Sheria mpya udhitibi vyombo vya habari: Je CDCM na Kanisa Katoliki wamo?

ByaseL

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
2,225
247
Serikali inaanda rasimu ya sheria ya kudhitibi umuliki wa vyombo vya habari. Katika mapendekezo ya awali ya sheria hii yanalenga kuzuia mtu (au taasisi?) mmoja kutomiliki zaidi ya chombo kimoja cha habari. Kwa mfano kama mtu anamiliki magazeti hataruhusiwa kumili radio au Television. Hivyo hivyo ukimiliki kituo cha television hutaruhusiwa kumiliki magazeti, n.k. Mapendekezo haya yamelalamikiwa sana na wadau kwamba yanawalenga watu wawili hususan Bwana Mengi na Mhe. Antony Diallo ambao wanamiliki magazeti, radio na vituo vya television. Swali langu ni: Je sheria hii itawagusa Chama Tawala cha CCM ambacho kinamiliki Gazeti la Uhuru na Radio Uhuru pamoja na Kanisa Katoliki linalomiliki magazeti ya Kiongozi na Tumaini Letu, Radio Tumaini na Tumaini Television? Wenye kujua undani wa rasimu hii mpya ya udhibiti wa vyombo vya habari watufafanulie tafadhali
 
Kwanini ulichanganye Kanisa Katoliki na CCM kwenye umiliki wa vyombo vya habari zaidi ya kimoja?
 
Je sheria hii itawagusa Chama Tawala cha CCM ambacho kinamiliki Gazeti la Uhuru na Radio Uhuru pamoja na Kanisa Katoliki linalomiliki magazeti ya Kiongozi na Tumaini Letu, Radio Tumaini na Tumaini Television?


Mlengwa mkuu wa rasimu hii bila shaka unamfahamu, ukijaribu kutafuta wengine utaiua hoja iliyo mbele yetu. Mbona huulizi kama serikali yenyewe nayo itaguswa kwa kumiliki TBC Taifa, TBC One, Daily News na HabariLeo?
 
Back
Top Bottom