurumishiwa mabomu ya machozi na virungu vya FFU kama wastaafu wa East African Community.

Na kwa jinsi ilivyo by the time unapewa hiyo hela itakuwa na thamani ya shs 15,000/= huko mtaani.. na wewe umeisubiria for 30 years!!
 
Wana JF,

Nimedokezwa kuwa sheria mpya ya mafao ina kifungu cha 43 (6) ambacho kinasomeka kama ifuatavyo:

''This act shall apply to a person or employee employed in the formal or informal or self-employed in the mainland Tanzania and shall not apply to a person who has been insured or registered under any other law.''

Alichonieleza mdokezaji wangu ni kwamba kifungu hiki kinawaondoa wabunge na viongozi wengine wa juu katika ile kadhia ya kusubiri hadi miaka 55 au 60. Kwa maana hiyo, wabunge kwa mfano, wakishamaliza ile miaka 5 watachukua pesa zao kama kawaida.

Kuna mwenye kujua zaidi juu ya hili?
Hapo kwenye red ina mana hii sheria haiwabani wa Zanzibar?
 
ALAANIWE MTU YEYOTE AMBAYE AMEHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA KUFANIKISHA SHERIA HII DHARIMU NA KANDAMIZAJI KWA WANYONGE,sasa naamini kuwa sikio la kufa halisikii dawa yaani kila kukicha serikali inawaza namna ya kuanzisha mgogoro mpya badala ya kutatua migogoro iliyopo. Hii ndiyo shida ya kuishi kiujanjaujanja mwisho wa siku unajikuta umejidanganya mwenyewe. Siku zote huwa najiuliza juu ya wasomi wenye madalaka katika nchi hii kama wamesoma ili wasaidie maskini wa Tanzania au wamesomea kuwanyonya maskini,mfano mtu anaamua kuuza nyumba zote za serikali wakati serikali hiyohiyo ndiyo ilizijenga,au mtu aliyependekeza kuongeza kodi katika mafuta ya taa ambayo ndugu zake kijijini kwao ndio wayotumia INATIA KICHEFUCHEFU
 
Mimi nina miaka 30 nimeajiriwa kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya mkataba wangu kwisha naweza kudai mafao yangu ya NSSF/PPF au itabidi nisubirie mpaka nifikishe miaka 55 au 60.Naomba jibu kwa wanaolewa humu.
 
Mimi nina miaka 30 nimeajiriwa kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya mkataba wangu kwisha naweza kudai mafao yangu ya NSSF/PPF au itabidi nisubirie mpaka nifikishe miaka 55 au 60.Naomba jibu kwa wanaolewa humu.

Habari ndo hiyo mkuu! Kwa mujibu wa sheria hii utalazimika kusubiri hadi ufikishe umri wa miaka 55.
 
Wananchi wasitegemee maendeleo kutokana na wawakilishi wao kama mambo yeneywe ndiyo hivi
 
Mi roho hapa inauma saaaaaaaaaana. Nimeacha kz muda sio mrefu (Mwezi wa 6) maana bosi wangu alinifanyia ndivyo sivyo. Mpaka sasa nachanganyikiwa maana nilijua ningepata kamtaji kuweza kusukuma maisha.

Sasa hivi niko njia panda - ada ya shule nadaiwa, mikopo ya benki n.k. Je Kikwete na serekali yake wamedhamiria kuniuwa???

Nani atakuwa sauti ya sisi wanyonge. Ama ndo wanataka niwe kibaka au jambazi sugu! Mimi ninauchungu!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom